Uchaguzi 2020 Hii ndiyo draft, sura, taswira na mipango halisi ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Hii ndiyo draft, sura, taswira na mipango halisi ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Iko hivii: kuna tetesi kuwa Bosi hataki matumizi makubwa kwenye Uchaguzi huu, hataki chama kitumie pesa nyingi kuwanadi wagombea wake wa ubunge na badala yake nguvu unaelekezwa zaidi kwe Urais ambapo kunaonekana changamoto ni kubwa kuikabili nguvu ya Tundu Lissu ambaye si kwamba ataungwa mkono na chama chake tu bali na makundi mbalimbali ya asasi za kiraia.

Kwahiyo, inasemekana kuwa Bosi anadai kwamba ikiwa katika kila jimbo Chama hakitakua na gharama za kuchangia isipokuwa Wagombea wajibebe wao wenyewe. Kama mgombea ana ukwasi wa kutosha na alishinda kura za maoni,anayo nafasi kubwa ya kupenya hata kama ana makandokando yenye ushahidi usiojitosheleza.

Kama una ushawishi halafu umepenya kura za maoni ila huwezi kumudu gharama za Uchaguzi basi tambua unaweza kuzidiwa na wapinzani wako urahisi, kwahiyo utajua uchore mchoro gani ushinde hata kama ni kwa kupita bila kupingwa.

Upinzani tegemeeni mapingamizi kibao na rafu za kila aina ilimradi tu mtu apenye Pila kupingwa. Kaeni kisaikolojia, Yaliyowapata uchaguzi wa serikali za mitaa is what is going to happen.

Alfajiri iwe njema kwenu.
 
Umeandika yale umetunga, umejitahidi kusumbua kichwa ila jaribu tena. Majembe tupo; tunawojua kusoma kati ya herufi kwanza.. 🔥🔥🔥 huo bebeni ndooo, kwa kuona 2020 inaacha historia nchini.

Magufuli 2020💯
 
Prof Koboko,

Kwa sasa hivi CCM ni mbwa mwenye njaa anatakakiwa asichague mifupa ila Mwenyekiti anafikiri hazina kuna minofu Prof Mpango ni Waziri anayejua kuzipepea korodani za mfalme
 
Umeandika.. yale umetunga.. umejitahidi kusumbua kichwa.. ila jaribu tena.. majembe tupo.. tunawojua kusoma kati ya herufi kwanza.. 🔥🔥🔥 huo bebeni ndooo.. kwa kuona 2020 inaacha historia nchini.

Magufuli 2020💯
Kuishi kwa hopes ni rahisi sana
 
Kwa sasa hivi CCM ni mbwa mwenye njaa anatakakiwa asichague mifupa ila Mwenyekiti anafikiri hazina kuna minofu Prof Mpango ni Waziri anayejua kuzipepea korodani za mfalme.
CCM haitegemei tena kutumia njia za kihalali kurudi kwenye dola. Hapa inavyoonekana ni hata afe punda lakini mzigo lazima ufike.
 
Kwahiyo, inasemekana kua bosi anadai kwamba ikiwa katika kila jimbo Chama hakitakua na gharama za kuchangia ispokua wagombea wajibebe wao wenyewe. Kama mgombea ana ukwasi wa kutosha na alishinda kura za maoni,anayo nafasi kubwa ya kupenya hata kama ana makandokando yenye ushahidi usiojitosheleza.
Nadhani hii ni kweli . Dodoma madiwani imejitokeza mkanganyiko baada ya kuwateua walioshika nafsi za pili . Barua zikatoka tena kuwa washindi wa kura za maoni ndio wapewe barua za uteuzi. Inajulikana kuwa washindi walitumia pesa na hivyo wana uwezo wa kifedha... waachwe hao hao wataweza kujiendeshea kampeni...
 
Mbwembwe ni mbwembwe tu
Wawalete wagombea wasio na madoa madoa wala halafu ya rushwa
 
Nadhani hii ni kweli . Dodoma madiwani imejitokeza mkanganyiko baada ya kuwateua walioshika nafsi za pili . Barua zikatoka tena kuwa washindi wa kura za maoni ndio wapewe barua za uteuzi. Inajulikana kuwa washindi walitumia pesa na hivyo wana uwezo wa kifedha... waachwe hao hao wataweza kujiendeshea kampeni...
Existing reality
 
Prof,Nilichogundua kwako ni zile propaganda za kishamba na hazina hata chembe ya utafiti wenye theruthi ya uhalisia

Bora ugesema, kwenye wabunge ndio wawekeze pesa nyingi zaidi za Kampeni ingawa Nako kuna kimbunga cha ushindi

Mkuu, upande wa Uraisi, uwe na uhakika wa asilimia zote kwamba, Mh Lisu anajaribu kuchangamsha genge Tu

Uwe na uhakika ifikapo saa 6 mchana wa siku ya uchaguzi, tayari Kura za Magufuli zisha tosha kumbwaga mpinzani wake, zinazobaki hata akipewa zote haitasaidia
 
Back
Top Bottom