Hii ndio maana ya kushauri kwa Vitendo

Hii ndio maana ya kushauri kwa Vitendo

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
HII NDIO MAANA YA KUSHAURI KWA VITENDO

SANT'AGATA, Bolognese ni makao makuu ya supercars aina ya Lamborghini. Maranello, Modena, ndio HQ ya Ferrari. Kutoka Sant'Agata kwenda Maranello ni umbali wa kilometa 34. Miji hiyo ipo Italia.

Mwasisi wa Ferrari ni Enzo Ferrari na Lamborghini godfather wake ni Ferruccio Lamborghini Enzo alikuwa dereva wa mbio za magari mstaafu aliyeasisi magari ya Ferrari. @Ferruccio alikuwa mhandisi bingwa wa kuunda trekta, kupitia kampuni yake ya Lamborghini Trattori.

Unaweza kuendesha trekta upige nalo misele mjini? Jibu ni hapana. Hivyo, ukiwa na kiwanda cha trekta itakubidi ukabishe hodi kwa muuza magari. Ndivyo ilivyokuwa kwa Ferruccio.

Mwaka 1958, Ferruccio alinunua Ferrari 250 GT (siti mbili). Kisha akavuta mikoko mingine kutoka Ferrari, 250 GT SWB Berlinetta na 250 GT 2+2 (siti nne).

Baada ya kuendesha magari hayo, Ferruccio aligundua magari ya Ferrari ni mazuri ila yalikuwa na kelele. Klachi hazikuwa sawa. Yalikuwa rafu barabarani. Ndani hayakuwa na mwonekano mzuri.

Mwaka 1963, Ferruccio alifunga safari kutoka Sant’Agata mpaka Maranello, kumtembelea Enzo na kumweleza kasoro za Ferrari. Alikusudia kumpa ushauri wa kujenga ili aboreshe magari yake. Lengo la Ferruccio lilikuwa kuendelea kufurahia Ferrari kama mteja, hasa baada ya kasoro alizotaja kufanyiwa kazi.

Kikao cha Ferruccio na Enzo hakikuisha salama. Enzo alimwona Ferruccio hajui kitu. Mbunifu wa matrekta anajua nini kuhusu magari viwango vya GT (Gran Turismo)? Enzo alimjibu Ferruccio: “Acha mimi nitengeneze magari. Wewe endelea kuunda trekta.”

Ferruccio aliondoka Maranello akiwa na hasira. Mpaka anafika Sant’Agata, tayari alishapata wazo la kuunda magari bora kuliko Ferrari. Kisha, Ferruccio aliwatafuta mainjinia wa zamani wa Ferrari, akiwemo aliyekuwa Injinia Mkuu, Carlo Chiti na Meneja Maendeleo, Giotto Bizzarrini. Akawaajiri.

Wakatengeneza gari la kwanza Lamborghini 350 GT, ndani ya miezi minne. Kisha Lamborghini Miura. Sifa nyingi zilikuwa kama Ferrari lakini wakaboresha. Mfano kuweka injini nyuma ya dereva na milango kufunguka kwa juu. Lamborghini ikawa moto. Ushindani ukawa mkubwa.

Somo; shauri, kama unapuuzwa, fanya wewe kwa ubora unaoutaka.

Nawapa challenge wote waliosema gari la Masoud Kipanya ni baya, waunde lao kama Ferruccio alivyomshauri Enzo kwa vitendo. Enzo alipuuza ushauri wa maneno wa Ferruccio. Magari ya Lamborghini yakamzindua, akafanyia kazi makosa.

#BeInspired

Credit: Luqman MALOTO
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom