Hii ndio aina ya Demokrasia yetu ya kichina, wapinzani wakiilazimisha ya kimagharibi watatumia

Hii ndio aina ya Demokrasia yetu ya kichina, wapinzani wakiilazimisha ya kimagharibi watatumia

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Nilishaandika maandiko mengi juu ya fikra za watawala wetu na Demokrasia tunayoiamini..

Ubaya NI kwamba Uchina ilipiga hatua kuanzia 1980 baada ya kufata Utawala wa kimagharibi. Waliporuhusu vyama vingi, Uhuru wa kibiashara, Sekta binafsi kupewa nafasi, Uhuru wa vyombo vya habari Kisha wakaondolewa vikwazo na kuanza kutrade na Ulaya. Ila baada ya kukua kiuchumi shida imeanza alipoingia Raisi huyu mwenye uchu wa madaraka na yule Wa Russia. Wanataka Kuurudisha dunia nyuma miaka ya 1800 huko kwa fujo zote.

Demokrasia tuliyoamua kuifata NI ya kichina. Na ilianza China na Russia na Sasa inasambaa duniani. Ina sifa zifuatazo.

1. Inaruhusu vyama vingi. Ila chama tawala huongoza vyama vingine vidogo dogo na vyama vyote hutii na kutoikosoa Serikali. Hiyo ndio msingi wa utawala.(unaitwa upinzani wenye busara). Na wapinzani watiifu hupewa vitengo serikalini. NI Kama ilivyo Rwanda ndivyo ilivyo uchina. Kifupi hakuna mpinzani mwenye wazo la kuingia Ikulu.

2. Kukosoa utawala NI kosa la uhaini kiimani lkn haipo kisheria na lazma utashugulikiwa tu kwa mbinu yoyote. Mfano Russia viongozi wa upinzani Alexei Navalny kutwa hufungwa na kufunguliwa mashitaka mapya. Democrasia ya Magharibi huwaogopa Sana viongozi wa upinzani. Rwanda na uchina hao wapinzani wapinga Sera walishatokomezwa zamani wamebaki wachache huko hongkon(Sasa wa kushugulikiwa zaidi NI mkubwa wa upinzani)

3. Democrasia hii inaruhusu Uhuru wa kutoa maoni lkn haikupi uhakika wa kuwa salama baada ya kutoa maoni. NI ile aliyoiamini Gadafi na Idd Amini Dada.

4. Democrasia hii vitu vingi vya utawala NI Siri. Hutakiwi kuhojihoji Sana. Ata kesi na hukumu huendeshwa kwa Siri.

5. Democrasia inayotoa Uhuru wa kupiga kura na sio Uhuru wa kuhesa na kupata matokeo halali.

6. Democrasia hii Bunge lipo Kama kivuli na utekeleza matakwa ya chama tawala bila kuhoji Wala kupinga.(tujifunze kupitia bunge la China. Ndilo huamua karibu kilakitu lkn haliko huru na limeshikwa na uongozi)
7. Kuwa tajili kupita kiasi kunahatarisha usalama wa nchi. Hapa wachina walitutumia sisi kuijaribishia Sera hii. Tukawabinya matajili. Na Sasa wao wameanza kuwapa kibano matajili hao.
8. Democrasia inayothibiti vilivyo mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vinavyoleta chokochoko.

9. Hii Democrasia utawala uongozwa na ushawishi wa uchina zaidi.

Kuipinga Aina hii ya Democrasia msiipinge kwa ndani tu mtaishA. Muongoze dunia iijue na itamke juu ya Democrasia. Kulazimika kuboresha utawala bora na kudhibiti uenevu wa kisiasa.
 
Hii demokrasia imefanikiwa China tu ambako wabadhirifu wa mali za umma hata wawe makada waandamizi hunyongwa.

China haki za binadamu ni msamiati ngumu. Ndugu yako akihukumiwa kwenda jela hasa kwa sababu za kisiasa, agana nae kabisa maana uwezekano wa kuonana nae tenawni mdogo sana.
 
Katika hii demokrasia, ya kichina, mabadiliko hupatikana kwa mtutu au kwa uasi wa nguvu ya umma pekee, NA NI MWISHO WA KUTISHA SANA KWA WATAWALA WA MWISHO NA VIZAZI VYAO!
👊 ☠️ ✌️ 💥
 
Hii demokrasia imefanikiwa China tu ambako wabadhirifu wa mali za umma hata wawe makada waandamizi hunyongwa.

China haki za binadamu ni msamiati ngumu. Ndugu yako akihukumiwa kwenda jela hasa kwa sababu za kisiasa, agana nae kabisa maana uwezekano wa kuonana nae tenawni mdogo sana.
Hata wachina hawaiamini Sana. Na baadhi ya vitu huvipenyeza kwetu ili vijaribiwe na watawala wetu na baadae wao wafanye. Wanatuchukulia Kama sehemu ya Majaribio.
 
