Hii ndio 2025 Uliyoisikia

Hii ndio 2025 Uliyoisikia

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
276
Reaction score
460
Naam huu ndio mwaka wa hekaheka, waswahili husema mtoto hatumwi dukani.
Kama ulikuwa unasikia "tukutane 2025" basi mwaka wenyewe ndio huu.


Kuna mtu aliwahi kusema "mwaka wa kula hela za wajinga" mwaka wenyewe ndio huu.
Mwaka wenye maigizo na vichekesho, mwaka ambao wanyonge hutukuzwa kweli kweli na kufanywa ngazi au daraja ili wenye uwezo wapande kileleni wakale biriani na kuku kwa mrija.


Mwaka wenye kila aina ya hujuma, uganga wa kuku mweupe, maombi ya maji na mafuta, sadaka chafu na harambee za kupangwa.


Mwaka wa vilio na vicheko, uongo na uwazi, mema na mabaya huu ndio ule mwaka uliousikia bwana.


Mwaka wa unafiki wenye matabaka na urafiki wa muda mfupi kama mapenzi ya jogoo na tetea.


Mwaka wenye pesa nyingi haramu, chache zilizo safi, mwaka wa kujitoa muhanga kutoboa au kuangamia kimaisha.
Kweli huu ndio mwaka ambao waheshimiwa hukaa na wanyonge fukara kwa maigizo ya kunywa kahawa na kula chakula kwenye misiba.


Huu ndio mwaka unaamua hatma ya miaka mingine itakayokuja, mwaka wa kusuka au kunyoa.


Huu ndio ule mwaka tulioungojea.


© Peter Mwaihola
1736743302791.jpg
 
Back
Top Bottom