Nimefanya naye Kazi. Alianza na Adv. Diploma huko Mzumbe. Nafikiri alifanya Kazi Mbeya kabla ya kuja Ifakara ambako aliajiriwa kama Social Marketing Research Officer kwenye masuala ya matumizi ya neti za kuzuia mbu wa malaria. Alifanya kazi kwa juduhi kubwa na akafanikiwa kupata scholaship ya kwenda kufanya Masters chuo kikuu cha London (School of Hygiene and Tropical Medicine). Hiki chuo kinaheshimika sana kwenye masuala ya Afya na hasa magonjwa ya kitropiki. Nafikiri alimaliza Masters yake miaka ya 2004/5. Akabahatika kupata mradi wa watu wa UNICEF kwenye masuala hayo hayo ya kusambaza neti. Akatumia zile data kufanya PhD yake kwenye chuo hicho hicho za London na aliimaliza miezi michache kabla ya Kampeni za uchaguzi nchini Tanzania. Hivyo tunaweza kusema kwamba kwenye afya ameingia kama mtafiti na siyo daktari wa binadamu. Ni mchapa kazi mazuri ila kama mwanasiasa siwezi kusema maana sikuwahi hata kusikia opinion zake kuhusu masuala ya siasa!