Hii ndio Sababu ya kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji

Kwahiyo vinakufa 15 out of 95??..Basi uko njema mkuu ! Kuna mikuku ilikua unaiwekea mayai 12 kinatoa kifaranga kimoja..siwehu huo! Na Kuna miez na miez ya kutotoa..mie toka corona umeanza had leo sijamwekea kuku yai tunakula tu coz Kuna baridi sana
Ufugaji wa kuku ni changamoto sana. Mwanzoni kwenye vifaranga 130, vilikufa vikabaki 20. vifaranga vilikua vinajikunyata sana, kinyesi kinaganda kwenye mnyeo, vilikua havina nguvu za miguu lakini vilikua vinadumaa sana yaani nikikuonyesha kifaranga cha miezi miwili ni kidogo sana hutaamini.

Nikaenda kuiba mbinu kwa jamaa fulani ili bachi ijayo ya vifaranga, nipunguze vifo.
Nilipopata vifaranga wengine 90, nilihakikisha vinakaa sehemu safi na vyombo vya chakula na maji ni visafi. Nikanunua chakula kwenye kampuni fulani inatengeneza chakula cha kuku. Nikanunua mifuko mitatu ya chakula cha vifaranga kuku wa nyama.

Vifaranga sikuvitoa nje, vilikaa ndani kwa siku 10 lakini siku ya saba nikavipiga chanjo ya matone. Baada ya ya siku saba tena nikawapiga tena chanjo ya matone. Nilihakikisha chakula wanachokula ni kile special tu.

Kati ya vifaranga 90, kilikufa kimoja tu. Hivi sasa nikikuonyesha kifaranga cha mwezi mmoja, hutaamini. Nasubiri vikikamilisha mwezi ndio nianze kuwapa Pumba, unga wa dagaa na mabaki ya misosi yetu.
 
Laiti ningekuwa jirani na ulipo ningeweka order ya mayai nitotoleshe
 
Lakini kuku wa Kienyeji ana kiwango cha kutaga, Kuna kuku akitaga mayai 8 anahatamia na wengine huwa wanataga wanafunga kutaga bila kuatamia.
 
Kuku ambao hawaangui mayai vizuri ni wale kuku wanaokula sana wakati wa kutoka. Unampa chakula kingi mpaka anajisahh anaanza kuacha kinyesi kwenye mayai hivyo mayai yataaribika. Kuku anaeatamia usiwe unampa chakula muache atafute mwenyewe akiwa nje akishiba atarudi kwenye kiota ila ukimpa chakula kingi atajisahau ataanza kubaki huko nje wakati mayai yanapigwa baridi
Kwahiyo vinakufa 15 out of 95??..Basi uko njema mkuu ! Kuna mikuku ilikua unaiwekea mayai 12 kinatoa kifaranga kimoja..siwehu huo! Na Kuna miez na miez ya kutotoa..mie toka corona umeanza had leo sijamwekea kuku yai tunakula tu coz Kuna baridi sana
 

Huo ni ufugaji wako na ndiyo maana ulikata tamaa na umeona usikatishe mwenzio tamaa.
We uliona wapi mfugaji mwenye lengo la kuongeza idadi ya kuku anamuachia kuku alee vifaranga kwa miezi mitatu??

Hiyo kulalia tu walio wengi kwa sasa huweka kwenye machine, so kuku anarudi haraka kwenye mzunguko wa kutaga tena na kazi ya kulea vifaranga ni ya mfugaji.
 
