~!~ Hii ndiyo Katiba ya CCJ ~!~

Luga hii ya "Kwa Kuwa" kama za Bungeni Vile. Hii inathibitisha kuwa ni mpasuko wa CCM.
 
jamii iliyokata tamaa siku zote huishi kwa kutegemea "masiha" atatokea
wakati wowote. hivyo yeyote yule atakaejitokeza na kudai "umasiha"
hakika atapata wafuasi. ndio maana tunashuhudia leo hii watu ambao
imani zao zinasema waziwazi kwamba hakuna ajuaye siku ya mwisho bado
baadhi yao huamini atokeapo "mwanamiujiza" na kutangaza siku, tarehe
na mwaka wa siku ya mwisho!

jee ccj ni "masiha" wa kweli au la?
 
natatizika tena saana

MATATIZO YA TANZANIA YATASULUISHWA KWA UTITIRI WA VYAMA?????? NAONA kama vyama vya siasa ni vimiradi tu vya wajanja wachache i hate politics + politicians
 
2015 ni mbali, tulitegemea mabadiliko yangetokea 2010, ili tuisukumenchi kungali mapema
 



mbona kwa kuwa nyingi sana?
 
inasikitisha kuona hata wataalamu tulio wategemea wakwamue nchi wanaenda kupiga domo la uwongo kwenye majukwaa ya siasa.
 
Suhala la kujiuliza... "kwa nini kianzishwe miezi michache kabla ya uchaguzi?

Sidhani kama hili ni tatizo!

Wapenda demokrasia wamepigania suala la mgombea binafsi lakini 'wenye nchi' wanaogopa/hawataki. Kulikuwa na dalili ya suala la mgombea binafsi kufanikiwa (rejea maamuzi ya mahakama kuu), lakini mahakama ya rufani and serikali hawana nia ya kulipatia ufumbuzi swala hili katika muda muafaka. Sasa hivi nona wameanza kufikiria referendum kwenye suala la mgombea binafsi!

Kwa mtu (ama watu) aliyekuwa na dhamira ya kusimama kama mgombea binafsi, simshangai kama sasa ataamua kuanzisha chama kuelekea uchaguzi mkuu kwa sababu uwezekano wa mgombea binafsi kwa mwaka 2010 ni almost NIL.
 
Wabunge na wanasiasa wanakiogopa sana CCJ...wanakikana kuogopa kivuli chake au unafiki??wanataka kuona kama kitu fulani hakitatokea wanahama...kama JK alivyoweka mtego wako Chadema!!
 
Swali kubwa ni je CCJ kitakuwa mkombozi wa watanzinia wanyonge?
 
UONGOZI
  1. Sifa za kiongozi:
      1. Awe na sifa zote za mwanachama kama zilivyoainishwa kwenye Katiba hii.
      2. Awe ana rekodi ya kutetea na kueneza Katiba na sera za Chama.
      3. Awe mchapakazi na mwenye uwezo wa kuongoza.
      4. Awe mkweli, mwaminifu, mwadilifu na mnyenyekevu kwa wananchi wenzake kwa kauli na vitendo, mtetezi na mpenda haki asiye na historia ya ufisadi au uhalifu wa aina yoyote ile.
      5. Awe na upeo mpana kiakili na kuwa tayari kujiendeleza yeye binafsi kielimu na kutumia elimu aliyoipata kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.
      6. Awe na moyo na uwezo wa kufanya kazi na makundi mbali mbali ya jamii katika mazingira mbali mbali.
      7. Awe mtu aliye mstari wa mbele katika kujua matatizo ya jamii na kuyatafutia ufumbuzi.
      8. Awe ni mzalendo na mwenye uchungu na nchi yake na awe na ushujaa na ushupavu wa kutetea masuala ya msingi yanayogusa maslahi ya Taifa.

      1. Asiwe mtu mwenye tamaa na rekodi ya ukigeugeu katika siasa.
      2. Awe na rekodi ya nidhamu ya kuheshimu vikao, viongozi na wanachama wenzake.
....sifa za kiongozi......naona na huku VIHIYO wanaruhusiwa kugombea.....sioni namna nzuri ya kumpima mtu kwa point namba 5!
 
NL,

thats too General, Hawaruhusu Vihiyo bana!

UONGOZI ni tathnia pana, na huwezi kuweka vigezo vya kumpima mtu hapo kwenye no5, maana viongozi wapo wa cadres nyingi mno ndani ya chama!

Mind you, uongozi unaanzia kwenye shina hadi taifani, so huwezi kuweka vipimo 'precise' vya viongozi, hii itategemeana na ngazi, ambapo hiyo itakuwa stipulated katika miongozo mingine, nje ya katiba!!

Lets be patient brodas, ...masihi amewasili nchini!
 
Hapa Hakuna kitu kipya zaidi yale yale ya siku zote na wakati ukifika ndio tutaona matokeao yake. Kwanini wasijiunge na vyama vilivyopo??? hapa ndio kuna tatizo kubwaa
 
Hapa Hakuna kitu kipya zaidi yale yale ya siku zote na wakati ukifika ndio tutaona matokeao yake. Kwanini wasijiunge na vyama vilivyopo??? hapa ndio kuna tatizo kubwaa

Labda wameona kuwa vyama vilivyopo vina ubabaishaji/usanii mwingi so wameamua kuja na kitu kipya kukidhi mahitaji yao ya kidemokrasia(Hasa ukizingatia kwamba wanayo haki ya kuanzisha na kujiunga na chama chochote mradi tu wafuate sheria za nchi)
 
Labda wameona kuwa vyama vilivyopo vina ubabaishaji/usanii mwingi so wameamua kuja na kitu kipya kukidhi mahitaji yao ya kidemokrasia(Hasa ukizingatia kwamba wanayo haki ya kuanzisha na kujiunga na chama chochote mradi tu wafuate sheria za nchi)
Hakuna kitu kipya hapa. Hapa Tanzania kuna utitiri wa vyama hii yote ni janja ya CCM ili kuwagawa watu na kuona hata kama kuanzisha chama kingine ila CCM watafanya ili kushinda na kusema kuwa JK ni Kiboko. Mimi naona ni bora kuingia kwa vyama hivi vilivyopo na kuwapa nguvu zao. Tanzania kuna kama vyama 20 hivi kwa sasa na pia hii ni mbaya sana kwa Taifa kama tanzania. Sijapendezwa na hali ya mambo ya divide na rule kama hivi
 
Mimi sijaona mantiki ya kuanzisha vyama kibao kama ilivyo sasa hivi. ila sijaona kuwa itakuwa tishio kwa CCM maana wanaweza kutumia instruments apparatus maana wanaweza kuwaweza kwa ndani na pia mfumo wa siasa zetu bila ya mizizi ndani ni mbaya sana
 

Hapana kiongozi,unaionea CCM hapa..kwa nini kila kitu CCM inaangushiwa lawama mkuu?,sidhani kama CCM watakuwa na akili mbovu kiasi hichi ya kuanzisha CCJ ili wawagawe watu ili washinde..Kwangu mimi mchawi wa upinzani yuko nadhani ya upinzani wenyewe maana wao ndo hufanya hila ya kugawa kura(kuwagawa wananchi) kwa kila chama kumsimamisha mgombea wake...So unakuwa hauitendei haki CCM kwa kuibebesha lawama hizi mkuu..Upinzani hauna ushirikiano hata kidogo aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…