- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na video inayosambazwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii, ikidaiwa kuonyesha eneo ambalo aliyekuwa mfanyabiashara nchini Zimbabwe, Sir Chivayo, atazikwa. Video hiyo inaonyesha mazingira ya kijijini yenye nyumba na majengo mbalimbali.
- Tunachokijua
- Kumekuwepo na video inayosambazwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii, ikidaiwa kuonyesha eneo ambalo aliyekuwa mfanyabiashara nchini Zimbabwe, Sir Chivayo, atazikwa. Video hiyo inaonyesha mazingira ya kijijini yenye nyumba na majengo mbalimbali.
Hata hivyo, ufuatiliaji wa video hiyo umebaini kuwa ni ya zamani na haihusiani na eneo ambalo Sir Chivayo anatarajiwa kuzikwa, kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.
Video hiyo ilichapishwa awali na Chivayo mwenyewe kwenye akaunti yake ya Instagram, ambapo aliambatanisha ujumbe akieleza kuwa nyumba na miundombinu inayoonekana kwenye video hiyo ilijengwa mwaka 1962, baada ya babu yake kununua shamba lenye ukubwa wa ekari 400 kwa fedha taslimu.
Chivayo pia alieleza kuwa nyumba hizo zina thamani kubwa ya kihistoria na kumbukumbu kwa familia yake, hivyo amezihifadhi katika hali yake ya awali kama sehemu ya kumbukumbu za familia.
Kwa hiyo, video hiyo ni ya zamani na haijathibitishwa kuwa inaonyesha eneo ambalo Sir Chivayo atazikwa, licha ya kusambazwa kwa madai hayo kwa sasa.