Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji. Nawafuga kwa biashara. Naomba nitofautiane na wewe.
Kuku wangu wanataga mayai 13 hadi 16. Hata kama itatokea matetea wanaotaga ni wengi, hua nachagua matetea 15 tu kwaajili ya kulalia. Muda wa kulalia ni siku 21. Kila kuku namuwekea mayai 10 ya kulalia. Wapo wanaoa toa vifaranga vyote na wengine wanatoa mpaka vifaranga 5 au 6. Baada ya kutotoa, nawapokonya vifaranga kisha navilea mwenyewe. Siku ya 7 mpaka 10, kuku wanaanza kutaga tena.
Chukulia hao matetea 15 wanipe vifaranga 95. Changamoto za hapa na pale vitakuwa 80.
Ndani ya miezi mitatu kwa matetea 15, nina uhakika wa kupata kuku 80. Kumbuka matetea hawa wanapokuwa wamelalia, kuna matetea wengine wanakua wanataga na wengine wanakaribia kuangua vifaranga. Yaani ni kupokezana akitoka kuku huyu anaingia yule.
Kuku tunauzia mnadani. Wife anaenda mnada wa juma tano na kuku 15, mimi naenda mnada wa jumapili na kuku 15. Bei ya kuuza ni 13000 kwa 14000 ila ukija kitajiri tunakula hadi 17000.
Changamoto zipo nyingi sana na ufugaji wa kuku unahitaji uvumilivu sana na roho ya kutokata tamaa.
Ukiweza kupunguza vifo kwa vifaranga, utaufurahia sana ufugaji wa kuku. Lakini ili uanze kuona faida ya kuku wa kienyeji, unatakiwa ufuge kwa malengo. Kwa mfano. Malengo yako kwa mwaka ni kufikisha kuku 1500 hadi 2000. Jitahidi sana usiwatunze mpaka wafike 2000. Kila Wakifika 300 anza kuuza.
Kwa upande wa tiba, kuku wa kienyeji anachangamoto akiwa kifaranga. Baada ya mwezi changamoto zinaanza kupungua.