Hii mboga inaliwa? Msaada wenu!

Ukisikia mchicha pori orijino ndiyo huu sasa. Majani yake yana faida lukuki ikiwemo kuongeza nguvu za kiume, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa sumu mwilini, kupunguza cholesterol, kuimarisha uoni wa macho na faida nyingi nyingine.

Hizo mbegu huwa zinavunwa na kusagwa na huuzwa ghali sana. Huwa zinachanganywa na ulezi pamoja na unga kidogo wa mbegu za maboga kupikia uji ambao unasemekana unafanya kazi vizuri zaidi kuliko viagra!
 
Kula majani hayo ni mboga safi sana na salama. Kuuogopa ni sawa na kuogopa mtama mwekundu kwa rangi yake hali mababu zetu huko Kishapu, Bariai, Maswa, Igunga n.k wamekula na walikuwa imara zaidi ya wala mahindi ya panna, zam seed n.k
 
Mpwa utafanya watu waufyeke Kwa matumiz πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
ni miongoni mwa mboga mujarabu sana huku kwetu,
yote nyekundu na isiyo nyekundu tunaitumia barabaraπŸ’
asubuhi ni mboga ya faster fasta sana, chapchap na kiporo cha kuchoma au kupasha, na mchana na ugali mujarabu wa dona na maziwa mtindi πŸ’

wewe acha kabisaa mimi na wanainchi wangu ni bam bam kwenye misosi....
 

Mhala sana shimba? Huo sio mgagani, bali ni mchicha pori mwekundu kama ulivyo mchicha pori wa kijani. Mgagani naujua vizuri majani yake machungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…