funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,468
- 31,952
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!
Kazi na Utu...!
Kwa fahari kubwa sana na kwa tabasamu lisilo kifani na nikiwa kama mdau wa muda mrefu hapa JF mwenye kuipambania kero ya kutokuwepo kwa bima ya afya kwa wote ninayo furaha kubwa sana kutambua usikivu wa Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM SAMIA SULUHU HASSAN pamoja na wasaidizi wake ndani ya chama na Serikali na hatimaye leo hii tumeanza utekekezaji wa suala la msingi kwa ustawi wa maisha ya watanzania.
Wakati tunapata uhuru yapo mambo makubwa matatu yaliyoainishwa kama maadui wa taifa ikiwemo Ujinga,Maradhi na Umasikini.
Matatu haya ndio yamekuwa Chachu ya muelekeo au dira kwenye Chama na Serikali na hivyo kwa uangalifu mkubwa imetupasa kuyafanyia kazi,kuyaishi,kuyahoji ,kuvutana na kushauriana kadri inavyofaa.
Chokochoko zote ndani ya Tanzania zitahusisha mambo haya matatu na sio vinginevyo.
Mwaka 2015 wakati Maria Sarungi akiwa binti mrembo na pengine akiwa kwenye haiba ya uzalendo na mwenendo wa harakati za kujenga nchi aliandaa mdahalo wa wagombea Urais uliohusisha JF ukitaka kujua wananchi tuna maswali gani kwa wagombea.
Kumbukumbu zangu ni kuwa mdahalo huo ulirushwa live hapa JF na nilibahatika kuhoji swali muhimu kuhusu uanzishwaji wa bima ya afya kwa wote.
Majibu ya kipindi kile kutoka kwa wagombea Urais ikiwemo mwakilishi wa mgombea wa CCM hayakuniridhisha na hayakuiridhisha jamii ya watanzania.
Swali langu kipindi hiko lilitokana na mpango wa Rais wa marekani kuhusu bima ya afya kuwagusa masikini ujulikanao kama OBAMA CARE na pia lilihusu uzoefu wangu wa kuona na kutabiri kuwa ipo siku misaada ya mataifa ya nje haitokuwepo....HAPA UTANIONA NIKITUMIA SLOGAN YA KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Kwa miaka yote hii nimekuwa nikifuatilia utekelezaji na kuona ni mwanasiasa yupi hasa atakuwa na kifua au tumbo(GUTS) la kuibeba sera hii ngumu duniani ya BIMA YA AFYA KWA WOTE au iite Universal Health Insuarance.
HATIMAYE ;Rais Samia Suluhu Hassan anaibuka kuwa mwanasiasa pekee nchini Tanzania na pengine bara hili la Africa kuibeba kikamilifu agenda hii ngumu na kuiweka kwenye utekekekezaji.
Rais Samia anaonesha consistency ya kipekee kwamba ajenda hii lazima ifikie mwisho na itekekezwe mosi kwa kuweka Sera/sheria rasmi ya BIMA YA AFYA KWA WOTE.
PILI..:Wakati nikitafakari kuwa suala hili litakuwa ni usanii wa kisheria usiotekekezeka nakutana na Jambo kubwa sana kwenye Ilani ya CCM 2025-2030.
Katika ahadi za Ilani ya CCM 2025-2030 Sekta ya Afya inatajwa mara moja tu na inatajwa na kuhusishwa na jambo moja tu yaani BIMA YA AFYA KWA WOTE.
REJEA SURA YA 2 C YA ILANI YA CCM 2025-2030.
Hii ni ishara kubwa sana kwa wanasiasa na watendaji kutambua Mtawala wa sasa ametaka na kumaanisha nini kwenye sekta ya afya Tanzania.
BIMA YA AFYA KWA WOTE NI NGAO DHIDI YA UTEGEMEZI !
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!