Hii ndiyo tofauti kubwa kati ya Ali Kiba na Diamond

Hii ndiyo tofauti kubwa kati ya Ali Kiba na Diamond

Dogo G

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,052
Reaction score
440
Waungwana habari zenu naamini mko swalama salimini,leo nimeamua kuuleta ukweli juu ya masuperstaa wakubwa hapa bongo yaani wasanii wenye nafasi zao kubwa katika ladha ya bongo(bongoflavour) na wasanii wenyewe ni huyu DIamond wa tandale from kigoma na Ali salehe kiba wakiwa wote from kigoma mkoa.Huwa kunakuwa na mitazamo mingi sana ya kiushabiki inayotolewa na wadau mbalimbali wakilenga kuwatofautisha hawa wasanii lakini waandishi wengi wanajikita katika ile nani anapendezwa naye.

Kwanza,kiukweli mimi ninaamini diamond ameufikisha muziki wa bongo mbali sana na kutangaza taifa letu na hivyo utakuwa humtendei haki ukikubali uwezo wake na hata kuweza kumtunuku ufalme wa mziki wa bongo(mafanikio) ukitofautisha na braza alikiba.

Unapozungumzia wasanii hawa ili kupata sifa zao kirahisi ni sawa na kuwafananisha na wachezaji,RONALDO cr7 na MESSI,Alikiba ana uweza muziki nikimaanisha muziki ni kutoka ndani ya damu kabisa na hata ukifatilia kipindi anaanza enzi hizo alikuwa anafanya muziki kama hobby tuu alimradi asizike kipaji,alikiba amekulia kwenye maisha ya kidini kidogo na hivyo kumfanya kuwa na hofu kidogo kimwenendo chunguza hata jinsi the way anaishi,jamaa sio mtu wa kiki nyingi sana wala skendo za kumwaga radhi hata watu wote wakajua,jamaa hata uvaaji wake hapa wote mtaamini huwa anavaa kimaadili kidogo kiasi kwamba kama humfahamu ukioneshwa kuwa ni msanii huwezi kuamini,jamaa havai mahereni mara kuvaa misalaba mara kuweka vipini puani mara kupaka marangi kichwani au mdomoni so inshu zima ni upande wa maadili zaidi yaani ile hofu ya kujiharibia haiba kwa watu ndio kitu alichonacho huyu jamaa,ndio maana kuna muda anaonekana mbinafsi kisa hapendi mikiki na miskendo ya kujichafua.

Lakini diamond platnumz,jamaa ana kipaji cha ajabu sana,ana mziki mzuri sana ila yeye kajikita katika muziki biashara kiasi kwamba hata iweje hawezikufaya show ya watu kumi hata iweje na inaonesha yeye mziki ulikuja baada ya zile harakati za kujitatua na hali ngumu ya maisha kule tandale enzi zile,lakini diamond hana haiba nzuri kabisa hebu angalia skendo zake sometimes ni kujitakia tuu kutaka kila kitu kiwe ni sehemu ya kujiongezea habari au umaarufu(kiki) mitaani,Jamaa kakosa kitu muhimu kimoja tuu ile haiba binafsi maana utamuona na mahereni,mikufu mingi,mara majeans yamechanika mapajani,mara rangi midomoni na kwenye nywele tena afadhali kwenye nywele shortly jamaa yupo nje ya kimaadili,kwani ukiwa msanii lazma uvae mlegezo?,vipi PROFESSA J,NIKK WA PILI,JAY Z huko mambele mbona wako humble tu.

Kuna muda huwa nawaza labda pengine ni haya masuala ya malezi kwa kuwa jamaa kalelewa na mzazi mmoja cha kwanza,na ukizingatia mama aliyemlea nae ndio hivyo MIRUKO na usikute ndio sababu ya baba diamond kupita kushoto(wanaume wanajitambua ukiona kamwaga mwanamke kuna tatizo katika akili ya huyo mwanamke)tofauti na kiba ambaye kalelewa na wazazi wote wawili.Lakini yote katika yote ni vema mtu ukiwa na nafasi kubwa kama mfano katikajamii,jamii ikikuheshimu basi huna budi kujiheshimu.Kwahiyo diamond kaka jiheshimu unao muda wa kubadilika licha ya yote.all in all mimi ni miongoni mwa tunaopenda muziki wa diamond na lengo la uzi kubadilshana.

