Hii Nchi Watu Wanafuatilia Umbea Kuliko Mambo Muhimu Ya Nchi

Hii Nchi Watu Wanafuatilia Umbea Kuliko Mambo Muhimu Ya Nchi

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
My Country People ni wajinga sana, Post mitandaoni zenye engagement kubwa au kufuatiliwa zaidi ni zile za umbea, sijui Ex wa Mobeto kafanya nini kwenye harusi ya Jux, Sijui Mke wa Jux ana Mimba. Kwa kifupi ni zile story ambazo husipozijua haikuathiri na hata ukizijua haikusaidii chochote kama Mwananchi.

Wakenya hapa ndipo walipotuzidi, Wakenya wengi sio watu wa umbea, ni watu wa kazi kazi, hawana muda na kufuatilia sana maisha ya wasanii na watu maarufu au connection za ngono. Amini nakwambia hii Harusi ya Jux ingefanyika Kenya hisingepata attention kubwa kwa sababu kwao maisha yako ni maisha yako, japo watataka kujua hila sio kwa ukubwa huo.

Hapa nimekaa na demu mmoja najaribu kumuwekea topic za kisiasa kuhusu hotuba ya Rais na mambo mengine ya kisiasa ambayo kimsingi ndio yanaaksi mustakabali wa maisha yake, yeye anaanza kuniletea story za Jux na mke wake na wanaijeria walioudhuria, yani umbea anaufuatilia utafiri ndio chakula chake. Yani mpaka unapata hasira lakini kwa sababu nami kipindi nilivyokuwa mdogo sikuwa napenda siasa zaidi ya movie, cartoon, games na mziki inabidi tu umuelewe.

Wanawake wengi bongo sio watu wa siasa kwa sababu hobby yao ni umbea kwa kiasi kikubwa, na vijana wengi wa kiume hawafuatili siasa kwa sababu ya Kubeti, kufuatilia mipira, pombe, starehe na mambo mengine yasio na tija.

Watu wengi wanafuatilia siasa kwa asilimia kubwa ni Watu wazima sana utakuta kuanzia miaka 30 na kuelendelea hasa wanakuwa wanaume kwa sababu sheria nyingi za Nchi zinakumbana na wanaume kwenye mihangaiko yao ya kutafuta ridhiki.

Nawasihi wananchi wangu, Siasa na mambo ya Nchi tuyape kipaumbele kama tunavyovipa kipaumbele vitu vya kijinga, kwa sababu siasa ndio inaendesha maisha yako. Hizo nauli za daladala, bei za mazao, na kila kitu kwenye mzunguko wako wa maisha kinaamuliwa na siasa na kupitia siasa ndio tunapata hao viongozi wa kutuongoza na kutunga sheria zitakazo kuwa juu yetu
 
Mienendo ya watanzania walio wengi imewarahisishia watala katika milioni 60 ninaamini wapumbavu ni takribani milioni 50
 
Hapo Kwa wakenya kwamba hawafatilii umbea huo ni uongo takatifu sema wa Kenya hawapend ujinga kweny mambo ya msingi haswa siasa
 
Mipasho ya leo si umeisikia.
Hivi mini nina akili sana au ni watu hasa walio shika mpini kujitoa ufahamu.?
 
Ukiona mtu ni shabiki wa simba na Yanga, ccm na chadema lazima awe na matatizo ya akili na n mpumbavu
 
Back
Top Bottom