Hii ndio VPN na faida zake. Je, ina msaada wowote kwa Taifa?

Hii ndio VPN na faida zake. Je, ina msaada wowote kwa Taifa?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,530
Reaction score
3,422
VPN au VIRTUAL PRIVATE NETWORK ni teknolojia ambayo inakupa ulinzi na usalama wakati unatumia Internet hususani Public networks au mitandao ya Umma .

Kwa kifupi inazuia kuonekana utambulisho wa kifaa chako ambayo network husika imekipa au kitaalamu ni IP ADDRESS . Hivyo ni ngumu taarifa zako kujulikana au kuchuliwa au kifaa chako kama ni simu kuwa controlled/ kuendeshwa na mtu mwingine.

Matumizi ya VPN ni kama yafuatayo:-

1.Inakuwezesha kuperuzi tovuti zenye END TO END ENCRYPTION (E2EE) hata kwa kutumia public Wi-Fi , hii inamaana aina ya kutumia taarifa au ujumbe ambayo ina USIRI mkubwa kutoruhusu mtu mengine kupata hizo taarifa.

Mfano mzuri ni JAMIIFORUMS ,ukichukua Simu yako ukaunga Wi-Fi ya kazini au hotelini utaona inasumbua kufungua sababu hiyo network haiko secure na JF haiwezi kubali ingia huko ukiongeza ulinzi kwa VPN itafunguka sababu inatoa utambulisho mpya .

2.Inaficha utambulisho wako
Hapa ni sababu VPN inabadilisha utambulisho au IP address.

3.Inalinda haki yako ya kupata Usiri au privacy

4.Ukiwa na VPN itakupa Uhuru wa kutembelea Tovuti za Nchi mbali mbali hata kama kwa Nchi uliyopo zimefungiwa .

5.Itakusaidia kuondokana na Ubaguzi wa ki gharama unaponunua vitu mitandaoni /Online shopping

6.Na faida nyingine kama kuepuka kupitiliza matumizi ya bando , kudownload haraka ..nk .

Hivyo haya ndio baadhi ya Matumizi ya VPN ingawa ikitumika vibaya ni Hatari pia .​

Je ina msaada wowote kwa Taifa?
 
Kwa ufupi, vpn( virtual private network) siyo salama sana na hio haimaanishi serikali ikikutaka haitakupata.
VPN kazi yake ni kuficha IP address yako, ila tambua mtandao unaotumia wa simu mfano tigo au voda wanaweza nasa mawimbi yako ya internet ikiwa utakuwa uko Tanzania na unatumia hii mitandao ya simu katika ku access internet.

Na je utatambuaje kama haupo salama hata kama unatumia VPN, ukiona vpn yako baadhi ya muda inakwama kwama hapo tambua haupo salama, pia ukiona inachukuwa muda mrefu au sanyongine inajizima pia jua haupo salama. Baadhi ya vpn zimekuwa zikitumika kuuza data za watumiaji wao. Baadhi ni kama proton, hola, onavo, hotspot, rabbit, super, fast nakadhalika.

STAY SAFE OUT THERE.
 
Unawewesekaaa nn sasaaa
 
Watu hawatumii vpn kwa ajili ya usalama, bali kwa ajili kupeana habari...

Umekuja kutisha watu sio.?
Sio kwa ubaya ila watoa huduma wanalog maelezo ya muunganisho wako, ikiwa ni pamoja na minara iliyotumiwa, ambayo inaweza kufichua eneo lako. Refer ile scenerio ya lisu
 
VPN za bure mara nyingi hukusanya data ili kujipatia mapato, kwani zinahitaji kugharamia gharama za seva. Hii inaweza kujumuisha kuuza data zako kwa watangazaji au kushiriki na washirika wa tatu.
Ujinga mwingine! Hivi unadhani watu wanazitumia ili wajifiche au ni kwa sababu huwezi ku-access unachotaka bila kutumia VPN? Kama ni kuogopa mbona tunaweza kusajili namba zisizo na majina yetu halisi?
 
Back
Top Bottom