GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Akitiririka na kuserereka na Kituo cha Redio cha Efm asubuhi hii mmoja wa Wadau muhimu wa Yanga SC, Mwanachama wa Yanga SC na Mdhamini pia ( japo huwa hapendi Kujulikana ) Mbunge wa Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na kuchukizwa na Kitendo cha ' Kipuuzi ' kilichofanya na ambacho kinaendelea kufanya na baadhi ya Wanayanga kutaka kushindana na Maamuzi ya BMT na TFF yanayowataka wao Kufanya Uchaguzi upesi.
" Timu inaenda na inaendeshwa kwa shida halafu anatokea Mtu anawaambieni fanyeni Mkutano ili mkae sawa nyie mnaanza Kubishana nao na kutaka kuleta mzozo mwingine wa Kipuuzi na usio na maana hasa kwa mpira wetu huu ", alisema Ridhiwani.
Hakuishia tu hapo Mbunge huyu ambaye huwa hafichi kabisa mahaba yake niue kwa Klabu yake ya Yanga SC hakutaka kutoonyesha ile inayoitwa ' Spirit of Sportsmanship ' pale ambapo aliipongeza pia Klabu ya Simba SC kwa Kufanya Uchaguzi wake hivi majuzi na kuingia rasmi katika mfumo wa mabadiliko ambao amesema ndiyo unatakiwa uigwe na Timu nyingi na hasa Wao ( Yanga SC )
" Angalia wenzetu Simba SC juzi wamechaguana na sasa wameshaanza kuelekea katika mafanikio na watafika mbali lakini cha Kushangaza huku Kwetu Yanga SC Watu badala ya kuwa na mawazo ya Kimaendeleo wao wamewekeza tu katika Majungu na kutaka Kutengeneza Makundi ndani ya Klabu huku wakitaka kutusababishia matatizo ya Wasimamizi wa mpira wa nchi hii Serikali kupitia BMT na TFF yenyewe ".
Haya Wana Yanga SC mmemsikia Ridhiwani Kikwete?
Kazi Kwenu ila Simba SC kwa sasa tunawaza Kushindana na akina TP Mazembe, Kaizer Chiefs, Al Hahly, Enyimba FC na kidooooooooooooogo sana Azam FC kwa hapa nchini Kwetu Tanzania na tuna mpango miaka mitatu ijayo Simba SC ifanane na Timu kama Liverpool FC, FC Barcelona na Paris Saint Germain hasa Kiutajiri na Kimaendeleo.
Nawasilisha.