NDUGUZANGU NAOMBA MWENYE MBEGU NZURI YA KUKU WAKIENYEJI ANAEUZAANIAMBIE NIPO MAENEO YA TABATA
 

Ni kweli mkuu.
Lakini bado ugumu unakuja kukuza vifaranga vyote
 

Mie Siri nayoijua kuhusu vifaranga hakikisha wasikanyage chini .wasipate unyevunyev miguuni Wala ule ubaridi wa sakafu..huo ya special diet mie sijawah nunua hizo misosi..ni pumba namix na uduvi na chanjo...Basi..nawakuzia kwenye box nahakikisha box haliloi .likiloa nabadili..🤧🤧! Lakini sijawah shawishika nifuge kibiashara
 
Nina kuku wanataga qa kienyeji piwa kama unahtaji nawauza bei nzur. Namna nzur ya kufuga kuku wa kienyeji ili upate faida uwe na eneo na incubeta. Watakuwa wengi sana kwa muda mfupi
 
Wakuu mwenye kutoa huduma ya kutotolesha (incubator) makao makuu tuwasiliane, ninakusanya idadi nzuri ya mayai ya kienyeji nataka niyageuze kuwa kuku...
 
Umefanikiwa kuonyesha ugumu/changamoto kuliko suluhisho.

Ungeeeleza jinsi ya kufuga kibishara ungekuwa umesaidia zaidi.
 
Soko halikuwa tatizo ,Serengeti national park kuanzia ndabaka mpk hoteli zote za humo wanahitaji sana sana supplier wa uhakika. Nikiwa na kuku 5000 walinifata na kunipa order 20000/= kwa kila kuku wa kilo 1.5 . Kwa sasa wanatoa kuku arusha,Kilimanjaro na tarakea upande wa Kenya. Kusafirisha kuku inawagarimu wastani wa 35000/kwa kila kuku kuwasafirisha na kuwatunza . So soko lipo niliuza krbu 4500 kwa bei 20000/= unaweza kufanya hesabu hiyo. Lkn sikupata faida niliyotarajia hivyo niliachana na huo mradi. Shida kubwa sio magonjwa ,wala production shida ni gharama ya chakula. Ni kubwa sana sana hata ukilima hutaweza kulima kila hitaji,ukumbuke nilifanya mradi karibu kbsa na Serengeti hapo lamadi.
Maji ipo ya kutosha maana ni karibu na ziwa viktoria,wizi sio tatizo wasukuma wa Yale maeneo ni very honest .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye idadi ya vifaranga vinavyototlewa tatizo ni utaalam,iko hivi kuku atagapo unatakiwa ufanye date labeling kwenye kila yai. Yai halitakiwa kukaa zaidi ya wiki mbili halijalaliwa na mtetea. Ukishachambua mayai yaliyo chini ya wiki mbili angalia body structure ya mtetea,mitetea yenye miili mikubwa au manyoa huwa na uwezo mzuri wa kulalia mayai na kuyapa joto la kutosha. Hakikisha kiota hakina unyevunyevu,na uweke mchanga mlaini na si matambala Mayai yalaze kwa kufuata angle iliyochongoka iangalie chini ili yasimchome mtetea . Weka maji na chakula karibu sana na banda ili isimchukue mda mrefu kutafuta chakula.Fanya hayo na ulete mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye incubator yanatakiwa kukaa mayai yasiyozidi siku nne toka kutagwa ndo utapata matokeo mazuri
 
Kuna taarifa nyingi za upotoshaji juu ya kuku wakienyeji..kila mtu anadhani ili ulime ama ufuge kibiashara ni lazma uwe na products za muda mfupi.very wrong..pia mtu anadhani kufuga kuku wa kienyeji ni kuwatupia makombo ya ukoko wa ugali..kuna project ipo mkuranga. Imegharimu heka tatu kwa ajili ya kufugia kuku wa kienyeji...heka moja ni kwa ajili ya kupanda mbogamboga zinazotumika kama chakula cha kuku.mimi binafsi nina tendaya kuwapelekea dagaa chenga nazozifata kilwa pia kuna section ya kuzalisha mende na funza kwa ajili ya chakula cha kuku. Hawa ni pure kienyeji..ufugaji ili ukulipe wekeza mzee acha habari za kuanza na kuku watatu...masoko yapo msumbiji jimbo la pemba na Comoros.
 
Yani umeanza na kuku 8, ila watatu tayari umeshawala. Upo serious ww? [emoji28][emoji28][emoji28]
Kwa kweli huyu mfugaji ana uchu. Ndani ya Muda huo mfupi ameshakula 37.5% ya mtaji wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…