Tetesi: Hii ndio picha ya Diamond iliyowekwa ikulu

Tetesi: Hii ndio picha ya Diamond iliyowekwa ikulu

Huyo Diamond ni sawa na maji ya moto yatapoa tu! Siamini kabisa kama ana mchango wowote kwenye uchumi wa nchi hii. Tatizo miziki ya vijana wa kizazi hiki ikiwemo ya Diamond haina ubunifu kama ilivyokuwa ya wazee wa zamani ambayo haichuji. Nyimbo za sasa ni sawa na moto wa mabua unaowaka haraka na kuisha haraka. Mi binafsi sioni haja ya huyu mtu kupaishwa ki hivyo. Kwa hivi karibuni mtu aliyeitangaza Tanzania ni Mbwana Samata na si huyo diamond! Kama kweli ikulu kuna hiyo picha, nawashauri waweke ya Samata badala ya hiyo!
 
najiuliza kama kenya wameweka picha ya lupita nyong'o hadi vyooni mwao!!!!!hivi angekuwa amewahi kushinda a grammy award si angewekwa hadi kwenye magari ya ikulu!!!!!!!!wabongo kwa ushamba bana....yani kwa hizi nyimbo za viswahili na subtitle za broken english!!!!...tumechelewa sana tanzania...gadem
 
Nyumba yake huwa anaita ikulu. Tunaomba screen shot ya ukuta wa Ikulu ya magu ikiwa imetundikwa iyo picha.
 
Diamond ameajiri vijana wengi mno wengi tayari wamejenga wanaendesha magari kupitia kampuni zake kama WCB record label, WCB production house, WCB photos nk.... Kwenye show zake watu wanatengeneza mamilioni kwa siku moja kuanzia wandaaji wamachinga nk... Kuna watu instagram wanaendesha family zao kupitia story za Diamond... So nje ya mapinduzi yake kwenye sanaa nzima ya Tanzania ametekeleza ajira nyingi sana.

Unataka kuniambia hapo ikulu kuna picha za Bakhresa, Mengi. Mo, etc...Maana kama kuajiri watu hawa wanastahili zaidi....Na mapinduzi gani ya sanaa aliyoyafanya?....
 
Huyu sio mfanyabiashara huyu ni gwiji la sanaa lililofanya makubwa ambayo hayakuwahi kufanywa na wengine huko nyuma. Ni kijana kutoka uswahilini hasiyekulia maisha mazuri ila kawa mfano kwa vijana wengi wanaoamini mfumo mmoja wa kufanikiwa.
Diamond ni kama Filbert Bayi ni kama Juma Ikangaa ni kama Kanumba ni kama Magufuli ni kama Msuguli watu awa hawatokei mara nyingi ukiwapoteza ndio unajua umuhimu wake.
Una akili sana kiongozi [emoji106]
 
Kuna mafanikio binafsi na ya kitaifa. Diamond binafsi lakini ukisema kaletea taifa sifa ni zipi. Tuna serengeti na bado baadhi ya nchi wala hawajui Tz itakuwa diamond. Acheni ushabiki katika mambo muhimu.
 
Hata wale walioshinda kukaa uchi big brother mliandamana. What a Nation. Tunataka ukitoka nje ya Tz ukisema mimi natoka Tz wakujue huko hatujafika.
 
Back
Top Bottom