Hii ndio sababu CIA na Mossad kuifanya Tanzania iwe tatu bora kwa upelelezi Duniani enzi za mwalimu

Hii ndio sababu CIA na Mossad kuifanya Tanzania iwe tatu bora kwa upelelezi Duniani enzi za mwalimu

Wakitaka kupiga picha mahali popote wanapiga tu 40 years back .. aerial photos technology
 
Habari Wanajamvi,

Enzi za mwalimu kulikuwa na Uzalendo uliotukuka. Watanzania walikuwa makini na waadilifu katika shughulu zao.

Majasusi wawili kutoka Marekani na Israel CIA na Mossad walikuja nchini kupeleleza kwa kisingizio cha utalii na kuomba tour guide in advance.

Walipofika tu Dar Int Airport kachalii tu ndio aliwapokea akawa tour guide wao.

Baada ya wiki mbili wakamaliza ziara yao. Yule Dogo kachalii akawapeleka uwanja wa ndege. Wakakumbatiana kuagana na kumpa tip. Kabla hawajaingia kuchek in Dogo akawaimbia.

Zile picha mlizopiga kisiri na kamera zenu za kalamu Ikulu, kambi za jeshi na bunge hazitatoka wala hamtaziiona. Ila zile mlizopiga Serengeti, Zanzibar, ngorongoro tumewaachia mtaziona hili mtutangazie utalii.

Hawa Majasusi walichoka wakabaki midomo wazi Dogo akageuza na kutokomea.
Chai ya kitoto
 
Hahahahaha hao uliowasema wakitaka kupiga picha wala hawana haja Yakuja Mpaka Nchini.
 
Back
Top Bottom