Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Nimewasikia wengi wakilitumia neno ndoa halali. Wakisema ni mume wangu halili, wengine wakisema mke wangu halali. Wengine wakisema kuwa wamefunga ndoa halali n.k.
Je, mume anaporudi nyumbani asubuhi bila kusema alikuwa wapi hiyo tutaendelea kuiita ndoa halali? Mke na mume kila mmoja hajui kipato cha mwenzie hiyo tutaendelea kuiita ndoa halali? Wanandoa wanapigana mpaka wanatoana meno na ngeu, je, hiyo tutaendelea kuiita ndoa halali?. Wanandoa wanashindana kuchepuka kwa kukomoana, je hiyo tutaendelea kuiita ndoa halali?
Jibu ni HAPANA.
Je, vijana wawili waliovutana wakaamua kuishi pamoja kama mke na mume pasi na ugomvi, visasi huku wakiepuka michepuko hiyo tuiite ndoa haramu kwakuwa Mchungaji hajaifungisha? Wapenzi wawili waliovutana wakaishi na kuzaa watoto kwa furaha hiyo tuiite ndoa haramu kwakuwa sheikh hajaifungisha?
HAPANA.
Ukweli ni kwamba sheikh au Mchungaji hawezi kuifanya ndoa iwe halali au haramu. Bali wanandoa wenyewe ndio wanaweza kuifanya ndoa yao iwe halali au haramu.
SWALI: Je, ndoa yako ni halali au haramu?