Hii ndio aina ya Demokrasia yetu ya kichina, wapinzani wakiilazimisha ya kimagharibi watatumia

Hii ndio aina ya Demokrasia yetu ya kichina, wapinzani wakiilazimisha ya kimagharibi watatumia

Sioni ulinganifu na Uchina wa mambo mazuri isipokuwa mabaya tu? Mbona kama tumefuata siasa za China, nasi hatuendelei kama uChina?

Nadhani kuwa siasa zetu hazieleweki. Bado sio viongozi tu, hata wananchi - hatujui tunataka nini. Kwa sababu hiyo tumechagua kufuata kila kitu - cha kichina, kimagharibi, chetu wenyewe na cha mwingine yeyote!! Ndio sababu ya mkwamo huu!!
 
Hata Marekani hawakua na na Demokrsasia hii ya sasa huko nyuma, walikua na Demokrsasia ya Uchina mpaka nchi yao ilivyokua kiuchumi na kutengeneza mifumo yote ndio wakaleta Demokrsasia ya sasa ya kubadilishana Madaraka
Marekani ipi unayoizungumzia wewe. Soma historia acha kuropoka tu.
 
Sioni ulinganifu na Uchina wa mambo mazuri isipokuwa mabaya tu? Mbona kama tumefuata siasa za China, nasi hatuendelei kama uChina?

Nadhani kuwa siasa zetu hazieleweki. Bado sio viongozi tu, hata wananchi - hatujui tunataka nini. Kwa sababu hiyo tumechagua kufuata kila kitu - cha kichina, kimagharibi, chetu wenyewe na cha mwingine yeyote!! Ndio sababu ya mkwamo huu!!
Uchina ilipiga hatua kuanzia 1980 baada ya kufata Utawala wa kimagharibi. Waliporuhusu vyama vingi, Uhuru wa kibiashara, Sekta binafsi kupewa nafasi, Uhuru wa vyombo vya habari Kisha wakaondolewa vikwazo na kuanza kutrade na Ulaya. Ila baada ya kukua kiuchumi shida imeanza alipoingia Raisi huyu mwenye uchu wa madaraka na yule Wa Russia. Wanataka Kuurudisha dunia nyuma miaka ya 1800 huko kwa fujo zote.
 
Nilishaandika maandiko mengi juu ya fikra za watawala wetu na Demokrasia tunayoiamini..

Ubaya NI kwamba Uchina ilipiga hatua kuanzia 1980 baada ya kufata Utawala wa kimagharibi. Waliporuhusu vyama vingi, Uhuru wa kibiashara, Sekta binafsi kupewa nafasi, Uhuru wa vyombo vya habari Kisha wakaondolewa vikwazo na kuanza kutrade na Ulaya. Ila baada ya kukua kiuchumi shida imeanza alipoingia Raisi huyu mwenye uchu wa madaraka na yule Wa Russia. Wanataka Kuurudisha dunia nyuma miaka ya 1800 huko kwa fujo zote.

Demokrasia tuliyoamua kuifata NI ya kichina. Na ilianza China na Russia na Sasa inasambaa duniani. Ina sifa zifuatazo.

1. Inaruhusu vyama vingi. Ila chama tawala huongoza vyama vingine vidogo dogo na vyama vyote hutii na kutoikosoa Serikali. Hiyo ndio msingi wa utawala.(unaitwa upinzani wenye busara). Na wapinzani watiifu hupewa vitengo serikalini. NI Kama ilivyo Rwanda ndivyo ilivyo uchina. Kifupi hakuna mpinzani mwenye wazo la kuingia Ikulu.

2. Kukosoa utawala NI kosa la uhaini kiimani lkn haipo kisheria na lazma utashugulikiwa tu kwa mbinu yoyote. Mfano Russia viongozi wa upinzani Alexei Navalny kutwa hufungwa na kufunguliwa mashitaka mapya. Democrasia ya Magharibi huwaogopa Sana viongozi wa upinzani. Rwanda na uchina hao wapinzani wapinga Sera walishatokomezwa zamani wamebaki wachache huko hongkon(Sasa wa kushugulikiwa zaidi NI mkubwa wa upinzani)

3. Democrasia hii inaruhusu Uhuru wa kutoa maoni lkn haikupi uhakika wa kuwa salama baada ya kutoa maoni. NI ile aliyoiamini Gadafi na Idd Amini Dada.

