Ndumbayeye
JF-Expert Member
- Jan 31, 2009
- 7,413
- 4,020
Boli kwanza hayo mengine baadae.Sawa, naungana na wewe kwenye hizi pongezi. Ni kweli kabisa chini ya uongozi wake, Yanga imepata mafanikio makubwa ndani ya uwanja. Mfano kuchukua ubingwa wa Ligi kuu kwa mara 2 mfululizo, kucheza fainali kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza kabisa katika historia, nk.
Ila mwisho wa siku nafikiri haya mafanikio ya timu nayo yaendane pia na uwekezaji wa miundombinu kwenye klabu.
Yanga ina miaka zaidi ya 80 tangu ilipoanzishwa! Lakini mpaka leo hii, timu haina hata uwanja tu wa kufanyia mazoezi. Kuna ule mradi wa Kigamboni! Sijui mpaka leo umeishia wapi!!
Mashabiki na wanachama wa Yanga tunatakiwa tuwaambie ukweli viongozi wetu. Mafanikio ya uwanjani pekee hayatoshi. Tunataka pia kuona timu inawekeza kwenye miundombinu.
Yanga hii ya sasa inayoimbwa kila kona ya nchi, ilishakuwepo enzi za Abbas Gulamali, na pia Yusuph Manji! Ila kwa nyakati zote hizo, iliishia tu kupata umaarufu wa uwanjani! Huku timu ikiendelea kujivunia jengo pekee la pale mitaa ya Twiga na Jangani!! Nje ya hapo, Yanga haina kitu kingine cha kujivunia!
Ni wakati muafaka huu kwa rais wa Yanga kuurejesha ule mradi wa Kigamboni kwenye utekelezaji. Na siyo kufurahia tu mafanikio ya uwanjani.
Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app