Hii ndio hatari inayoweza kujitokeza baada ya mkataba wa Songas kumalizika

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
1730455189025.png

Sasa ni rasmi kwamba mkataba wa ununuzi wa umeme (PPA) kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Songas umemalizika rasmi jana Oktoba 31, 2024.

Hatua hii inaiweka Songas kwenye njia ya kudai takriban Dola milioni 90 za Marekani (takribani Sh250 bilioni) kutoka Tanesco ambazo ni malimbikizo endapo hakutakuwa na makubaliano ya kuongezwa muda wa PPA.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Felchesmi Mramba wamelithibitishia gazeti la The Citizen kuhusu kumalizika kwa mkataba huo.

“Umeshamalizika. Kwa bahati mbaya niko kwenye mkutano hivi sasa siwezi kueleza zaidi,” amesema Dk Biteko.

Alipoulizwa ni nini kitakachofuata baada ya kumalizika kwa PPA, Mramba amesema, “siwezi kusema chochote kwa sababu mkataba unamalizika leo (Oktoba 31, 2024) kwa hiyo hatujafanya mipango yoyote.”

Hata hivyo, taarifa zimeeleza kumalizika kwa PPA kuna maana kuwa Songas inaweza kuanza mchakato wa kusitisha shughuli zake katika kituo cha umeme cha Ubungo na kugawa hisa zote zilizobaki kwa wanahisa wake.

Kwa sasa, Serikali kupitia Tanesco, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni ya Maendeleo ya Fedha Tanzania (TDFL) wanamiliki asilimia 46 ya hisa za Songas. Hisa zilizobaki zinamilikiwa na Globeleq.

Fedha za malimbikizo ambazo Songas inaweza kudai kutoka Tanesco zimeongezeka kutoka kiasi kilichokokotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka jana.

Katika ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2022/23, CAG, Charles Kichere alionya dhidi ya kuchelewesha kusuluhisha migogoro mitatu kati ya Songas na Tanesco, ambayo ilikuwa imetajwa kuwa Sh109.07 bilioni wakati huo. Mapitio ya CAG yalionyesha migogoro inayojirudia ambayo haijasuluhishwa tangu mwaka 2022.

Kichere alisema Tanesco ilipinga malipo yenye thamani ya Sh67.94 bilioni.

Hata hivyo, Songas iliendelea kujumuisha gharama za tozo za ukarabati wa mali (sinking) kwenye ankara za kila mwezi kuanzia Agosti 2022 hadi Juni 2023, zikiwa na thamani ya Sh29.34 bilioni, licha ya taarifa ya mgogoro iliyotolewa na Tanesco Desemba 2022.

"Zaidi ya hayo, ankara ya Januari 4, 2023, yenye thamani ya Sh23.94 bilioni na Dola milioni 4.02 kwa Desemba 2022, ilizua mgogoro kuhusu deni la Sh11.78 bilioni la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayodaiwa na TRA kutokana na kukosekana kwa nyaraka za kuunga mkono,” alisema CAG mwaka jana.

Mei, mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alilieleza Bunge kwamba, Tanzania ingezingatia masilahi ya kitaifa kabla ya kutoa ruhusa ya kuongeza mkataba kati ya Tanesco na Songas.

Alisema timu ya majadiliano ya Serikali iliundwa Aprili 2023 na kwamba, majadiliano yalitarajiwa kukamilika kabla ya kumalizika kwa mkataba.

Ingawa Serikali imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa megawati 662 kutokana na kuwashwa kwa mitambo mitatu kati ya tisa katika mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP), umuhimu wa vyanzo mbadala bado unahitaji kusisitizwa.

Uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia hutoa nguvu muhimu kwenye gridi ya Taifa hasa wakati wa ukame.

Wataalamu wa ndani wanasema kwa senti za Marekani 4.9 kwa kilowati kwa saa (kWh), Songas imekuwa ikiuzia Tanesco umeme kwa viwango vya bei nafuu zaidi.

Katika pendekezo la kuongeza mkataba wa PPA kwa miaka sita, kampuni hiyo ilipunguza bei hadi senti 3.9 za Marekani kwa kWh bila kujumlisha gharama za gesi asilia.

