Hii ndio hali ya wahitimu wengi bila ajira, wanarudi "back to the basics" biashara za std 7 / form 4

Sasa mtu aliesomea banking unategemea aje mtaani na kuanzisha benki yake? Au aliesomea udaktari aje mtaani kufungua maabara au dispensary? Mambo tunayosomea chuo yanahitaji mtu awepo kwenye taasisi ndio aweze ku-utilize alichosomea. Ukimpa mtaji wa milioni moja milioni mbili atalazimika kuanzia chini kwanza huku kwenye tigopesa, mpesa.
 
Oya mkuu nikiuza viatu vya mtumba nitatoboa kweli?🥹
Vya kike au vya kiume? Nishawahi kufanya hiyo biashara miaka mingi kidogo imepita. Wanaume wanapendelea zaidi ubora. Hawana shida ya kulipia hela kubwa kama ubora unaridhisha. Lakini sio wavaaji kwaiyo utauza vichache, lakini faida ya kiatu kimoja itakua kubwa.

Wanawaje wanapendelea zaidi quantity, yaani yeye awe tu na pea nyingi za kubadilisha kila siku hata kama ubora wa kiatu ni mdogo. Vilevile kwenye suala la bei hawapo tayari kutoa hela nyingi. Kwahiyo utalazimika kuwauzia vitu cheap. Kwa sababu wanawake ni wavaaji Utauza vingi lakini faida ya kila pea itakua ndogo.

Kwahiyo kama utaspecialize viatu vya wanaume zinagatia quality. Kama utaspecialize viatu vya wanawake zingatia quantity and low price
 
Nilikuwa namzingua tu

Biashara yangu miaka nenda rudi nauza vya wanawake, ila special!
 
Hakuna biashara ya std 7 wala ya PhD holder
Jitahidi kuwa unatumia hata akili za majirani
Zipo biashara za phd ambazo std 7 hataweza kufanya mfano unauza research kwa taasisi mbalimbali hiyo mtu wa std 7 anaweza fanya?

Alafu kingine si watu wote walibarikiwa kuwa na kipaji cha kufanya biashara sababu sio rahisi hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…