Hii ndiyo kauli ya msomi na waziri wa elimu Tanzania juu ya matokeo form four

Hii ndiyo kauli ya msomi na waziri wa elimu Tanzania juu ya matokeo form four

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
821
Reaction score
335
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk. Kawambwa.

Mwisho wa kunukuu

Hapo ndiyo amesikitika mpaka basi, na wala hausiki wa hali iliyotokea. Upo uwezekano wakati anatoa kauli hiyo watu walipiga makofi sana tu.Bado tutaliwa kweli kweli.
 
Nijuavyo mimi Watanzania siyo watu wa kuuliza "WHY?....Tu watu wa kuhubiriwa na kushabikia basi,....na baada ya hapo tunabaki wanung'unikaji tu!...
Huyu jamaa ingekua nchi za wenzetu alikuwa anaachia ngazi instantly
 
Akili iliyosababisha tatizo akili hiyo hiyo haiwezi kulitatua tatizo ililosababisha
 
Mbona hatuwahusishi waliofanya mitihani? Yaani lawana kwa mtu ambae hajafanya mitihani ! Wanafunzi wanahusika kwa haya matokeo kwa asilimia kubwa ikifatiwa na wazazi mwisho kabisa ni serikali
Siku wakifaulu sana mtasema serikali imewapitisha wakifeli pia serikali imesababisha hebu tuweni binadamu
 
Huyu naye anatakiwa kujiuzuru ameshindwa kazi!
 
tunasubiri mtaala utoke ndio tuanze kufanya vzr katika mitihani
 
wanafunzi waliofeli wanawalaumu walimu wao,walimu wanailaumu serikali kwa kutojali maslahi yao, wazazi wanailaumu serikali dhaifu ya kikwete na bunge lake. hapa cha msingi na kuboresha maslahi ya walimu kwanza kabla hata ya yote.
 
hahaha yani huyo ukimuuliza uliza atakuambia kwani mimi ndo nimefanya mtiani? uajibikaji tanzania bado sana, ingekuwa kenya wazazi weshamfuata nyumbani na fimbo kumlazimisha aachie ngazi... lowasa kaanzisha project yake ya shule za Kata Dhaifu wenu akitaka aje apatie umaarufu hapo akamtengenezea Jungu... kaficha proposal yakhe sasa wata desa wapi..ELIMU KWANZA KILIMO BAADAE..
 
Mbona hatuwahusishi waliofanya mitihani? Yaani lawana kwa mtu ambae hajafanya mitihani ! Wanafunzi wanahusika kwa haya matokeo kwa asilimia kubwa ikifatiwa na wazazi mwisho kabisa ni serikali
Siku wakifaulu sana mtasema serikali imewapitisha wakifeli pia serikali imesababisha hebu tuweni binadamu

kweli kabisa
 
Akili iliyosababisha tatizo akili hiyo hiyo haiwezi kulitatua tatizo ililosababisha

Ni kweli kabisa ndugu yangu, hawa watu tunaowaita viongozi sijui watawala wetu hawana nia ya dhati ya kuboresha sekta ya elimu ya nchi hii, NI BOGUS KABISA!
Laiti kama wangelikuwa nayo wasingekurupuka kuanzisha utitiroi wa shule za kata wakati wanajua fika hawana uwezo wa kuzifanya ziwe shule kweli....NA MATOKEO YA AKILI ZAO FUPI NDIO HAYA!
TUNAWANG'ANG'ANIA WA NINI LAKINI?
 
Tatizo kubwa ni wanafunzi wenyewe unasubiri utafuniwe cc tulikuwa tunapambana wenyewe kusoma, wakat wao facebook na jamii forum masaan 24,headphone masikion muda wote wanawaza mapenzi wakati wote unategemea nn! thamani ya elimu itarudi kule kule tulipotoka shule nzima anafaulu mmoja tu
 
Back
Top Bottom