Inawezekana ndio watawala wanavyotaka demokrasia ya uchina lakini wameshachelewa kuweka mizizi, maana Tanzania Watu hasa vijana wanataka Demokrasia ya magharibi angalia rate ya vijana kujiunga chama tawala ikoje, ni suala la muda tu hata ndani ya chama tawala hawataitaka hiyo Demokrasia ya uchina maana inawapa nguvu wachache kuliko walio wengi pia uchumi wa ujamaa wa China sasa hauna nguvu kusukuma aina hiyo agenda ndio maana sasaivi kufanya biashara na wachina watu wanatumia akili na kujihoji sana mfano Bandari ya bagamoyo China ingekua na nguvu kwa kutumia Demokrasia yao huo mradi ungeshatekelezwa
 
Hatufati kwasababu NI nzuri. Ila inatupa uhakika wa kuwa madarakani sisi na vizazi vyetu na watu wanaotutii
 
Hata Marekani hawakua na na Demokrsasia hii ya sasa huko nyuma, walikua na Demokrsasia ya Uchina mpaka nchi yao ilivyokua kiuchumi na kutengeneza mifumo yote ndio wakaleta Demokrsasia ya sasa ya kubadilishana Madaraka
 
Hatufati kwasababu NI nzuri. Ila inatupa uhakika wa kuwa madarakani sisi na vizazi vyetu na watu wanaotutii
Hapo ndio shida inapoanzia wanakuja watu au vijana ambao hawafaidiki na huo mfumo hawatakubali wawekwe pembeni lazima italeta mgogoro ikiwezekana haya ile ndoto ya kisiwa Cha amani ikafa kabisa ndio maana nasema wamechelewa either ni kwa bahati mbaya au makusudi mfano Demokrasia inayofundishwa mashuleni na vyuoni ni ya magharibi sio ya China pia hata nchi zinazofuata aina hiyo ya Demokrasia nyingi zina migogoro kwaiyo hakuna kizuri tunachojifunza
 
Hakuleta upinzani yeye aliasi. Lakini Mungu hakumpoteza kabisa au kumuua. Amemuacha na Sasa wanapambana kwa Uhuru tu kuwashawishi wanadamu wawafate na anapata ufuasi. Na hiyo ndio maana ya Democrasia
Na ndio mfumo wa Demokrasia ya magharibi inavyo operates
 
Hapo ndio shida inapoanzia wanakuja watu au vijana ambao hawafaidiki na huo mfumo hawatakubali wawekwe pembeni lazima italeta mgogoro ikiwezekana haya ile ndoto ya kisiwa Cha amani ikafa kabisa ndio maana nasema wamechelewa either ni kwa bahati mbaya au makusudi mfano Demokrasia inayofundishwa mashuleni na vyuoni ni ya magharibi sio ya China pia hata nchi zinazofuata aina hiyo ya Demokrasia nyingi zina migogoro kwaiyo hakuna kizuri tunachojifunza
Kwenye hii Democrasia hua hatufikirii Sana ya mbele uko. NI sawa tu na ile inayowachafua Sasa Waethipia. Ata yalitokea machafuko tunaotawala tunapambana ikishindikana kabisa tunakimbia tu
 
Kwenye hii Democrasia hua hatufikirii Sana ya mbele uko. NI sawa tu na ile inayowachafua Sasa Waethipia. Ata yalitokea machafuko tunaotawala tunapambana ikishindikana kabisa tunakimbia tu
Kama inavyotokea Afaganstan, Syria, libya hata hapo Uganda na Rwanda ila ndio maana nasema kwa Tanzania wamechelewa maana hata ndani ya chama tawala kuna watu hawakubaliani na huo mfumo
 
Bandiko zuri sana kielimu. Huo ndio mfumo halisi wa siasa wa China. Salute mkuu.

China wameweza kutumia mfumo huo kupunguza upinzani wa ndani. Misingi imara ya uchumi iliyojengwa wakati wa ukomunisti pia imesaidia sana. Aidha, wamedhibiti ufisadi mkubwa kwa kubana wigo kuruhusu walaji wachache tu wenye connection kubwa.

Wamepunguza mashambulizi toka nchi za magharibi kuhusu haki za binadamu kwa kuhakikisha wanatoa fursa kibao za uwekezaji na masoko kwa mabepari wakubwa wa Marekani na Ulaya.

Sisi hatuna uwezo wa kuwa na demokrasia ya Kichina. Labda kama tunataka kumuiga Kagame kitu ambacho hakiwezekani kama utawala wa mwendazake ulivyothibitisha.
 
Hata Marekani hawakua na na Demokrsasia hii ya sasa huko nyuma, walikua na Demokrsasia ya Uchina mpaka nchi yao ilivyokua kiuchumi na kutengeneza mifumo yote ndio wakaleta Demokrsasia ya sasa ya kubadilishana Madaraka

Si kweli. Taifa la Marekani lilianzishwa na watu waliokimbia tawala za kidikteta za Kifalme za Ulaya. Wengi walikuwa ni wajasiriamali waliotaka fursa na uhuru mkubwa wa kufanya shughuli zao. Walipowasili Marekani walianza mapambano mapema kabisa kujihakikishia uhuru wa mtu binafsi, haki za binadamu, na demokrasia vinaongoza jamii zao.

Maendeleo ya kiuchumi kwao yalienda sambamba na harakati za kisiasa kwa vile walikuwa ni wajasiriamali walioamini katika uwezo wa kila mtu kufanya shughuli zake za kiuchumi kwa uhuru katika mfumo wa soko huria. Uchumi wa Marekani ulipaishwa na fursa kubwa za kiuchumi walizozikuta na uhuru mkubwa wa kufanya ujasiriamali tofauti na kibano cha udikteta kilichokuwepo ulaya.

Hata China, uchumi wao ulipaa katikati ya miaka ya 80 baada ya kulegeza kibano cha ukomunisti na kuruhusu uchumi wa soko huria kwa kiasi kikubwa. Uzuri tayari walikuwa mbali kwa misingi ya kiteknolojia jambo lililowavutia wawekezaji wakubwa toka Marekani na Ulaya.
 
Back
Top Bottom