Gharama za gesi zinazotarajiwa kujadiliwa zikijumlishwa bei itakuwa senti 6.82 za Marekani kwa kWh.

Kwa mujibu wa watu walio na ufahamu kuhusu suala hili, bado ni chini ya senti 11 za Marekani kwa kWh ambazo Tanesco inawatoza wateja wake.

Kinyume chake, uchambuzi unaonyesha Tanesco italazimika kulipa takribani senti nane za Marekani kwa kWh iwapo itaagiza umeme unaozalishwa kwa maji kutoka Uganda na Zambia, huku gharama zinazotarajiwa za uagizaji kutoka Ethiopia zikijumuisha gharama za usafirishaji zikiwa na makadirio ya senti 7.78 za Marekani kwa kWh.

Bei ya senti 3.0 kwa kWh kama ilivyopendekezwa na Serikali, kwa mujibu wa wachambuzi wa ndani, haitakuwa kivutio kwa wawekezaji wa kimataifa wa kampuni hiyo ambao hawatakubaliana kuwekeza kwenye PPA iliyoongezwa na kufanyia ukarabati mitambo kama inavyohitajika.

Tangu mwaka 2012, Songas imelipa Sh180 bilioni kwa Serikali.
 
Bwawa la umeme la stieglers gorge linawavuruga mafisadi kweli kweli..

SONGAS na yeye amepagawa baada ya kuonekana haitajiki tena.

Mwenzake Simbions walikimbilia mpaka UN kupeleka umbea kwamba bwawa linajengwa kwenye World heritage site ili tu lisijengwe yeye simbions aendelee kuzoa hela za wa Tanzania.. chuma magufuli kikakomaa likajengwa.
 
Hakika Magufuli kwa lile nilimpongeza sana
 
Hizo hesabu daah.
Kuna viongozi hawana huruma na nchi yetu.

Mkataba unaisha na hawajafikia muafaka wa majadiliano tangu 2023. Nchi ipo mikononi mwa wapiga deal
 
Hao Watu Magufuli alikataa Huo Ujinga na kama angekua hai wangekua wamekimbia lakini Tanesco ni Deal tupu zinaendeshwa pale mtu anahongwa dola mil 5 anaidhinishisha sisi tuumie wote kwa kulipa majizi dola mil 250!!!

Mkataba umeisha kwanini tuhangaike na mtu kumlipa????
 
R.I.P JPM
Hakika tutamkumbuka, Kama ilivyosema "00:31 Siku moja mtanikumbuka - Magufuli...."
Magufuli alikataa Huo Ujinga na kama angekua hai wangekua

[00:00] Lakini ninajua watanzania wananipenda pamoja na nyinyi.
[00:06] Ninajua ninayoyafanya ni kwa masilahi mapana ya watanzania.
[00:11] Hasa watanzania masikini.
[00:14] Kwa hiyo ndugu zangu tuendelee kuchapa kazi.
[00:18] Tuendelee kumtanguliza Mungu mbele.
[00:21] Kila mmoja kwa imani yake. Lakini tujenge Tanzania yetu.
[00:26] Mimi ni mtumishi wenu.
[00:28] Na nataka niwaambie ndugu zangu.
[00:31] Siku moja mtanikumbuka.
[00:34] Na mimi ninajua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya.
[00:39] Kwa sababu nimeyatoa sadaka maisha yangu kwa ajili ya watanzania masikini.
[00:44] Kwa hiyo tusimame pamoja tusibaguane kwa vyama.
[00:49] Tusibaguane kwa ajili ya dini zetu, tusibaguane hata kwa makabila yetu.
[00:53] Sisi tuijenge Tanzania.

=
translation of the Swahili text into English, attempting to use British English phrasing where appropriate:

[00:00] But I know Tanzanians love me, including you all.
[00:06] I know what I'm doing is for the greater good of Tanzanians.
[00:11] Especially poor Tanzanians.
[00:14] So, my friends, let's keep working hard. / Let's carry on working hard.
[00:18] Let's keep putting God first.
[00:21] Each one of us according to their faith. But let's build our Tanzania.
[00:26] I am your servant.
[00:28] And I want to tell you, my friends,
[00:31] One day you will remember me.
[00:34] And I know you'll remember me for the good, not the bad.
[00:39] Because I have sacrificed my life for poor Tanzanians.
[00:44] Therefore, let's stand together, let's not discriminate against each other because of parties.
[00:49] Let's not discriminate because of our religions, let's not discriminate even because of our tribes.
[00:53] Let us build Tanzania.

