Quemu
JF-Expert Member
- Jun 27, 2007
- 984
- 133
Kuna documentary moja naiandaa ambayo inahitaji video production.
Sasa basi, niliwasiliana na kampuni maarufu za video production nne (sitozitaja) hapa nchini katika ku-shop moja ambayo itaifanya hiyo kazi kwa ufanisi. Tatu kati ya hizo zinamilikiwa na wabongo wenzetu. Moja na Mkenya.
Mkurugenzi wa kampuni moja ya mbongo hakunipa nafasi hata ya kumtembelea ofisini kwake. Kwani kila nikiwasiliana naye kwenye simu ananiambia yupo bize kichizi, na kwamba atanitafuta atakapopata nafasi. Ieleweke kuwa toka nilipompigia simu ya kwanza kabisa, nilimweleza sababu ya kwa nini nahitaji kuonana naye.
Nilipotembelea kampuni nyingine ya mbongo nilimkuta mkurugenzi amesafiri. Basi nikaongea na mhusika mwingine muhimu hapo na kumwelezea kilichonipeleka pale. Akanielewa vizuri na kuahidi kuwa pindi mkurugenzi atakaporudi (alikuwa arudi siku 3 baadaye) atamwelezea. Na kwamba mkurugenzi atani-contact ili tuonane. Wiki ikapita. Nikamwendea hewani yule mhusika, akanieleza kuwa alimwelezea mkurugenzi pindi aliporudi tu, mkurugenzi akaahidi kunitafuta. Basi nikasubiri siku kama 2 hivi, nikaibuka pale ofisini kwao tena. Stori niliyoipata hapo ikaniacha hoi .eti mkurugenzi amesafiri tena, amekwenda nje ya nchi kwa kama wiki 3 hivi, na kwamba hajaacha maagizo yoyote kuhusu kazi ambayo nimewapelekea. Nikagwaya!
Kampuni ya 3 ya mbongo, nilifanikiwa kumwona mkurugenzi baada ya kujaribu kama mara 3 hivi. Tukaongea naye na akaniambia atajibu siku inayofuatia. Wiki imepita sijasikia chochote kutoka kwake.
Pia, nilikwenda kwenye kampuni ambaye mkurugenzi wake ni mkenya. Kwanza attention aliyonipa huyo jamaa ilinitia moyo sana. Nilipokuwa namwelezea program yangu, jamaa alikuwa anathubutu mpaka kuchangia ideas zake (wabongo hawakufanya hivyo) ni vipi kampuni yake inavyoweza ku-shoot hii documentary kwa ufanisi wa hali ya juu. Jamaa akahidi kukutana na timu yake kesho yake, halafu tungeonana naye keshokutwa yake kwa majadiliano zaidi. Kesho yake asubuhi na mapema, mshikaji akanitumia sms kuniambia kuwa amepitia tena maelezo niliyompatia na kwamba amepata ideas nyingine mzuri za kuongezea. Na pia hakanihakikishia kuwa vifaa na uwezo wa ku-produce program yangu anavyo vya kutosha. Hakuishia hapo ! jioni yake akanipigia simu na kuniambia kuwa ameshajadili na timu yake, na kwamba tuonane siku inayofuatia saa 5 asubuhi kwa mazungumzo zaidi. Kwenye appointment yetu ya siku iliyofuatia, sio tu alizidi kunihakikishia kuwa anaweza kazi, bali pia alinionesha baadhi ya documentary walizowahi ku-shoot, na akaenda mbali zaidi kwa kunionesha vifaa vyote vya production alivyonavyo.
Chagua langu likawa rahisi !!!!
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wabongo wenzangu !
Mchawi wetu ni nani Wakenya au Sisi wenyewe?
Yaani mtu unapeleka kazi kwenye haya makampuni, lakini wao wanataka uwafukuzie kana kwamba unaenda kuomba kazi au msaada ! Kha gademu!!