Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah kumbe upo vizuri kaka, ila sasa kule kuropoka ropoka kunatoka wapi? Wakati unaelimu nzuri tu.
TandaleOne Master of Business Administration na sababu zinazochangia ushiriki wa wapiga kura zina uhusiano gani? Angefanya "Reasons lead to poor performance of public corporations" hii kidogo ingelandana na hiyo master yake @Nnauye Jr
Chakachua ya elimu hiyo.....
ni masters ya public administration kaka umesoma haraka kama unakimbizwa. Ila nashangaa hiyo masters kaisoma kwa mwaka mmoja tu naona alikuwa kichwa sana. Pia sijaelewa yeye kusoma advance na kumaliza Butimba TTC.
ndo kwanza nimetoka kwenye ban ila acha ni tukane shens
we gamba MNYIKA FORM FOUR ALIKUWA TANZANIA ONE, UWEZO WAKE WA KUFIKIRI NI SAWA NA WABUNGE 50 WA CCM, NANI CCM AMESHA WAHI KUONGOZA KITAIFA HATA MTIHANI WA LA SABA TU??????? NAPE FORM FOUR DIVISION FORM 31Yupo vizuri sana, unafikiri unaweza fananisha na Mnyika? Mzee wa evening class, Mzee wa kuungaunga. Maneno mengi sana. lakini CDM viongozi wenu wengi ni mbumbumbu sana Kama Mbowe, Sugu nk
[*]Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
[*]
Hii Cv angekua anakuja kuomba kazi alikuwa anatupwa kabla ya hata kujadiliwa, inaji confuse hovyohovyo, ndo viongozi wa ccm wa sasa ambao hata vyeti wanapeana kwa jina la chama, hovyo kabisa
Hongera Nape kwa kuwaacha mbali KIELIMU viongozi waandamizi wa Chadema ambao ni: Mbowe (Form Six), Arfi (Standard Four), Mnyika (Form Six), Nyerere (Form Four), Mr 2 (Form Four)
Ushauri kwa vijana,
Hii mijadala ya elimu ya Nape na Mnyika ina mafundisho mengi sana kwa vijana kama mnataka kujifunza. Wekeni siasa pembeni na jifunzeni jinsi maisha yanavyobadilika na jinsi ambavyo kushindwa jambo moja sio mwisho wa mafanikio.
Hapa inaonyesha wazi Mnyika alikuwa na uwezo mkubwa sana shuleni na bado ana uwezo mkubwa maana hata hoja zake nyingi zina mshiko. Lakini inakuwaje kwa miaka yote hiyo kashindwa kumalizia hako kadegree ambako kwa uwezo wa Mnyika ni kadogo sana? Sidhani kama muda ndio tatizo pekee, labda hata hakuona umuhimu, kitu ambacho mimi nakielewa maana hata akina BIll Gates, Jobs hawakuona umuhimu wa kubaki vyuoni wakati tayari kichwani walikuwa na uwezo wa kufanya yale waliyotaka kufanya baada ya vyuo.
Tukija kwa Nape ni wazi uwezo wake ulikuwa mdogo, hakuwa na credits za kuingia A-level. Lakini kijana Nape hakulala chini na kuanza kulia au kulalamika, badala yake aliamua kujiendeleza kwa kuunga uunga elimu. Mwisho wa siku amesoma mpaka sasa ana masters yake kwenye Public Administration. Hili ni fundisho hata kwa vijana wote waliofeli mwaka huu, tumieni elimu hiyo ya Nape kama hamasa ya kwamba kama Nape ameweza kwanini na nyie msiweze? Bila kujali umepata sifuri au division four. Elimu ya karne ya 21 bado kijana una nafasi ya kuweza kusoma, kujiendeleza na mpaka hata kuwa profesa ukitaka. Uamuzi ni wako, kuamua kupambana au kuishia kucheka wengine. Ukipata F si unarudia?
Sisi sote tuliosoma zamani tunawajua watu wengi sana ambao form six walipata zero hata ya F zote lakini wengine sasa ni maprofesa, madaktari, wachumi nk. Kama mtu anabisha, awaangalie watu waliokuwa wanasoma PCB miaka ya 80. Utawakuta wengi pamoja na kufeli form six lakini leo wako mbali sana. Walichofanya, walijiendeleza na kufeli form six haikuwa sababu ya kuwakwamisha. Kuna jamaa mmoja juzi juzi akaniambia utani akimsema msomi mmoja maarufu wa sheria TZ kwamba alipata division zero PCB Tabora. Nilishutuka sana, sikuamini. Lakini ukweli ndio huo, kupata four au zero sio mwisho wa elimu.
Binafsi kuna vijana nimewahi kuwasaidia ambao form four walitoka na points kama hizo za Nape. Through kuwashauri na kuwasaidia, leo hii wamemaliza degree zao na wana mafanikio kwenye kazi zao.
Sawa tutumie siasa kuchekana kama kujifurahisha, lakini kwenye mioyo yetu tutambue hili ni somo tosha. Kufeli jambo mara moja sio mwisho wa dunia. Badala yake amka, jipukute na anza safari tena kwa speed hata kubwa kuliko mara ya kwanza.
Wakati wewe unacheka na kupoteza muda, wenzako wanasonga mbele.
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika thesis iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)
- Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
- Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu 3 kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
- Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
- Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
- Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
- Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
- Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
- Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
- Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe.
"Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC'
Kaandae upya hii cv ya kuforge, 1998-2000 High School + kuhitimu Butimba TTC ambako ni chuo cha ualimu!!!!!!!!!!!
ndo kwanza nimetoka kwenye ban ila acha ni tukane shens