Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
Salamu mbele!
Kumekuwa na malalamiko mengi sana ya chini chini na ya wazi kwa muda mrefu ya jinsi clouds media ambavyo wamekuwa wakiwanyonya na kuwaburuza wasanii wa muziki nchini Tanzania.
Wengi waliojaribu kujinasua na unyonyaji huo ama kwa kuongea hadharani na kukemea na kupinga dhuluma hii ya clouds media walikumbwa na mkono wa chuma wa Ruge na clouds media. Wengi walishindwa kustahimili mkono wa chuma na kupotea kwenye gemu na wengine waliishia kurudi kuomba radhi.
Utajiuliza jinsi msanii kama Ruby kwa kipaji chake alishindwaje kuhimili mkono wa chuma wa clouds media?
Figisu na kuwekewa kauzibe ni kawaida sana pale penye riziki kuna watu huwa wanasema sijui media zimekuwa nyingi kwa hiyo siyo rahisi kuwekewa kauzibe au figisu na clouds media sasa siyo clouds media tu hata EATV au EFM wanaweza kukuwekea figisu na ukashindwa kutoboa.
Nilimsikia msanii Otile Brown akieleza jinsi media za Kenya zinavyojaribu kumuwekea kauzibe na figisu ili kumshusha. Naongea haya ili kuthibitisha kuwa figisu na kauzibe bado vipo sana tu kwenye sana yetu and they are here to stay.
Hebu tazama Diamond Platnumz alichofanyiwa na clouds media na EATV vipi?
Zipo mbinu mbili muhimu ambazo zinaweza kumsaidia msanii kushinda dhidi ya figisu na kauzibe kutoka kwa media za ndani.
1. Wasanii wajaribu kuwekeza kwa nguvu zote kwenye social media, social media inanguvu sana kuliko kitu chochote na kila siku itazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi. Social media kama Instagram, Jf, WhatsApp, twitter, Facebook telegram na muhimu zaidi YouTube ni njia muhimu zaidi za kuwafikia mashabiki wakati wowote hakunaga mhariri wala mkurugenzi wa vipindi huko.
Wasanii ambao siyo watumiaji wazuri wa mitandao kama Rich Mavoko ni wakati sahihi sasa wa kuajiri team ya vijana wa kuwasaidia ili wawe active mtandaoni.
Ni mbaya sana kwa msanii active kupita wiki mbili hujapost Instagram wala Facebook wala twitter watu wakikusahau utasema umeibiwa nyota? Ujio wa mitandao ya kijamii umepunguza kwa kiasi kikubwa watazamaji na wasikilizaji wa redio na tv, wengi hawaoni haja ya kwenda kusikiliza redio asikie kilekile alichokiona YouTube au jf au Instagram. Hivyo msanii mwenye base na team nzuri kwenye mitandao ya kijamii hawezi kushushwa eti kwa media kushindwa kuplay Nyimbo zake. Hamissa Mobetto na ngoma yake ya madam hero ni mfano mzuri wa watu ambao mitandao imewasaidia, wimbo wa madam hero haujapigwa na redio yoyote lakini kupitia timu yake ya mtandaoni amepata viewers karibia laki nne YouTube na hiyo ni audio tu, wakati kuna video YouTube hazijafikisha hata nusu ya viewers hao.
2. Njia ya mwisho kwa wanamuziki waliotoka na kufanya vizuri hakikisheni mnatoka na kufahamika nje ya Tanzania kwa kujizolea mashabiki wa kutosha nje ya Tanzania. Hii inawezekana kwa kuwashirikisha wasanii wa nje ya Tanzania mfano wasanii kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Nigeria na South Africa. Msanii ukiwa na base kubwa ya mashabiki nje ya nchi ni ngumu sana kushushwa na hii siyo na media tu huwezi kushushwa na mtu yeyote isipokuwa Mungu. Mtu kama Diamond Platnumz anaweza akahamia nchini Kenya au Nigeria na bado akaendelea na muziki wake.
Wasanii kama akina Lady Jaydee, AY ni vigumu kuwashusha Lady Jaydee Clouds wamejaribu wameshindwa. Ni rahisi media za bongo kumdhibiti Mwanafa kuliko kumdhibiti AY.
Naona wasanii kama Rayvanny, Harmonize, lavalava na mbosso wanafanya hivyo, wamekuwa na tour na collabo katika nchi nyingine zaidi Kenya.
Wakatabahu!
Sent using Jamii Forums mobile app