A few notes on the translation choices:
  • "Friends" vs. "Brothers and Sisters": While "ndugu zangu" can literally mean "my brothers and sisters", in this context of a public address, it's often used more broadly to mean "my friends" or "fellow Tanzanians." Using "friends" feels a bit more natural in British English for this setting.
  • "Working hard" vs. "toiling": "Kuchapa kazi" implies diligent work. "Working hard" or "carrying on working hard" captures this better than "toiling," which has a more arduous connotation.
  • "Putting God first" vs. "prioritising God": While both are valid, "putting God first" is a more common idiom.
This translation aims to convey the overall meaning and tone of the original Swahili while sounding natural in English. There might be other equally valid translation choices.

My take: AI katika ubora wake.
 
Mtoa mada ingekuwa vema ungeweka wazi idadi ya makampuni yote yanayotuuzia umeme na bei zake. Pili mahitaji ya umeme vs uzalishaji wa ndani.

Ukisoma hii habari bila kukurupuka na ukiweka hisia pembeni ni wazi umeme wa Songas ni wa bei nafuu kuliko Tuna onunla Uganda na Zambia, na ni nafuu zaidi kuliko unaouzwa na TANESCO. Kama ndivyo ilivyo, kwa nini tusiache vyanzo ghali zaidi na tukadeal na Songas?

Altenatively Songas anaweza kuruhusiwa kuwauzia moja kwa moja watumiaji wakubwa wa umeme na kupunguza mzigo kwa TANESCO huku gesi ikiendelea kuuzwa.
 
View attachment 3140447
Sasa ni rasmi kwamba mkataba wa ununuzi wa umeme (PPA) kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Songas umemalizika rasmi jana Oktoba 31, 2024.

Hatua hii inaiweka Songas kwenye njia ya kudai takriban Dola milioni 90 za Marekani (takribani Sh250 bilioni) kutoka Tanesco ambazo ni malimbikizo endapo hakutakuwa na makubaliano ya kuongezwa muda wa PPA.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Felchesmi Mramba wamelithibitishia gazeti la The Citizen kuhusu kumalizika kwa mkataba huo.

“Umeshamalizika. Kwa bahati mbaya niko kwenye mkutano hivi sasa siwezi kueleza zaidi,” amesema Dk Biteko.

Alipoulizwa ni nini kitakachofuata baada ya kumalizika kwa PPA, Mramba amesema, “siwezi kusema chochote kwa sababu mkataba unamalizika leo (Oktoba 31, 2024) kwa hiyo hatujafanya mipango yoyote.”

Hata hivyo, taarifa zimeeleza kumalizika kwa PPA kuna maana kuwa Songas inaweza kuanza mchakato wa kusitisha shughuli zake katika kituo cha umeme cha Ubungo na kugawa hisa zote zilizobaki kwa wanahisa wake.

Kwa sasa, Serikali kupitia Tanesco, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni ya Maendeleo ya Fedha Tanzania (TDFL) wanamiliki asilimia 46 ya hisa za Songas. Hisa zilizobaki zinamilikiwa na Globeleq.

Fedha za malimbikizo ambazo Songas inaweza kudai kutoka Tanesco zimeongezeka kutoka kiasi kilichokokotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka jana.

Katika ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2022/23, CAG, Charles Kichere alionya dhidi ya kuchelewesha kusuluhisha migogoro mitatu kati ya Songas na Tanesco, ambayo ilikuwa imetajwa kuwa Sh109.07 bilioni wakati huo. Mapitio ya CAG yalionyesha migogoro inayojirudia ambayo haijasuluhishwa tangu mwaka 2022.

Kichere alisema Tanesco ilipinga malipo yenye thamani ya Sh67.94 bilioni.

