Hii ndio sababu kubwa kwa nini ujiwekee malengo yasiyowezekana kwenye maisha yako

Hii ndio sababu kubwa kwa nini ujiwekee malengo yasiyowezekana kwenye maisha yako

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kama unaamini Mungu ni wa Yasiyowezekana, alafu wewe unavimalengo vinavyowezekana, au unaogopa kukusudia jambo kubwa linaloumiza kichwa, humuamini huyo Mungu.

Malengo au lengo lisilowezekana katikati ya malengo yako litakusaidia kwanza wewe ubadilike ili litokee. Wewe kabla ya kutekeleza na wewe baada ya kutekeleza ni watu wawili tofauti. Kama unamuamini Mungu jipangie vitu vya kawaida ila changanya kimoja kisichowezekana kuonyesha wewe ni binadamu unayemuamini Mungu wa yasiyowezekana. Hata hivyo imeandikwa "Awazavyo mtu moyoni mwake ndivy alivyo", kwa maana kama umeweza kuwaza kicho kitu kikubwa tayari Mungu aliyekupa huo uwezo wa kuwaza hivyo ametoa na uwezo wa kuwa mtu wa hivyo, kutekeleza. Hivyo tu. Ndio maana kama unamipango alafu ule wa kwanda mbinguni na kuishi na Mungu mahali bora kuliko hii dunia huna, wewe bado ni mtu wa Yanayowezekana.

Mungu ndio Muasisi wa kuwa na malengo yasiyowezekana. Aliwahi kumtoa Yesu ambaye anasifa zote za uungu afe wakati Mungu hapatikani na mauti. Alirisk kumfanya awe na umbile la mwanadamu ili iwezekane kufa na kufufuka ili kifo hicho kiwe mbadala wa kifo cha milele cha yeyote atakayemuamini huyo Yesu
 
Nimeelewa bandiko lakini kwanini niweke malengo yasiyowezekana? Huoni kama ni kupoteza muda? Elewa maana ya hilo neno kwanza yasiyowezekana

Ungesema kuweka malengo makubwa kushinda uwezo wetu hapo ningeelewa sababu akili/ nguvu/uwezo wetu unapoishia ndio Mungu anapoanza
 
Nimeelewa bandiko lakini kwanini niweke malengo yasiyowezekana? Huoni kama ni kupoteza muda? Elewa maana ya hilo neno kwanza yasiyowezekana

Ungesema kuweka malengo makubwa kushinda uwezo wetu hapo ningeelewa sababu akili/ nguvu/uwezo wetu unapoishia ndio Mungu anapoanza
Kwa sababu kuna mambo mengi ambayo kwetu hayawezekani ila akihusishwa Mungu yanawezekana.

Hii inatanua wigo wa kiakili kupokea na kufanikiwa hata kwa yale ambayo hata akili zetu haziyaamini.

Mfano mtu mmoja alikuwa hatua ya kufa, hadi watumishi wakaja kumpaka mafuta na kumuombea afe kwa amani, kila kipengere cha yeye kufa kilikuwa kimetimia. Lakini alipowasikia alikataa, maana bado alikuwa na malengo ya kuishi wakati hakuna kigezo cha kibonadamu kinachomruhusu aendelee kuwa hai. Kwa imani hii ya yasiyowezekana kifo chake kilihairishwa hadi sasa anadunda vizuri tu akisubiri wakati wa kifo baada ya kutekeleza kusudi ambao Mungu ameliweka ndani yake. Sio kila mtu anapokufa huwa ni mapenzi ya Mungu pengine huwa ni mapezi ya mfu bqada ya kukubari ushawishi wa waliomkatia tamaa. Na Mungu anasema wawili watatu wakikubaliana jambo yeye huwa analofanya.
 
Hili andiko ni zuri ila limekaa kidini sana kiasi likapoteza muelekeo.

Naweza kusema kua jiwekee malengo makubwa na sio yasiowezekana, Push yourself beyond the limit and you will be astonished with what you can accomplish!

anyways, KUDOS!
 
Back
Top Bottom