4. Democrasia hii vitu vingi vya utawala NI Siri. Hutakiwi kuhojihoji Sana. Ata kesi na hukumu huendeshwa kwa Siri.

5. Democrasia inayotoa Uhuru wa kupiga kura na sio Uhuru wa kuhesa na kupata matokeo halali.

6. Democrasia hii Bunge lipo Kama kivuli na utekeleza matakwa ya chama tawala bila kuhoji Wala kupinga.(tujifunze kupitia bunge la China. Ndilo huamua karibu kilakitu lkn haliko huru na limeshikwa na uongozi)
7. Kuwa tajili kupita kiasi kunahatarisha usalama wa nchi. Hapa wachina walitutumia sisi kuijaribishia Sera hii. Tukawabinya matajili. Na Sasa wao wameanza kuwapa kibano matajili hao.
8. Democrasia inayothibiti vilivyo mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vinavyoleta chokochoko.

9. Hii Democrasia utawala uongozwa na ushawishi wa uchina zaidi.

Kuipinga Aina hii ya Democrasia msiipinge kwa ndani tu mtaishA. Muongoze dunia iijue na itamke juu ya Democrasia. Kulazimika kuboresha utawala bora na kudhibiti uenevu wa kisiasa.
Muhimu demokrasia hiyo uliyoeleza iongozwe na strong man muadilifu mwenye correct vision kuhusu maendeleo ya umma wa wananchi. Ina maana serikali iweze kudhibiti sekta binafsi na ile ya umma kusababisha umma wa raia kupata maendeleo kijamii na kiuchumi.
 
China kuna vyama vingi?

Una malaria?Unajua unachokiongea?

China kuna mwananchi yeyote bilioni 1.4 alishawahi kupiga kura kuchagua rais au mbunge wa nchi hiyo?

NEVER!

Stop this nonsense,unaongea kitu hukijui
Kama hujasoma historia Basi ingia Google uone. Nilichokiandika kuhusu China ndicho. Kama ilivyo Rwanda. Ila bunge ndilo uunda serikali
 
Una malaria wewe

China hakuna vyama vingi,kuna chama Kimoja pekee yake

China hakuna uchaguzi mkuu kwa wananchi kuchagua rais wa nchi au wabunge

Wachina wanapiga kura mitaa yao na vitongoji vyao kuchagua muwakilishi wa mtaa wao tu...

Hakuna uchaguzi China

Get that in your stupid brain

Hujui unakiongea,kama umesoma Google soma tena,hujaelewa chochote

Usipaniki mkuu. Chama tawala China NI CCP. Nyuma Kuna vyama 8 vidogo. Ila vyama hivyo vya siasa havipingani na Serikali lkn hujitegemea. Yenyewe inajiita Ina vyama vingi Ila wanademocrasia huvikosoa na kuviona sio vyama haswa.

Vyama hivyo NI

Name
(abbreviation) Date founded Existed Location founded Members Current leader Official
website
Chinese Communist Party (CCP)
中国共产党(中共) 23 July 1921 100 years, 77 days Shanghai French Concession 89,450,000 General Secretary
Xi Jinping [8]
China Zhi Gong Party (CZGP)
中国致公党(致公党) 10 October 1925 95 years, 341 days Los Angeles, United States 48,000 Chairman
Prof. Wan Gang [9]
Chinese Peasants' and Workers' Democratic Party (CPWDP)
中国农工民主党(农工党) 9 August 1930 91 years, 38 days Shanghai, China 145,000 Chairman
Prof. Chen Zhu [10]
China Democratic League (CDL)
中国民主同盟(民盟) 19 March 1941 80 years, 181 days Chongqing, China 282,000 Chairman
Prof. Ding Zhongli [11]
Jiusan Society (JS)
九三学社 3 September 1945 76 years, 13 days Chongqing, China 167,218 Chairman
Prof. Wu Weihua [12]
China National Democratic Construction Association (CNDCA)
中国民主建国会(民建) 16 December 1945 75 years, 274 days Chongqing, China 170,000 Chairman
Prof. Hao Mingjin [13]
China Association for Promoting Democracy (CAPD)
中国民主促进会(民进) 30 December 1945 75 years, 260 days Shanghai, China 156,808 Chairman
Prof. Cai Dafeng [14]
Taiwan Democratic Self-Government League (TDSGL)
台湾民主自治同盟(台盟) 12 November 1947 73 years, 308 days British Hong Kong 3,000 Chairwoman
Su Hui [15]
Revolutionary Committee of the Chinese Kuomintang (RCCK)
Twende kwa fact. Usitukane burree.

