matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Kilele cha kila matukio ya sherehe za kidini ni matukio ambayo moja kwa moja au kwa kinyumenyume yanahamasisha dhambi kwa wahusika na wasiohusika.
Sikukuu za kikristo ambazo hazina baraka (endorsement) za Kristo huitimishwa na ongezeko la zinaa, matumizi ya anasa ya fedha, ulevi, ulafi, ajali, majanga duniani.na uhairishwaji wa utakatifu uliokusanywa kwa siku kadhaa.
Sikukuu za mashariki ya kati nazo zinaichukua dunia ya wahusika na wasiohusika na kuwahitimishia katika dimbwi la tamaa na anasa kama za majirani wao kiimani.
Dhambi kubwa ya Sodoma na Gomora haikuwa Ushoga na Usagaji. Hii ilikuwa ni matokeo. Dhambi kubwa ilikuwa kwa Mujibu wa nabii Ezekiel ni Ulafi na ulaji uliopitiliza. Dhambi hii hufanywa duniani kwa viwango vya juu kama sehemu ya kifurushi (package) cha shamlashamla hizo.
Yesu kwa kujua hilo, alipokufa msalabani na kufufuka tukio hilo liliambatana na kugongomelewa msalabani kwa matukio ya sherehe na sikukuu zote za kidini. Kuamini tukio hilo tu ni sherehe toshelezi ya Moyo, na ni maandalizi ya sherehe kubwa ambayo wanadamu watakaa kwenye meza ya vinono mbinguni na Mungu wao.
Waliozirudisha, na kubuni mpya baadae walifanya hayo kwa maslahi mema ya kibadamu yaliyosukumwa na ushahaulifu wa ugongomelewaji wa sherehe na shamlashamla za kidini.
Ushauri:
Jifunze kujiepusha na matukio ya kibinadamu ambayo ni mazuri kwa macho lakini ndani ya unono huo kumefichwa ndoano ya ibirisi. Kuwa mtu wa dini unayejitambua ukijua hatari zilizofichwa ndani ya ubunifu wa kibinadamu kwa uvuvio wa roho kutoka kusikojulikana.
No hayo tu.