Hii ndio Sababu ya kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji

Fursakibao

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
6,813
Reaction score
11,540
Habari za usiku huu wadau.

Baada ya kupata taabu ya kutafuta kuku wa kienyeji wa kula, sasa nimeua rasmi nianze ufugaji mwenyewe. Nimejaribu kuangalia sokoni, utakuta kuku wa elf 17 ni mdogo sana hatoshi mwanaume wa shoka kula, hiyo inaonekana soko la kuku hawa lipo ukizingatia upatikanaji wake ni wa tabu sana.

Vifaa vyote vya kufugia ninavyo nimeviweka ndani kwa mda wa miaka kama mitatu hivi. Vifaa nilivyo navyo ni Incubator ya mayai 1056, feeder 500 na drinker 500. Kwa sasa nimeanza na kuku 8, watatu nimeshakula wamebaki 5 mbegu safi na kuna sehemu nimeweka order ya kuku 10. Nimenunua kuku wachache kwani ndio naanda mabanda.

Nitawapa mrejesho zaidi baada ya miezi 3.

1624959656724.png

sikukatishi tamaa ila nakupa somo la kuku wa kienyeji liko hivyo

Kuku wa kienyeji hutaga mayai 15 hadi 20 kwa bachi moja.

Kuku wa kienyeji hutamia/hulalia mayai hayo kwa siku zisizo pungua 21.

Na anakuwa na uwezo wa kutotoa vifaranga 7, 10, 15 au zaidi, hii idadi inategemea sababu nyingi tutazieleza wakati mwingine.

Kuku huyu hulea hivyo vifaranga kwa muda wa siku 90 yani miezi mitatu ndipo atapo anza kutaga tena.

Na ndani ya siku hizo 90 tukadirie wastani alitotoa vifaranga 13, lakini sio kweli kwamba ukimuachia kuku avilee vifaranga atavikuza vyote hapana, tuseme vifaranga vilivyo kuwa ni vinne (4) tu.

Haya sasa tujumlishe siku zote za huu mzunguko wa kupata vifaranga vinne kwenye bachi moja aliotaga kuku.

Kutaga siku 15 + Kulalia siku 21 + Kulea siku 90 Jumla zinakuwa siku 126.

Kwa hiyo siku 126 utakuwa umepata vifaranga vinne (4) tu, na kwa mwaka wenye sikumaana hiyo mwaka uwenye 360 utakuwa umefanya mizungo kama hii ya siku 126 mara tatu hivyo utakuwa na vifaranga na kuku wanaokuwa 12 tu ndani ya mwaka, HII NI HASARA #TUBADIRIKE SASA.

Sasa fahamu kwamba kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya na kupata vifaranga zaidi ya 100 kwa mwaka kutoka kwa kuku wako wa kienyeji badala ya kuku 12 kwa mwaka.

Ushauri: tufuge kibiashara
 
Lakini amesema ana incubator mkuu..
 
hv unajua mayai ya kienyeji siku ngap yana kaa na utagaji wake wa mayai uko low
Nafahamu....Kama kipindi hiki Cha baridi yanalast had 2mths ...ufugaji kuku kienyeji mie najua na kitambua ni wakula tu..sio kibiashara ..lakini kila mtu anaupeo wake..
 
Habari za usiku huu wadau.

Baada ya kupata taabu ya kutafuta kuku wa kienyeji wa kula, sasa nimeua rasmi nianze ufugaji mwenyewe.

Nimejaribu kuangalia sokoni, utakuta kuku wa elf 17 ni mdogo sana hatoshi mwanaume wa shoka kula, hiyo inaonekana soko la kuku hawa lipo ukizingatia upatikanaji wake ni wa tabu sana.

Vifaa vyote vya kufugia ninavyo nimeviweka ndani kwa mda wa miaka kama mitatu hivi.

Vifaa nilivyo navyo ni Incubator ya mayai 1056, feeder 500 na drinker 500.

Kwa sasa nimeanza na kuku 8, watatu nimeshakula wamebaki 5 mbegu safi na kuna sehemu nimeweka order ya kuku 10.

Nimenunua kuku wachache kwani ndio naanda mabanda.

Nitawapa mrejesho zaidi baada ya miezi 3.
Ama kweli ulijiandaa. Hivi gharama ya kununua incubator yenye ukubwa huo, feeders 500 na drinkers 500 ni kama shilingi ngapi na gharama ya kuku watano uliobakiwa nao ni kiasi gani?
 
Kuna sehemu nimesema hivyo vifaa nilivinunua kwa ajili ya kuku wato?

Kama umesoma kwa unakini utagundua kuwa nimesema vilikuwepo ndani.
 
hv unajua mayai ya kienyeji siku ngap yana kaa na utagaji wake wa mayai uko low
Tuseme nina kuku majike 20 wa umri sawa. Wakianza kutaga tuchukulie ratio ya 20:15 ambako kila siku napata mayai 15.

Kwa wiki nitakuwa na mayai nitakuwa na mayai 105 na kwa mwezi nitakuwa na mayai 420 nikiyaweka kwenye incubator nitaweza kupata vifaranga 300. Nikivitunza vizuri naweza kuza hadi 250.

Mpaka mda mayai yanatoka kwenye incubator tayari kuku wengine watakuwa wameanza kutaga. Hivyo utagundua nitaweza kupata kuku wengi.

Kuwa na kuku watano haimaanishi ndio uwezo au mtaji Bali najaribu kutafuta breed nzuri.
 
Ika incubator nyingi ni Vimeo .katika mayai hayo unaweza Pata vifaranha 30! Sijui huwa wanaiba au poor performance ya machine. .yaan tray moja unaambiwa wametoka kuku 5
 
Back
Top Bottom