Ahsante,
FB_IMG_15309849550805806.jpg
FB_IMG_15310126561697792.jpg
 
Nothing lasts forever, wapi kina Olufela Olusegun Oludotun Ransome-Kuti ( Fela Anikulapo Kuti)?
Wapi kina Luambo Makiadi Franco?
Mwisho wetu u karibu kuliko mwanzo wetu.
Tubadilike, maisha Bila ya Yesu KRISTO ni ubatili mtupu.
Ni wakati sasa wa kutubu, kuokoka na kuiamini injili.
 
Endelea kushuhudia hadi JF wote waokoke
 
Ha ha....ni mtazamo wako ila sidhani kama ni jambo rahisi kwa kizazi hiki cha wasanii kwa dunia nzima kuweka mipaka kwenye personal life style... vipi umewahi kufikiria juu ya branding na kujua diamond ameamua kui present brand yake kwa style ipi? ...... ukielewa hilo hutashangaa visanga na mambo yake!
 
Diamond hajaufikisha muziki wa Tanzania mbali, yeye anapiga Afro Beat ambao ni muziki wa Nigeria, hivyo anaendeleza pale walipofika Nigerians. He doesn't have a brand, yeye ni msanii muigizaji tu hata Kiba naye ni hivyo hivyo. Bongo fleva si muziki wetu hata siku moja, tuache kujidanganya.
 
Nothing lasts forever, wapi kina Olufela Olusegun Oludotun Ransome-Kuti ( Fela Anikulapo Kuti)?
Wapi kina Luambo Makiadi Franco?
Mwisho wetu u karibu kuliko mwanzo wetu.
Tubadilike, maisha Bila ya Yesu KRISTO ni ubatili mtupu.
Ni wakati sasa wa kutubu, kuokoka na kuiamini injili.
Na mie nikikwambia maisha bila ya Krishna ni bure kabisa utasemaje..?! Waislamu je? Na watu wa dini nyengine je?! Hizi ni story tu just live your life in a humanistic way to make a better world instead of kupeana story za kutenga humanity. On the other hand Olufela Olusegun Oludotun Ransome Kuti bado anaishi mioyoni mwa millions of his funs including me..! Every year kuna concerts kwenye majiji makubwa karibu yote duniani. Concerts hizo zinaitwa Felabration kumkumbuka gwiji, genius na baba wa music wa afrobeat..! Peace

Ubavu.
 
wewe wasema
 
Tatizo mtoa mada umeonesha upande, wala hujatoa uchambuzi umejitahidi kumpamba mmoja na kumchafua mwingine. Unataka kunambia hofu ya Mungu ipo kwa kutovaa hereni na mikufu pekee lakini hofu hiyo isiwe ya kuwa na mahusiano holela na kuwa na watoto lukuki mana kwa dini ya kiislam hao watoto tayari kuna haki ambazo watazikosa kutoka Kwa Baba yao kwa mujibu wa dini.
 
We Jay Z humjui Jay Z anavaa mlegezo sana (angalia show zake) na ana mikufu na micheni kama mia na kama hujui USA hamna labda rapper asiyevaa Micheni hayupo. Hao akina Rakhim, uncle Luc wasanii wa long wanapiga milegezo na micheni kama kawa (wanamiaka zaidi ya 55+). Huyo Prof Jay sababu ya ubunge lakini naye milegezo na micheni kaipiga sana, labda kama umezaliwa juzi (Hebu itafute nyimbo aliyoiimba juzi chafu tatu). Ila ni ujana tu akikua ataacha, hata huyo kiba Kuna picha moja kapiga na Bob junior kavaa hereni enzi hizo.
 
Diamond hajaufikisha muziki wa Tanzania mbali, yeye anapiga Afro Beat ambao ni muziki wa Nigeria, hivyo anaendeleza pale walipofika Nigerians. He doesn't have a brand, yeye ni msanii muigizaji tu hata Kiba naye ni hivyo hivyo. Bongo fleva si muziki wetu hata siku moja, tuache kujidanganya.

Turudi kwenye chakacha na Mnanda
 
Nothing lasts forever, wapi kina Olufela Olusegun Oludotun Ransome-Kuti ( Fela Anikulapo Kuti)?
Wapi kina Luambo Makiadi Franco?
Mwisho wetu u karibu kuliko mwanzo wetu.
Tubadilike, maisha Bila ya Yesu KRISTO ni ubatili mtupu.
Ni wakati sasa wa kutubu, kuokoka na kuiamini injili.
naam naam,hakika hakika mkuu,shetani ana nguvu sana duniani na kwakuwa alishapewa mamlaka..no way out watu wanajirahisisha na kumtii kile asemacho.

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom