Hii nchi tushukuru mchina laasivo Panya Road wangekua mara 7 ya waliopo sasa hivi

Hii nchi tushukuru mchina laasivo Panya Road wangekua mara 7 ya waliopo sasa hivi

Mr Chromium

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2020
Posts
2,761
Reaction score
3,835
Kilichoandikwa hapa ni mawazo binafsi haina uhusiano na siasa wala haiwakilishi upande wowote/kundi la watu!

Tanzania tunaelekea milioni 60 kwa makadilio (sensa itajibu ufasaha). Lakini katika miaka yote zaidi ya 50 na kenda ni kama serikali au nchi haikujipanga na ongezeko hili la watu.

Mwaka 1961 tulikua milion 10 (10,337,891-macrotrent.net) so katka kipindi chote idadi ya watu imekua mara 6 zaidi ya ile tuliyokua nayo!

Hata hivo nchi haikujipanga na ongezeko hili au haikufikiria kama tutaongezeka au ilijua lakini ilipuuzaa au haikutilia umakini!

Kwanini?
Nchi yyte inabidi iwe na mipango kabambe ya kukabiliana na ongezeko la watu na kutatua matatizo kama Ajira, Miundo mbinu, huduma za jamii maji, umeme na shule.

Ukiangalia leo ongezeko la viwanda ni dogo sana ukilinganisha na tulivokua navyo enzi za uhuru .Hapa siongelei viwanda vidogo vya mikono vya kuajiri watu watatu naongelea vile viwanda kama vya Textile, usindikaji nyama, viwanda vya sukali, viwanda ambavyo vinauwezo wa kuajili watu hata 300 na kuendelea.

Swali je vijana wanaohitimu na wanasiosoma wote maelf na maelfu tunawapeleka wapi??

Je, nchi inazalisha ajira za kuweza kukabiliana na ongezeko la vijana mtaani? Tuna viwanda vya kuwapeleka kupunguza wimbi na vijana wasio na kazi ambao baadae wanageuka kua al shabab?au panya road!


UKITAKA KUONA HILO ANGALIA WANAO ENDESHA BODA NI WANGAPI? hesabu tu hata mtaani kwako?
kwa mkoa ? kwa nchi nzima?

Utagundua ni vijana wengi sana ambao kabla ya hapo walikua mtaani!

Na hapo hao ni baadhi tu ya hao kuna walioko bado mtaani? wana kwa kwenda?

Asingekua mchina kuleta au kuzalisha mapiki piki ayo kwa bei ndogo kuleta huku kwetu athari ya uhalifu kutokana na vijana waliopuuzwa ingekuaje?

Sijui ila huwa nawaza!! Nikisikia panya road najiuliza hao ni kiasi tu cha vijana waliopo mtaani ingekua na boda hamna hizi nchi zingegeuka somalia.

Kama ushawai waza hili swala GONGA LIKE!
 
Hali ngumu ya maisha na ukosefu wa ajira utasabisha uhalifu wa hatari sana huko mbele.

Yaani mtashtukia tunakuwa kama Nigeria au Gangs za Latina america na mexico au nchi inakuwa na vikundi vya waasi wanaotaka kuipindua serikali. Mtu ukishakuwa na njaa unakuwa zaidi ya mnyama.

Yaani nchi itakuwa hatari mpaka watu wata. Au Basi !

Inabidi ishu ya ukosefu wa ajira itatuliwe.
 
Mtaani boda boda ni nyingi kuliko idadi ya watu.ila hii nchi kweli hatujajipanga hivi mnajua hapa hapa mjini kuna shule za msingi ina wanafunzi mia tatu wanasoma darasa moja.

Aiseee ni aibu nzito.
 
Mtaani boda boda ni nyingi kuliko idadi ya watu.ila hii nchi kweli hatujajipanga hivi mnajua hapa hapa mjini kuna shule za msingi ina wanafunzi mia tatu wanasoma darasa moja.Aiseee ni aibu nzito.
Sio Bodaboda tu, na Sasa hivi sehemu nyingi kuna changamoto kubwa ya biashara kuwa nyingi kuliko wateja.

Halafu kila mtaa, kila kona, kila sehemu, kila uchochoro kuna fremu kama ugomvi 😂😂. Sasa wafanyabiashara wanakuwa wengi kuliko wateja. Sasa maana yake wafanyabiashara ama wabadilishe biashara au waanze kufanyiana fitina.

Hiyo ni changamoto kubwa kwa sasa Tanzania. Na inaleta migogoro sana.

Mfano: Migogoro kati ya wafanyabiashara wa maduka na machinga, mgogoro kati ya daladala na bajaj, migogoro kati ya mama ntilie na watu wa migahawa, migogoro kati ya coaster na mabasi ya mikoani, migogoro kati ya mfanyabiashara mmoja na mwenzake. N.k
 
Mtaani boda boda ni nyingi kuliko idadi ya watu.ila hii nchi kweli hatujajipanga hivi mnajua hapa hapa mjini kuna shule za msingi ina wanafunzi mia tatu wanasoma darasa moja.Aiseee ni aibu nzito.
Umenikumbusha shule ya msingi kibamba shule...

Aisee kule ni kawaida kukuta darasa lina wanafunzi 1000
 
Mtaani boda boda ni nyingi kuliko idadi ya watu.ila hii nchi kweli hatujajipanga hivi mnajua hapa hapa mjini kuna shule za msingi ina wanafunzi mia tatu wanasoma darasa moja.

Aiseee ni aibu nzito.
Umaskini umewapiga watu mpaka kwenye kope lakini ndio kwanza viongozi wetu wanaongoza kwa kutembea kwa magari ya kifahari.
 
Hii nchi ni ya kukaa upandeupande. Bomu la ukosefu wa ajira litalipuka muda wowote ule.
 
Tanzania bado kwa asilimia zaidi ya 90% vijana hawajitambui, kwa hiyo mabadiliko yoyote chanya ni ngumu kutokea kwenye jamii ya namna hii.
 
Mawazo yako yako relevant kabisa na hali halisi kwa kweli umeona mbali, kwa sasa ukiachana na bodaboda hata ukiangalia status za watu wetu wengi biashara ni udalali wa magari na simu kwamba wauzaji ni wengi kuliko wanaonunua na ndo maana kweny biashara wanaowin ni wachache mno.
 
China ilianzisha sera ya kila familia izae mtoto 1 tu (1 child policy) kuanzia mwaka 1980 mpaka mwaka 2015. Ili iweze kuleta na kupanga maendeleo. Tanzania tunafyatua tu tunasubiri mwingine atasomesha na kutoa ajira

 
Mchina kaleta bodabodda ambazo zimeleta ajira kwa vijana wengi sana
 
Back
Top Bottom