Hii ndio maana ya uzalendo kwa vitendo

Hii ndio maana ya uzalendo kwa vitendo

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wakti wengine wanaonyesha uzalendo kwa kuvaa nembo na tai zenye bendera ya Tanzania, wanyama wakuu wa tanzania na mlima Kilimanjaro na Zanzibar tu huyu kijana ameamua kutufundisha maana halisi ya uzalendo.
Hivi ni kweli ni yeye tu aliyekuwa ameiona ndege ikianguka kwenye maji?

Tunajua kuna wengi sana waliiona ikianguka lakini walikuwa akisubiri maagizo kutoka juu yanaoambatana na barua inayoonyesha posho zao zitakuwaje na ikiwezekana walipwe kabla ya kuondoka kuelekea kwenye tukio na vifaa vya uokozi.

Ni nani ametoa amri ya kuivuta ndege nchi kavu badala ya kuhangaikia kumaliza kuwaokoa waliomo kwenye ndege kwanza. Akipatikana mtu huyu nashauri akamatwe kwa mujibu wa sheria, avuliwe cheo, afukuzwe kazi na apelekwe mahakamani.

 
Huyu mzalendo anadai kwamba alishuka majini kwenye kioo cha rubani, akawapungia, wakamwambia avunje kioo ili watoke. Lakini alizuiwa. Inasikitisha sana.
 
Kumbe alikuwa na wenzie! Kwa nini wengine hawatajwi na hawajazawadiwa kama yeye? Na yule aliyemwokoa baada ya kupigwa na kamba na kuzirai, je? Hastahili naye kutuzwa kwa kumwokoa Majaliwa?
 
Kumbe alikuwa na wenzie! Kwa nini wengine hawatajwi na hawajazawadiwa kama yeye? Na yule aliyemwokoa baada ya kupigwa na kamba na kuzirai, je? Hastahili naye kutuzwa kwa kumwokoa Majaliwa?
yeye ndiye steringi
 
Back
Top Bottom