Hii misemo ina Tija kwa Taifa?

HP1

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2012
Posts
3,362
Reaction score
878
Kuna misemo mingi ya kiswahili ambayo tumeipokea kutoka kwa mababu na viongozi wetu wa kitaifa. Misemo mingine imekuwa inatafsiriwa au imekuwa ikileta maana tata. Tujaribu kuitazama kiundani nakuona kama bado ina tija kwa taifa hili ama la, tukiwa tunatoka mifumo ya analogia na kuingia digitali.

Misemo yenyewe ni mingi, baadhi yake ni kama ifuatavyo
  1. Pole pole ndio mwendo
  2. Aliye juu mngoje chini
  3. Mbio za sakafuni huishia ukingoni
  4. Haraka haraka haina baraka
  5. nk
Je hii misemo inajenga busara au inadumaza akili za wanaotaka kuleta maendeleo ya haraka katika taifa hili?
 
Ukiichunguza misema/methali za kiswahili kila moja ina nyingine ambayo ni oppositi yake kwa mfano mvumilivu hula mbivu opposite yake ni ngoja huumiza matumbo, polepole ndio mwendo opposite yake ni chelewa chelewa utakuta mwana si wako, mbio za sakafuni huishia ukingoni opposite yake ni mgagaa na upwa hali wali mkavu...
Kwahiyo unaangalia tu mazingira gani unahitaji methali gani na kuitumia. Kama ina tija au lah inategemea na jinsi mtumiaji atakavyokuwa makini kwenye kuchagua mazingira muafaka...
 

Asante mkuu kwa mchango wako. Nchi yetu ina wanafalsafa wengi kama ZeMarcopolo na wengineo, nafikiri ifike mahali tu tuwe na misemo ambayo itakuwa ni positive zaidi yenye kuhamasisha kuleta maendeleo ya Taifa letu changa lenye zaidi ya miaka arobaini.
 
Huo msemo wa 4 una tija sana tu!
-Haraka inafanya watu wapasuliwe vichwa badala ya miguu!:smile-big:
 
Huo msemo wa 4 una tija sana tu!
-Haraka inafanya watu wapasuliwe vichwa badala ya miguu!:smile-big:

Mkuu, nchi ipo nyuma sana kiuchumi, kwa nini tusifanye haraka kuiendeleza?
 
Mkuu, nchi ipo nyuma sana kiuchumi, kwa nini tusifanye haraka kuiendeleza?
na hao tuliowapa dhamana ya kuongoza upatikanaji wa maendeleo hayo kwa haraka wenyewe wanaharakisha kujipatia maendeleo yao tena kwa harakaharaka na kutumia shortcut (ufisadi)..isingekuwa hii harakaharaka yao ya kutaka maendeleo yao binafsi kwa haraka pengine tungekuwa tupo mbali sana kimaendeleo..
 

Hujamsoma Zemarcopolo vizuri. Na mimi niliwahi kusema hili.

Hamna msemo ulio positive au negative. Inategemea na utakavyotumiwa.

Kijana anayeanza kazi na kutaka utajiri wa haraka anaweza kuambiwa "haraka haraka haina baraka" na msemo ukawa na mafunzo mazuri.

Mama anayechelewesha chakula kwa watoto wake kiasi watoto wakose lishe kwa muda muafaka akitumia msemo huo huo atakosea. Ila hapo inabidi apewe msemo opposite wa "Ngoja ngoja huumiza matumbo".

Kwa hiyo issue si msemo. Ni matumizi ya msemo. Kujua wapi utumike msemo upi na wapi usitumike upi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…