~!~ Hii ndiyo Katiba ya CCJ ~!~

Chama cha siasa ni vitu vitatu: Katiba, Uongozi na wanachama. Hivyo vitu viwili vya mwisho, na hasa hicho cha tatu, kwa nini vinafichwa?

Tatizo ninaloliona ni tabia yetu watanzania kupenda vitu vipya na kuingia kwenye mkenge wa kipya kinyemi.

But it's always good to be hopeful, maybe a messiah is coming, though I am very skeptical!!
 

Heshima mbele Mkumbo!

How do you expect chama kiwe katika process ya kujisajili, halafu kiwe na wanachama overnight?

Jamani, why too suspicious on this messiah?

Mi ningekuelewa kama ungehoji no 2, ambapo ni uongozi, kama ulivyodefine mwenyewe:, ambapo pia duru zinasemakuwa watajulikana very soon.

Patience- i insist!
 
Utakuja kuona kuwa siku zinavyokuja na ndipo utajua nini ambacho nafanya. Sasa hawa jamaa kwanini wasiingie kwenye vyama hivi?? Hapa ndipo kwenye tatizo la msingi sana.
 
Utakuja kuona kuwa siku zinavyokuja na ndipo utajua nini ambacho nafanya. Sasa hawa jamaa kwanini wasiingie kwenye vyama hivi?? Hapa ndipo kwenye tatizo la msingi sana.

Wataingiaje wakati vyama vyenyewe vilivyopo vimejaa ubabaishaji kila kona...Ufisadi,ukosefu wa demokrasia,ubinafsi,wasio na pesa kukosa nafasi(wenye pesa ndo wana nafasi kwenye vyama sasa)...So ni bora kuja na kitu kipya badala ya kung'ang'ania hivyo vyama unavyosema vilivyopo ambavyo havija jipya lolote lile....Wapeni CCJ nafasi,msiwakatishe tamaa mapema hivi....
 
The only condition nilisikia kupata wanachama kutoka mikoa mbarimbari kitu ambacho waasisi wamesema sio issue.
Wangekisajiri toka last year zengwe la chama tawala lingeshaanza kuwatafuna.
Imagine chama ndo kwanza kimeanzishwa tayari usalama washaanza kuhoji watu,sijui democrasia ya wapi hii
 
May be if we give them time, unless otherwise, at least kwa sasa, nothing new news can be observed from CCJ vs CCM, rather than a pure hoax.

Watu wachache wamekaa, wakafikiria namna gani wataweza kuweka pressure ili interests ambazo wamekuwa wakizipigania mara kwa mara zinapata nafsi ya kufanyiwa kazi, wakaamua 'kubuni kamradi' ambako katawatisha watu wa CCM na System kwa ujumla, wakaunda CCJ.

Wakiwa na uhakika kuwa wale wote wasiotaka kuona CCM ikifa na hasa wale wanaotaka kuonekana wako 'neutral' katika mijadala ya vita dhidi ya 'mafisadi' (siyo ufisadi) wa-take into account complaints za waundaji wa CCJ, wakiogopa kuwa wasipofanya hivyo jamaa wanaweza kufanya jambo fulani...

Kwa nini wamesubiri miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu?Ili hali wakijua kabisa kuwa kupata registration is a little bit long process, hasa kwa nchi kama Tanzania ambapo demokrasia bado inaendeshwa kwa mazingira ya chama kimoja.

Ninafikiri 'HUENDA' kwa sababu katika kutafuta umaarufu wa kisiasa kila kitu kinawezekana jamaa wanataka ku-gain fame kwa kutumia appealing to people's simparthy, kwamba iwapo watachelewa kupata usajili wa kudumu, watalalamika kwa wananchi kuwa CCM imewahujumu ili wasishiriki uchaguzi kwa kuwa kinawaogopa. One can guess what would be next...

Vinginevyo kwa nini basi hawakufanya jambo hilo mapema? Ili wajiandae, tuwajue kwa undani, wananchi wafanye maamuzi sahihi. Kwa nini wanataka kuwavamia wapiga kura kwa staili hiyo ya kuwatanguliza vibaraka kuandikisha chama na kukipatia promo kubwa kama ilivyo sasa?

I dont believe in anyone, kati ya hao ambao mpaka sasa wanatajwa kuwa wako nyuma ya hii kitu. Wengine walikuwa ni wanamtandao wa Kikwete, walichofanya kwa nchi hii na baadhi ya watu mwaka 2005 wakati wa kampeni kinajulikana. Hawajawahi kutubu mahala popote, wamebadilika lini?

Ulkiangalia kwa undani malumbano yanayosemwa yako ndani ya CCM ambayo yanaweza kuwa msukumo wa kuundwa CCJ ni kuhusu interests zao, siyo za wananchi haswa, wako wachache mno wanosukumwa na matatizo ya watu. Wangelikuwa wako wengi wangeshafanya kitu hiki tangu siku nyingi ili watu tuwaunge mkono. Otherwise, wanakuja kwa staili ile ya MTANDAO mwaka 2005. Ogopa Chui aliyejivika ngozi ya Kondoo...
 
Kama kimeshasajiliwa si lazima kuna viongozi japo wa muda waliotajwa kwenye process za usajili. Au niulize kiivi, nani amefanya taratibu za kukisajili?
 
Huwezi kuona kuwa hii ni janja ya kutaka kuwatenganisha Watanzania?

Give me a break! Watanzania walishatenganishwa already kati ya mafisadi walionacho na wananchi wasionacho it can't be done twice.
 


Mkumbo kupenda kipya si mbaya sababu hakuna chama ambacho hakijawahi kupitia upya. hATA CHADEMA HUKO NYUMA KILIKUWA KIPYA
 

Chama cha Jamii?????????????
chama cha Mapinduzi ????????
Tuwe macho this could be Chama cha Jakaya. Kuwapumbaza watz
 
Shukran Mwanakijiji,

Katiba nzuri, je unaweza kutupatia lineup ya uongozi wa muda wa CCJ?
CCM 'B'????????
Kuhusu uongozi na wanachama watarajiwa mbona wanajulikana? soma alama za nyakati wala hautopata shida. I WISH THEM LUCK
 
Mwanakijiji.
Nahisi kama unahisa na chama hiki.Umepata wapi Katiba yao mapema Hivyo?
 
CCM 'B'????????
Kuhusu uongozi na wanachama watarajiwa mbona wanajulikana? soma alama za nyakati wala hautopata shida. I WISH THEM LUCK

Sio wote wenye utaalamu wa kusoma alama kama wewe mkuu. Katika hili tufahamishe tu kama una majina yao!
 
Hawa waungane na CHADEMA na CUF,hapo mziki utaeleweka but hili suala lakuibuka tu na chamabila mtandao wa kutosha ni yale yale ya COPE south Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…