Hii misimamo ya kichama kuhusu serikali mbili au tatu maanake nini?

Hii misimamo ya kichama kuhusu serikali mbili au tatu maanake nini?

bbahati2012

New Member
Joined
Feb 6, 2013
Posts
3
Reaction score
1
Bunge maalumu mipaka yake inakomea kwenye mamlaka ya wananchi kwa sababu wananchi ndio wenye katiba na ndio wlioto maelekezo kwa Bunge maalum juu ya Katiba waitakayo.

Pamoja na ukweli huo,nasikitika kusema hapa kwamba vyama vya CCM na CHADEMA, tayari vinakwenda kinyumena
uhalisia wenyewe. CCM imeweka msimamo kwa wajumbe wake kung'ang'ania muundo waMungano wa Serikali mbili.

CHADEMA nao wameweka msimamo na wabunge wake wa kuwana muundo wa Muungano wa Serikali tatu. Vyama hi
vivimejipamadaraka makubwa kuliko madaraka waliyonayo wananchi wao.

Vyama hivi vinapaswa kuelewa fika kwambamaoni yaliyotolewa na wananchi sii ya kichama au kiitikadi. Mng'ang'anio huu wa
muundo wa Muungano wa Serikali mbili au tatu unaosimamiwa na nyama husika ni wa kijingakwakua Tume ya warioba haikwenda kwa wanahama wanaa kuchukua maoni ya Wana CCM au wanaCHADEMA wengine.

Wala wakati tunatoa maoni yetu hatukuulizwa tunatoka chama gani, vilevile takwimu za wliochangia rasimu ya katiba ambayondio dira kuu ya katiba mpya, haikuonyesha waliochangia wanatoka chama gani chasiasa.

Napenda tuu niwafahamishe wabungewetu hawa wa Bunge la katiba kwamba, ndani ya rasimu hii ambayo ndio sababu yawao kuwepo ndani ya bunge la katiba yapo mambo mengi ambayo yanahitajikujadiliwa na kufikia muafaka.

Mnataka sisi wananchi tuwaelewe kwamba wanaletamalumbano yasiyoisha ili waendelee kupata posho za vikao? Katika hili naona wapowabunge ambao wanahiyari vikao viahirishwe kila siku alimradi posho inaingia.
 
Binafsi nasema kosa lilifanyika kwa kujaza wanasiasa wengi kwenye bunge hili! Ccm wanautumia uwingi wao vibaya kwa kukanyaga haki za wajumbe walio wachache ndani ya bunge la katiba. Ingawa cdm nao wamo kwa upande wao, lakini ccm wazidi zaidi.
 
chadema wanasimamia msimamo ya watanzania waliowengi ikumbukwe chama cha demokrasia na maendeleo kilizunguka nchi nzima kukusanya maoni ya watanzania, pia rejea kamati ya warioba inasemaje juu ya swala la serikali tatu ama mbili...
 
Vyama hivyo vinaonekana vimekosa sera, ndiyo maana wanataka kulazimisha kuwasemea Watanzania zaidi ya milioni 45, wakati wao kwa ujumla wao hawafiki hata milioni 7!
 
Back
Top Bottom