Habari zenu wakuu mbalimbali... E bwana nipo hapa Riverside ubungo darajani kituo cha daladala...zimepita kama dakika 10 hivi kuna gari aina ya Rav4 imepita hapa kituoni na ikapunguza mwendo kiasi bila kusimama...Cha ajabu niliona mwanamama mmoja kupita mlango wa mbele wa abiria katoa nazi na kuitupa chini kwa nguvu sana hatua ambayo ilipelekea ile nazi kupasuka hapa kituoni na kisha gari ile ikaondoka kwa kasi sana.
Naomba nieleweshwe kwa wajuzi wa haya mambo au experience yeyote juu ya hili....hii ina maana gani.