Hii migomo ya wafanyabiashara: Makamu wa Rais awe tu Rais wa mpito asimamie uchaguzi mwingine

Hii migomo ya wafanyabiashara: Makamu wa Rais awe tu Rais wa mpito asimamie uchaguzi mwingine

Doslamari

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
4
Reaction score
1,499
Rais ni cheo kikubwa sana yenye madaraka makubwa sana mwenye kupata hiyo nafasi lazima aihenyee ndio atakuwa na wivu na hiyo nafasi. Siyo kupewa tu na katiba.
Migomo hii ni udhaifu wa Rais wa sasa, Rais anachezewa na wahalifu wakwepa kodi. Mpaka leo hajatoa kauli kisa "chura kiziwi", ndio kusema hasikii yanayoendelea nchini? Namwomba asifikishe nchi yetu walikofikia wakenya, eti mpaka raia anaingia bungeni na kuchukua utukufu wa bunge(siwa). Nchi gani ya hovyo km ile, kila mtu mjuaji. Raia anaingiaje mazingira ya bunge? Vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi? Hapana hiyo siyo demokrasia. Jifunzeni kwa Kagame na Museveni. Yaani natamani sana nchi hii ipate Rais km Kagame, nchi haitakiwi ijaribiwe na kundi lolote ktk jamii. Wananchi lazima watii serikali iliyoko madarakani, hilo siyo ombi ni lazima. Km kuna changamoto watafutwe wawakilishi wawasilishe kwa njia sahihi.
Samia alikuwa makamu wa Rais, pengine hakujiandaa kuwa Rais tunamlazimisha tu, bora akae pembeni tumchague ambaye amejiandaa kuwa Rais maana ataomba mwenyewe ridhaaa. Mila, desturi yetu ibaki km ilivyokuwa, heshima yetu kimataifa inajulikana. Hao kima wachache waangamizwe kwa maslahi ya Taifa
 
Kitendo cha kumteuwa Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa fedha na January Makamba kuwa waziri wa umeme ndio tangu siku hiyo nilimuona huyu mama hayupo serious, na kwa bahati system imejaa machawa tu hamna kitu.

Huwezi kuacha Wataalam kama Dr Kimei halafu eti umteuwe Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa fedha hii ni dharau na matokeo yake ndio haya wanajitungia kodi za hovyo tu zinazalisha migomo.
 
Mwigulu ni hovyo sana yani kazi yake kubwa ni kubuni kodi hana cha ziada
 
Kitendo cha kumteuwa Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa fedha na January Makamba kuwa waziri wa umeme ndio tangu siku hiyo nilimuona huyu mama hayupo serious, na kwa bahati system imejaa machawa tu hamna kitu.

Huwezi kuacha Wataalam kama Dr Kimei halafu eti umteuwe Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa fedha hii ni dharau na matokeo yake ndio haya wanajitungia kodi za hovyo tu zinazalisha migomo.
Siku ukijua kwanini Kimei hapewi hata unaibu utaheshimu sana hayo maamuzi. Huyo mzee wenu wa Vunjo hafai hata kidogo.
 
Fisiemu wame amua kuto wapa attention na karibu fisi wata shinda hili jaribu ..Round hii wafanyabiashara mme yakanyaga badilini technique

Ila kusema kweli Rais mwanamke hapana atukua tayari kwa hili ni weak sana
 
Unaposema Kenya vyombo vya usalama vilikua wapi, Kuna muda hata na wao wanachoshwa na hizo Kodi, alafu tumia busara, Hawa waajiriwa wa vyombo vya usalama hawakai kambini Wala maporini, wanakaa katikati ya raia, na familia zao zinakaa na raia, sasa we mchana jitie kimbelembele kuua watu usiku ukiwa na mke na watoto wako Raia wakija kukusalimia ndo utapata akili
 
Naona kama Rais anaweza!
Shida wateule na washauri wameshika zaidi vitovu vyao kuliko nywele.
Hili genge limeishika nchi pabaya.
 
Mtei ndio Gavana wa kwanza na alimshauri Nyerere sera zake za kiuchumi zinakwenda kuingiza nchi shimoni.

Kama tatizo ni uchaga wa Dr Kimei lakini kwa Mwigulu hapana.
Enzi za Nyerere uzalendo ulikuwa mkubwa sana kwa mtu wa kabila lolote lile,hawa wa sasa wenzake na kina Mbowe huwezi kuwapa imani asilimia mia.
 
Naona kama Rais anaweza!
Shida wateule na washauri wameshika zaidi vitovu vyao kuliko nywele.
Hili genge limeishika nchi pabaya.

..wenzetu wanapochagua kiongozi mwanamke huchagua mwenye mvuto. Tulipaswa kujifunza toka kwa Croatia.

..Ukiacha kukosa mvuto, hana hoja kabisa. Hawezi kuzungumza jambo lolote la maana bila kuwa ameandika, na hilo pia linaweza kumpa shida.
 
Back
Top Bottom