Na swala la bunge kuunda Serikali nimelisema hapo juu. Shida Nini Kaka.
 
Si kweli. Taifa la Marekani lilianzishwa na watu waliokimbia tawala za kidikteta za Kifalme za Ulaya. Wengi walikuwa ni wajasiriamali waliotaka fursa na uhuru mkubwa wa kufanya shughuli zao. Walipowasili Marekani walianza mapambano mapema kabisa kujihakikishia uhuru wa mtu binafsi, haki za binadamu, na demokrasia vinaongoza jamii zao.

Maendeleo ya kiuchumi kwao yalienda sambamba na harakati za kisiasa kwa vile walikuwa ni wajasiriamali walioamini katika uwezo wa kila mtu kufanya shughuli zake za kiuchumi kwa uhuru katika mfumo wa soko huria. Uchumi wa Marekani ulipaishwa na fursa kubwa za kiuchumi walizozikuta na uhuru mkubwa wa kufanya ujasiriamali tofauti na kibano cha udikteta kilichokuwepo ulaya.

Hata China, uchumi wao ulipaa katikati ya miaka ya 80 baada ya kulegeza kibano cha ukomunisti na kuruhusu uchumi wa soko huria kwa kiasi kikubwa. Uzuri tayari walikuwa mbali kwa misingi ya kiteknolojia jambo lililowavutia wawekezaji wakubwa toka Marekani na Ulaya.
Umesoma history vizuri na kuielewa vizuri kongore kwako. Marekani umejengwa na fugitives kutoka ulaya na msingi mkubwa wa mafanikio yao ni katiba ambayo imetoa uhuru mkubwa wa mwanadamu kutia kipawa chake kujiletea maendeleo. Sisi hatuna democracy kabisa tuna udictator wa kishamba. People a
 
I read you shemrji William Mshumbusi .
Vyama vya upinzani viwe Kama
UDP
TLP
NCCR
Kama Cha yule msukuma anayeongeaga kiswahili kizuri alikuaga mwenyekiti wa ccm wazazi.
ACT
CUF
Ambao every now and then wanatupiwa mfupa na CCM.
 
Mkuu

Hakuna vyama vingi

Chama ambacho hakipingwi na vyama vingine sio vyama vingi ni single party supremacy

Get that in your head

Vyama vyote ulivyotaja hapo havitambuliwi na serikali,hakuna chama kingine cha siasa china ukiacha CCP.

Usituletee vyama "dhania" eti ndio vyama rasmi vya kisiasa rasmi vinavyopambana na CCP,unageuka unasema haviruhusiwi kupingana na CCP,then unaita "vyama vingi"?

Inachofanya China ni tofauti na bunge kuunda serikali,sio parliamentary democracy

Hakuna mwanadamu yeyote China anachaguliwa kwa uchaguzi mkuu China.

China infact hakuna mambo ya kura,ni balozi wa nyumba kumi kumi wananchi wa hizo nyumba kumi wanamchagua kusimamia kamtaa kao,basi.

Hakuna kupiga kura CHina.

CCP inaundwa na group la Wachina waliojichagua wao kwa utashi wao kutawala watu bilioni 1.4 kwa lazima....CCP inaamini wananchi bilioni 1.4 hawana akili ya kuchagua kiongozi bora,wao waliomo ndani ya CCP ndio wana akili na utashi huo
Kupitia uchaguzi uliopita umeona CCM inaamini kunamwananchi anaakili ya kuchagua kiongozi zaidi ya uongozi wenyewe wa CCM. Kura zinapigwa kwa fashion na ndiko tunakokutaka
 
Mkuu

Unaongelea WIZI wa kura?

Huo ni WIZI wala sio mfumo legal....

Au uniambie ni mfumo wa wizi tupo which ni kwamba ni mfumo wa mahayawani...CCM ni mahayawani
Mi nimeuliza kupitia uchaguzi wa Aina hiyo wananchi wanAhezhimiwa maamuzi yao na utawala. Huioni nguvu ya Viongozi wa CCM kwenye kilakitu kama ilivyo kwa CCP?
 
Back
Top Bottom