Hii ndio target yangu kabla kuacha kazi/Ajira

Kwa huu upuuzi uliouandika nakuombea kwa Mungu uajiriwe halafu ufanye hizo biashara za faida za milioni 12 kwa mwezi halafu uache Nazi...kila LA heri
[emoji23] [emoji23] wooo
 
Nilitaka kuuliza hili kwamba atapata wapi hela ya kuandaa biashara ambayo annual income iwe 25m , yaan akibahatika kupata ajira nzuri atapata 1.5m per month ambayo kwa mwaka atakua na 18m hapo bado kodi, nauli, kula, mavazi, vocha, kusaidia ndugu n.k
 
Ni rahisi kusema kuliko kutenda...wengi waliopo kwenye kazi wana mitaji mikubwa sana...changamoto ni ili uwe na biashara yenye faida lazima usimamizi ambao huwezi kuufanya ukiwa kwenye ajira....ukiingia ndio utaona hali ilivyo.
Ni ngumu kibongo bongo...ndio maana wenye uthubutu huacha kazi kuanzisha biashara
..lakini hakuna lisilowezekana chini ya jua.
 
Ukiwa na mipango mingi hivyo hitapata kazi aisee. Nina jamaa yangu ni kichwa alikwenda kwenye zile interview za wakati ule ajira za TRA wakawa applicant 50,000 kwenye ajira sijui hata elfu moja hazikufika.
Alipita michujo yote mpaka mpaka top 100 anashika nafasi ya 10 lakini ajira alikosa. Nikamwambia hapa tumepigwa hizi ajira wamepewa kwa kujuana.
Naye ana malengo makubwa sana ndo mana naona anakwama.
Hapo ndo ujue mtoto fulani wa kigogo kakaa kizezeta tu kwa vile kasoma huko Australia ndio watampa ajira sisi wa hali ya chini tuendelee kusubiri
 
Watu 50K [emoji23] [emoji23]
 
Kwahuo mtaji unaotafuta hapo kazini ndani ya miaka 7 angalia wasije wakakufunga tu kwa kesi ya kuhujumu uchumi kabla hujaacha kazi na kukuajiri, maana kwa hii mishahara ninayoifahamu kupata huo mtaji ndani ya kipindi hicho ni changamoto
 
Kwa hii mipango yako bro, sidhani kama utaacha kazi aisee [emoji23]
 
utoacha kazi kwa plan hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…