Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Kweli kabisa sasa hivi mufindi Kuna viwanda vingi vya mchina kwa vijana wanaotafuta maisha bila kujali ugumu wa kazi njoo mufindi hakika hautojuta
Nje ya mazao makuu yanayofanya vizuri Kama mbao, mahindi, viazi maua na matunda. Ukiangalia Mkoa wa Iringa kuanzia Ruaha mbuyuni au mtera kuelekea Iringa town hadi ufike Makambako, asubuhi na mapema utakutana na makundi makubwa ya vijana maeneo ya Ifunda, Rungemba na Mafinga wakielekea kwenye viwanda vya kuchakata mbao na mazao, Jambo ambalo unaona limesaidia kwa kiasi kikubwa uhaba wa ajira kwa vijana hususan wanawake. Hali hiyo imeimarisha uchumi binafsi na mchango wa mtu mmojamoja kuchangia Pato la taifa.
 
Kwani mkoa WA tanga ipo mingapi?
Tanga iko tofauti na mikoa mingine.Kuna Tanga wilaya,na kuna Tanga Mkoa,Tanga wilaya ndio Tanga jiji.Wilaya zingine bado ni halimashauri za miji.Huwenda hii ikawa ni Tanga city(sio mkoa mzima wa Tanga).Kama sivyo naomba maelekezo.
 
Kwani mkoa WA tanga ipo mingapi?
Kuna wilaya ya Tanga,ndio jiji(city).Na kuna mkoa wa Tanga,hiyo wilaya ya Tanga,na wilaya nyingine ziko ndani ya huo mkoa wa Tanga.Nafikiri wilaya nyingine za mkoa wa Tanga,bado ni halimashauri za miji.Kama nimekosea,nifahamishwe.
 
Kwa hyo tanga kuna mikoa miwili?
Tanga iko tofauti na mikoa mingine.Kuna Tanga wilaya,na kuna Tanga Mkoa,Tanga wilaya ndio Tanga jiji.Wilaya zingine bado ni halimashauri za miji.Huwenda hii ikawa ni Tanga city(sio mkoa mzima wa Tanga).Kama sivyo naomba maelekezo.
 
Tanga iko tofauti na mikoa mingine.Kuna Tanga wilaya,na kuna Tanga Mkoa,Tanga wilaya ndio Tanga jiji.Wilaya zingine bado ni halimashauri za miji.Huwenda hii ikawa ni Tanga city(sio mkoa mzima wa Tanga).Kama sivyo naomba maelekezo.
Sijui mnabishana nini,hapo juu imeandikwa Tanga CC
 
MApato ya serikali hayapimi unafuu wa maisha wa sehemu ww mbona ukiangalia mtu wa hali ya chini aliyepo makambako anamaisha mazuri kuliko njombe
Kupata kichekesho kama hiki jiunge na Mdatchu blog πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ .Pesa hizo zinakusanywa kutoka mbinguni au kutoka kwenye shughuli za wananchi?

Mkuu hicho kijiji chenu cha Makambako kinachekesha,Mwaka huu wa fedha Njombe TC tuna hit 7.0 bln ya makusanyo ya ndani wakati kijiji chenu hata 3b haijulikani mtapata lini.Unapozungumzia mapato ya Mkoa wa Njombe unazungumzia Njombe TC na Njombe DC.

Kingine just kwa taarifa yako own source zinatumika kutoa huduma kwenye Halamshauri husika,zinduka mnapotea na mitumba yenu huko.
 
Bila Kahama na Makambako hii report ni ya kupika.
 
Bila Kahama na Makambako hii report ni ya kupika.
Uwe unasoma kabla ya kukurupuka ku comment mkuuπŸ˜‰πŸ˜‰ ,Kahama ndio iko kwenye list hicho kijiji cha Makambako size yake ni Nanayamba,Ifakara,Liwale,Masasi na tumiji twingine dizaini ya hiyo.Hiyo orodha ni kwa ajili ya heavy weight.

