May be if we give them time, unless otherwise, at least kwa sasa, nothing new news can be observed from CCJ vs CCM, rather than a pure hoax.
Watu wachache wamekaa, wakafikiria namna gani wataweza kuweka pressure ili interests ambazo wamekuwa wakizipigania mara kwa mara zinapata nafsi ya kufanyiwa kazi, wakaamua 'kubuni kamradi' ambako katawatisha watu wa CCM na System kwa ujumla, wakaunda CCJ.
Wakiwa na uhakika kuwa wale wote wasiotaka kuona CCM ikifa na hasa wale wanaotaka kuonekana wako 'neutral' katika mijadala ya vita dhidi ya 'mafisadi' (siyo ufisadi) wa-take into account complaints za waundaji wa CCJ, wakiogopa kuwa wasipofanya hivyo jamaa wanaweza kufanya jambo fulani...
Kwa nini wamesubiri miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu?Ili hali wakijua kabisa kuwa kupata registration is a little bit long process, hasa kwa nchi kama Tanzania ambapo demokrasia bado inaendeshwa kwa mazingira ya chama kimoja.
Ninafikiri 'HUENDA' kwa sababu katika kutafuta umaarufu wa kisiasa kila kitu kinawezekana jamaa wanataka ku-gain fame kwa kutumia appealing to people's simparthy, kwamba iwapo watachelewa kupata usajili wa kudumu, watalalamika kwa wananchi kuwa CCM imewahujumu ili wasishiriki uchaguzi kwa kuwa kinawaogopa. One can guess what would be next...
Vinginevyo kwa nini basi hawakufanya jambo hilo mapema? Ili wajiandae, tuwajue kwa undani, wananchi wafanye maamuzi sahihi. Kwa nini wanataka kuwavamia wapiga kura kwa staili hiyo ya kuwatanguliza vibaraka kuandikisha chama na kukipatia promo kubwa kama ilivyo sasa?
I dont believe in anyone, kati ya hao ambao mpaka sasa wanatajwa kuwa wako nyuma ya hii kitu. Wengine walikuwa ni wanamtandao wa Kikwete, walichofanya kwa nchi hii na baadhi ya watu mwaka 2005 wakati wa kampeni kinajulikana. Hawajawahi kutubu mahala popote, wamebadilika lini?
Ulkiangalia kwa undani malumbano yanayosemwa yako ndani ya CCM ambayo yanaweza kuwa msukumo wa kuundwa CCJ ni kuhusu interests zao, siyo za wananchi haswa, wako wachache mno wanosukumwa na matatizo ya watu. Wangelikuwa wako wengi wangeshafanya kitu hiki tangu siku nyingi ili watu tuwaunge mkono. Otherwise, wanakuja kwa staili ile ya MTANDAO mwaka 2005. Ogopa Chui aliyejivika ngozi ya Kondoo...