Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Huyo mama wa kizungu anaonesha mtazamo wa wazungu walio wengi dhidi ya Afrika, ingawaje hata huyo mtoa mada ni mzungu. Lakini, mtoa mada inaonekana anaongea hivyo baada ya nchi yake, Ugiriki, kupigika kiuchumi. Mama huyo anahofia maisha yao ya mbeleni endapo Afrika itaamka kiakili, kiuchumi, na kisiasa. Na anayekuja kuamsha Waafrika ni Mchina. Ingawaje Mchina anatafuta influence pia kupitia 'soft power'. Kwa upande mwingine Mchina ana ma-deal ya kuumiza kama Hayati Dr Magufuli alivyoongelea deal la bandari ya Bagamoyo, lakini inaonekana wapo tayari kubadilisha terms kwa mfano wa huyo Prof.
Afrika tunatakiwa ku-deal na wazungu kama China anavyofanya. Mchina apigi makelele ya kumshughulikia mzungu kama baadhi ya viongozi wa Afrika kama hayati Daktari JPM. Hayati Dr JPM aliwaambia kuwa tunaamka na kuonesha kweli kuamka, ndipo alopigwa zengwe kila kona. Sawa na akina Gadaffi kuwa na hari ya kuamsha waafrika.
Tuwe na mkakati wa kuamka kimya kimya. Hata pale tutakapoanza kuamka, tujifanye tumefumba macho.
Ila kwa hapa nyumbani ninashaka sana na mrithi wa hayati Daktari JPM kama anaelewa hasa nia ya ndani ya wazungu.