Ukiangalia trend ya Makusanyo kwa mwaka huu unaoisha june 2021,utakuta Halamshauri za Geita TC,Kahama MC,Chalinze DC, Tarime DC,Mkuranga DC na Njombe TC zinakuja kwa kasi sana kwenye mapato seems hayo maeneo watu wana pesa sana ukiacha Majiji makubwa
 
Kichwa cha habari kilifaa kuandikwa ,,miji 40 inayoongoza kwa makusanyo.
Nilichelea kuandika hivyo kwa sababu mambo yanabadilika badilika sana kadiri mda unavyoenda,Na uhakika List ya mwakani Halmashauri nyingi zitaanguka na mpya kuingia kulingana na mwenendo wa makusanyo ya kufikia mwezi wa pili 2021.
 
Endelea kujifariji na njombe yko ila kumbuka mapato yanabadilika kila mwaka na kunaa baadhi ya sekta Kama majengo mabango walichukua mapato serikal kuu saiz yamerud halimashaur na usilo lijua na upo usingizini njombe tc inaokolewa mapato na vijiji mjini kupo hoi ndo maana hata ugawaji walingangania vijiji ukienda ile halimshaur ya mji haina utofati na wilaya za vijijin ko unavoendelea kujiliwaza lazima upigwe gap tu na wenzio tumesoma mapato vizuri tatizo unatuoletea makadirio ambapo kimakusanyo njombe imekusanya bln 4.7 pitia kwenye page yao usitupotoshe alafu hiyo makambako unayo iita Kijiji ndo mji kwasasa mkubwa kimkoa ko endelea kula mtori nyama ipo chini utaongea sana mk inazidi kusonga mbele
 
Bila Kahama na Makambako hii report ni ya kupika.
Jamaa anaipamba njombe wee alafu watu wa njombe wanahamia makambako hahaha makambako imekuwa mji mkubwa kuliko njombe na bado wataisoma tu mapato yanabadilika kila mwaka nenda kaanga wamejengewa soko wote wamerundikana barabaran si mji wa kishamba huo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamaa umeongea kwa kutia huruma sana.

Mkuu Acha kutapatapa,taarifa iko rasmi kutoka Tamisemi sasa hiyo ya mdomoni mwako utaiamini wewe Ili ujifariji.Kusomea mapato sijui ndio kozi gani kama unashindwa kuelewa kwamba vyanzo vikuu vya mapato kwenye Halmashauri zote nchini vimegawanywa kwenye category mbili,moja vyanzo halisi kutoka shughuli za kiuchumi ndani ya Halmashauri na pili ni ruzuku ya maendeleo kutoka serikali kuu ambapo kwa Halmashauri ni Kati ya Mil.900--1.5bln kutegemea hadhi ya Halmashauri husika eg DC,MC au CC.

Ndio maana unaona Tamisemi ni 5.6 vs 4.7bln.So hiyo ndio formula unatakiwa kuelewa.

Kwamba Vijiji vina mapato mengi kuliko Mji mkubwa wa Mkoa Makambako [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mkuu kubali tuu kwamba hicho kijiji cha Makambako bado saaana kuliko kuweweseka na kulia lia mara mabango mara TRA yaani utadhani hivyo havipatikani Njombe Mjini.

Kwa taarifa yako hadi kufikia Juni 30,2021,Njombe itavunja rekodi ya mapato kufikia 7 bln ambayo haitakaa ije kufikiwa na hicho kijiji cha wachuuzi.

Soma hiyoo [emoji116][emoji116]
View attachment 1783672View attachment 1783673
 
Wewe labda una tatizo uelewa.Wanaohamia huku sio wawekezaji ni wachuuzi,wawekezaji wakabaki Njombe mkuu.

Yaani Mji unazidi kuchanua na kub feature kwenye lists ya Miji yenye mapato mengi Kitaifa afu kibwengo mmja anakuja kupayuka ,haya si ni maajabu?

Eti napamba,kwa nini nipambe wakati takwimu zinaongeza? Mapato yenu yanabadilika kwenda chini huku wenzetu yakibadilika ki upwards mfano 2017/18 mapato =3.5 bln,2018/19=5.6bln,,2019/20=6 plus bln sasa hicho kijiji mnachohangaika nacho veeepe?

Shindaneni na Nanyumbu TC ndio level yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…