Hii ndio sababu halisi kwanini watu wengi sana siku hizi wanaota ndoto wapo shule ya msingi au sekondari

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Wakati wewe mtanzania ukiwa unaendelea na mchakato wa kuwahamisha watoto wako kutoka kwenye shule za kiingereza ( English Mediums) na kuwarejesha kwenye shule za Kayumba, wacha nikuambie kwanini umekuwa ukiota ndoto upo shule ya msingi au sekondari unafanya mitihani etc.

Wanao jiita mitume na manabii wasasa jibu lao huwaga ni moja tu. Kwamba eti kuna watu wanakuroga kukurudisha nyuma. Ukumbafu mtupu.

Ndoto za kuota umerudi utotoni zina tafsiri zaidi ya mia 4.

Tafsiri hutegemeana na mtu na mtu na hutegemeana unapitia kipindi gani wakati unaota ndoto hiyo.

Kwa mfano katika kipindi ambacho unapitia magumu na unaona hauna msaada wowote wa kimwili na kiroho halafu ukaota ndoto upo shule ya msingi,maana yake ni kwamba hutakiwi kukata tamaa kwa sababu hauko peke yako. Kuna nguvu kubwa kushinda wewe ambayo inatazama kila kitu unacho kipitia na ipo tayari kukutetea/ kukusaidia.

Kwanini? Kwa sababu ndoto ni kioo kinacho kuonyesha wewe ni nani/ nafasi yako katika ulimwengu wa roho.

Kama katika ulimwengu wa roho ( ndoto ) wewe ni mtoto basi tafsiri yake ni kwamba katika ulimwengu huo huo wa roho una wazazi pia ( baba na mama ), mabibi na mababu etc.

Kwa hiyo unacho takiwa kufanya ni kusonga mbele kwa sababu ipo nguvu inayo kulinda katika ulimwengu wa roho.

BACK TO MY THREAD.

Katika nyakati za hivi karibuni, watu wengi sana sio tu hapa Tanzania but almost Afrika yote na dunia nzima kwa ujumla wamekuwa wakilalamika kwamba wanaota ndoto wapo shule ya msingi au primary( Many times wapo kwenye chumba cha mitihani)

TAFSIRI YA LIKUD👇👇👇

Kuna masomo muhimu ambayo hukuyazingatia ulipokuwa shule ya msingi au uliyaacha ulipokuwa shule ya sekondari.

Unatakiwa kuyasoma upya masomo hayo utake usitake.

Hayo masomo yalikuwa ni muhimu sana katika maisha yako halisi.

Moja kati ya masomo hayo ni : HISABATI.

Amini kwamba matatizo mengi na changamoto nyingi unazo kutana nazo kwenye maisha yako ni kwa sababu huna maarifa ya HISABATI.

Hisabati ni ufunguo halisi wa kila kitu hapa duniani. Nasema kila kitu mkuu.

Mimi niligundua ukweli huu nikarudi kusoma HISABATI. Nilianza kusoma vitabu vya form 1-4, nikaenda cha Advance ( Both Basic Applied Mathematics na Pure Mathematics) sikuishia hapo nikasoma ( self taught ) kozi zote za Hesbabu zinazo fundishwa kwenye Degree ya Hisabati.

Na sasa hivi nimekuwa enlightened. Ninayatawala maisha yangu. I am living in the future.

Kuna baadhi ya vitu hapa duniani huwezi kuvielewa kama hujui hesabu.

Soma Hisabati. Ukianzakusoma hisabati basi hata hizo ndoto zitaanza kutoweka

Utakuja unishukuru.
 
Na ndo naotaga nipo kwa paper lake alafu kichwani 0
 
Mimi niligundua ukweli huu nikarudi kusoma HISABATI. Nilianza kusoma vitabu vya form 1-4, nikaenda cha Advance ( Both Basic Applied Mathematics na Pure Mathematics) sikuishia hapo nikasoma ( self taught ) kozi zote za Hesbabu zinazo fundishwa kwenye Degree ya Hisabati.

Na sasa hivi nimekuwa enlightened. Ninayatawala maisha yangu. I am living in the future.

Kuna baadhi ya vitu hapa duniani huwezi kuvielewa kama hujui hesabu.

Soma Hisabati. Ukianzakusoma hisabati basi hata hizo ndoto zitaanza kutoweka
Nzuri, kujifunza

Na pia ubongo kwenye kubumba ndoto huwa unapendelea kuchukua eneo lenye kumbukumbu nyingi.

Na wengi wametumia muda mwingi shule tena walikuwa na ubongo unaopokea bado mambo mapya kwa kasi kubwa.
Miaka saba na sita si mchezo tena kwa mtoto anayekua.

Matokeo yake ndoto nyingi zinakuwa staged huko
 
Katika ulimwengu wa ROHO kuota upo shule hii humaanisha unsolved issue kuna either kwako halijawa solved

Mimi hii ndo huwa tafsiri yangu
Lakini ile tafsiri ya watu kuwa ukiota upo shule utarudishwa nyuma au upo nyuma haileti maana .

Pia ndoto zinazohusu maisha ya MTU zizotoka katika subconscious mind yake huwa zipo symbolically
 
Nzuri, kujifunza

Na pia ubongo kwenye kubumba ndoto huwa unapendelea kuchukua eneo lenye kumbukumbu nyingi.

Na wengi wametumia muda mwingi shule tena walikuwa na ubongo unaopokea bado mambo mapya kwa kasi kubwa.
Miaka saba na sita si mchezo tena kwa mtoto anayekua.

Matokeo yake ndoto nyingi zinakuwa staged huko
Big up sana mkuu. Nimejifunza kitu kipya hapa.
 
Nzuri, kujifunza

Na pia ubongo kwenye kubumba ndoto huwa unapendelea kuchukua eneo lenye kumbukumbu nyingi.

Na wengi wametumia muda mwingi shule tena walikuwa na ubongo unaopokea bado mambo mapya kwa kasi kubwa.
Miaka saba na sita si mchezo tena kwa mtoto anayekua.

Matokeo yake ndoto nyingi zinakuwa staged huko
Umejibu vizuri mkuu na kitaalamu.

Hata katika ufanyaji Kazi wa universe upo hivyo kile ambacho kitakuwa kingi ndo kitakutokea katika maisha Halisi.

Mfano ukitumia muda mwingi kuwaza negative utapata negative the same ukiwaza positive.

MTU aliyesoma hadi chuo kikuu huyo MTU kafanya mitihani mingi hivyo uwezakono wa yeye kuota yupo shule ni mkubwa. Sana
 
Nafikiri hii ndio tafsiri sahihi. LIKUD anazingua
 
Umejibu vizuri mkuu na kitaalamu.

Hata katika ufanyaji Kazi wa universe upo hivyo kile ambacho kitakuwa kingi ndo kitakutokea katika maisha Halisi.

Mfano ukitumia muda mwingi kuwaza negative utapata negative the same ukiwaza positive.

MTU aliyesoma hadi chuo kikuu huyo MTU kafanya mitihani mingi hivyo uwezakono wa yeye kuota yupo shule ni mkubwa. Sana
100% Fact.
 
Back
Top Bottom