Hata hivyo, Songas iliendelea kujumuisha gharama za tozo za ukarabati wa mali (sinking) kwenye ankara za kila mwezi kuanzia Agosti 2022 hadi Juni 2023, zikiwa na thamani ya Sh29.34 bilioni, licha ya taarifa ya mgogoro iliyotolewa na Tanesco Desemba 2022.

"Zaidi ya hayo, ankara ya Januari 4, 2023, yenye thamani ya Sh23.94 bilioni na Dola milioni 4.02 kwa Desemba 2022, ilizua mgogoro kuhusu deni la Sh11.78 bilioni la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayodaiwa na TRA kutokana na kukosekana kwa nyaraka za kuunga mkono,” alisema CAG mwaka jana.

Mei, mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alilieleza Bunge kwamba, Tanzania ingezingatia masilahi ya kitaifa kabla ya kutoa ruhusa ya kuongeza mkataba kati ya Tanesco na Songas.

Alisema timu ya majadiliano ya Serikali iliundwa Aprili 2023 na kwamba, majadiliano yalitarajiwa kukamilika kabla ya kumalizika kwa mkataba.

Ingawa Serikali imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa megawati 662 kutokana na kuwashwa kwa mitambo mitatu kati ya tisa katika mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP), umuhimu wa vyanzo mbadala bado unahitaji kusisitizwa.

Uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia hutoa nguvu muhimu kwenye gridi ya Taifa hasa wakati wa ukame.

Wataalamu wa ndani wanasema kwa senti za Marekani 4.9 kwa kilowati kwa saa (kWh), Songas imekuwa ikiuzia Tanesco umeme kwa viwango vya bei nafuu zaidi.

Katika pendekezo la kuongeza mkataba wa PPA kwa miaka sita, kampuni hiyo ilipunguza bei hadi senti 3.9 za Marekani kwa kWh bila kujumlisha gharama za gesi asilia.

Gharama za gesi zinazotarajiwa kujadiliwa zikijumlishwa bei itakuwa senti 6.82 za Marekani kwa kWh.

Kwa mujibu wa watu walio na ufahamu kuhusu suala hili, bado ni chini ya senti 11 za Marekani kwa kWh ambazo Tanesco inawatoza wateja wake.

Kinyume chake, uchambuzi unaonyesha Tanesco italazimika kulipa takribani senti nane za Marekani kwa kWh iwapo itaagiza umeme unaozalishwa kwa maji kutoka Uganda na Zambia, huku gharama zinazotarajiwa za uagizaji kutoka Ethiopia zikijumuisha gharama za usafirishaji zikiwa na makadirio ya senti 7.78 za Marekani kwa kWh.

Bei ya senti 3.0 kwa kWh kama ilivyopendekezwa na Serikali, kwa mujibu wa wachambuzi wa ndani, haitakuwa kivutio kwa wawekezaji wa kimataifa wa kampuni hiyo ambao hawatakubaliana kuwekeza kwenye PPA iliyoongezwa na kufanyia ukarabati mitambo kama inavyohitajika.

Tangu mwaka 2012, Songas imelipa Sh180 bilioni kwa Serikali.
Hili si la Magufuli wabaya wake msimzushie
 
Wakati wanagundua hii gesi tulilishwa uongo mwingi sana na kikwete kuwa tatizo la umeme litaisha na gharama itapungua kuliko Nchi yeyote afrika lakini tumejionea matokeo yake imekuwa kinyume chake.Na Kwa Sasa lazima wakafungue kesi za kimataifa watupige Hela nyingi maana mabeberu wamegundua uongozi uliopo ni legelege na Kila beberu anajipigia pesa jinsi atakavyo
 
Tanzania iagize umeme toka Ethiopia? Umechanganyikiwa? Na tungerenew mkataba, hayo madeni yangefutiks?
 
Hizo hesabu daah.
Kuna viongozi hawana huruma na nchi yetu.

Mkataba unaisha na hawajafikia muafaka wa majadiliano tangu 2023. Nchi ipo mikononi mwa wapiga deal
Kwanza mnajadiliana nini na muafaka gani ? Mkataba umeisha, tupeana mikono ya kwa heri, basi. Mijadala hiyo ndio mianya ya rushwa.
 
tangazo la songas lime pendekea songas kwa kila sehemu ni songas
 
Back
Top Bottom