mansakankanmusa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 4,162
- 796
WEWE jiunge tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika thesis iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)
- Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
- Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu 3 kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
- Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
- Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
- Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
- Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
- Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
- Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
- Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe.
Mbona hakuna habari hata moja iliyokuwa inavumishwa ambayo wewe umeikosoa, hasa kwenye perfomance zake? Afu wewe siyo Nape, kwani yeye hayupo mpaka uje hapa umtetee?
Ambatanisha na ufaulu wake kwa kila ngazi ya elimu
Alizaliwa mwaka gani????.
Tuanzie hapa form 4
NAPE NNAUYE
SEX M DIV IV PTS 29 KISW D HIST D GEOG D ENGL F B/MATH F BIOL D CHEM D PHY D CIV F
-----------------------
JOHN MNYIKA
SEX M DIV I PTS 7 PHY A CHEM A BIOL A CIV A ENGL A GEOG A HIST A B/MATH A KISW A B/KNOW A
Mbona hueleweki agwe?Kama unafikiri kusoma hakuna maana hebu jilinganishe wewe kilaza na waliohudhuria madarasa.Au kwa maneno mengine kama elimu haina maana basi jaribu ujinga.Nchi hii inahitaji kusoma sana hao wasomi wenyewe hawana lolote wanalolifanya
Anaomba kazi? Hii CV ya nini? Hizi diploma za mwaka mmoja mmoja Duhhhh.
Mkuu nimekosa kitufe cha LIKEAnaomba kazi? Hii CV ya nini? Hizi diploma za mwaka mmoja mmoja Duhhhh.
Shule za kuunga unga kama super glue!