Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Mawazo haya ni bora tena yenye kutaja uhalisia..,yanatoa somo na fundisho kwa walio wengi (wenye kufikiri) natamani laiti kama haya yangelieleweka katika vichwa vya wengi miongoni mwa vijana wetu.

Lakini pamoja na kuandika hapa ni vyema habari hii,.ingeanzishiwa thread yake binafsi kushauri..,kama hilo linawezekana lifanye.,tena lifanye hivi sasa. Maneno haya uliyoyaandika yanahitajika mno kwa wakati huu ambao vijana wamepata matokeo mabovu kupindukia na kuwafanya wao na jamaa zao kuwa frustrated wote wakitaka kumnyooshea kidole mwingine.,kunyoosheana vidole ambako sio suluhisho na wala hakutasaidia kitu.

Naomba nieleze mtazamo wangu kwako..,nakutazama kuwa wewe ni mtu unayestahili kuitwa great thinker tena aliyetofauti na wa kipekee humu jamvini.

Maneno mazuri ni sadaka nami nimeipokea sadaka yako, ubarikiwe...!
 
Pleaseeeee tunaomba utuambie matokeo Yale ya o level na A level, aliscore division ngapi? Kama alivyofanya mnyika.......Ndio ombi letu
 
Unashangaa hayo kuna mtu Ana Div 4 ya 31 na ni mwenyekiti wa Chama

Unamshangaa mwenye four ya 31 na kuwa mwenyekiti wa chama? Kuna huyu Rais wetu, ana Gentleman ya UDSM, mbona hushangai kuongoza maprofessor? Ndio shida ya akili ndogo kuongoza akili kubwa na ndio maana ya kuuliza "Eti nani hajui kuwa Dar hakuna maji?" Yaani anajua, halafu anauliza, sijui alikuwa anataka nini? We have lost 10 years (2005 - 2015) hakuna kitu tumefanya, hata sisi ambao hatukumpigia kura, tunamia kutokana na akili za wajinga wachache. Stupid!!!!
 
Guys miaka hiyo ambayo wengine tulisoma pande za Rocky city, Butimba TTC ilikuwa inatumika kama kituo cha kufanyia mitihani watu wa A level so its not something new kwani kuna hata close friends of mine walitumia kituo hicho kufanyia mitihani yao ya A level (kipindi hicho mama Gaudencia Kabaka - Waziri- alikuwa mkuu wa chuo). Inawezekana hata Ndg Nape naye akawa ni mmoja wa watu walio tumia kituo hicho.
 

mangwela,

Wewe unaonekana huelewi kinachozungumzwa hapa.

Tuliopitia shule tunajua nini maana ya PC na SC. Private Candidate Centre haimfanyi mtu kuhitimu combination ya EGM hata siku moja. Pale unapojisajili kwa ajili ya mitihani iwe ni ya F4,F6 au QT kwenye kituo(centre)haikufanyi kuwa mwanafunzi wa kituo. Unaweza ukawa unasomea Dar na ukajisajili kufanyia Mitihani yako Butimba TTC. Itakuwa ni upuuzi kuwaambia watu kuwa umehitimu F6 Butimba TTC unless hujui unachozungumza. Nnape anajua Butimba TTC HAKUNA ELIMU YA A LEVEL(F6) inayotolewa!!!

Acha kutetea upuuzi na ujinga wa viongozi wababaishaji wa CCM kama Nnape.
 
mkuu uko sahihi uelewa wa watu wengine inabidi tuingie ndani ya akili zao ndio watajua nini tunaongelea hapa
 

kama ni O-Level na A-Level mbona wamemaliza wengi tu?
si unaona hata matokeo ya wadogo zetu wa form 4 mwaka huu???
kusoma sio issue, the point is umetoka na divission ngapi?
una class ipi???
embu na hapa uweke kwa majigambo kama ulivyoweka hiyo CV Japo naona kama nayo ni ya kuunga na super glue.

NAWAZA TU JAMANI.
Hapo kwenye RED wadau si mnajua kwenye kuvuka hivyo vidato kuna mitihani ya michujo?
sasa hapo nahisi kuna namna ndio maana mtu mzima akahama na shule kabisa manake si unajua ile wenzio wanasonga mbele wewe unapiga mark-time?
 

Achani wendawazimu wa kimawazo na fikra finyu.
Huyu jamaa amejiendeleza vema sana na anastahili pongezi nyingi sana. Kama hayuko vema kiakilia kama unvyoataka tujue asingeweza kufaulu masters pale Mzumbe.
Dr Salim Ahmed Salim na mzee Mwinyi (rais mstaafu) hawakuwahi kusoma Bachelor degree lakini ni moja wa nguli wazuri sana duniani.
Pili, si vema kabisa kuvishusha vyuo vikuu vya India, kwani kuna watu mashuhuri na wenye heshima sana nchini, akiwema Malecela waliosoma huko. Hiyo sijataja wazuoni wengine wengi Duniani. Marekani kuna vyuo bogus zaidi kuliko India.
Bila kujali mwelekeo wetu kisiasa, ni lazim tufike sehemu tufikirie kwa kutumia akili akili.
 
Elimu ya mtu utampima iQ yake.Angalia maongezi yake hotuba zake.Kuna wengine wana vyeti vizuri lakini kichwani hakuna kabisaaaaa.walikuwa wamekwenda shuleni kukremu tu.Wengine baba zao watu wakubwa na wana uwezo kusema make sure mwanangu anapata marks nzuri.Cha msingi ni utaona tu akili yake sasa hivi na utapata jibu huyu kichwani hakuna.Husiangalie vyeti kabisaaaa.Hangalia mchango wake wa kitaaluma kwa jamii.
 
Napita tu,maana umri wangu hauruhusu lkn naelekea kumzidi Nape kitaaluma.Haya jamani majadiliano mema.
 
form 6 huyo alifeli hapo ndio akaamua kwenda kusoma hiyo certificate na sio diploma! huyo kilaza nape wala hana ki2 kichwani!
 
Inaweza kuwa "private candidate" kuna center pale.

Degree za kuunga unga na kazi za kunga unga kutoka katibu muktasi mpaka katibu mwenezi subiri kesho atauuga mpaka waziri au Rais kwani hamjui tanzania yetu watu kwa kuungisha ndio viongozi wetu madokta ukishindwa wa darasani unavarisha mwenyewe kama dokta Lyatonga ? Kwani shida gani Bongo ? kuwa mjanja
 

Mzumbe ni chuo ambacho kinapashwa kujiangali sana na watu hawa wa kuuungaunga. Wapo wengi ambao wamepita Mzumbe na wana Masters lakini ni wahitimu wa ovyo sana . Tunao na tunawajua maana hata thesis wameandikiwa mitahani. na wengi wakishatoka mzumbe sio kwamaba wanakwenda kutumia taaluma zao hizo ila wanaingia siasa.
Fuatilia wahitimu wa Mzumbe walio kwenye siasa uone ni watu wana namna gani , Fanya utafiti mtajua nisemalo
 
DU! Fanya kama mnyika ambae amuthubutu kutaja na daraja alilopata kila level. uoga wa nini kama upo safi
 
Hata mimi niliye feri mwaka huu najua tu jamaa na e aliferi form 4
 
Yani Nape alipiga Yai kwenye Civics? sasa CCM walimpaje itikadi na uenezi mtu asiyejua hata uraia?:shut-mouth:
 

:israel:Mbona wewe Tandaleone PS wa Nape hauko makini? kwanini usiweke alifaulu kwa kiwango gani O-Level na A-Level? inaonekana wewe ni mpambe tu haujui kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…