Hii ndo hali ya Uchawi (Ushirikina) katika mchezo soka hasa watani wa Jadi

Hii ndo hali ya Uchawi (Ushirikina) katika mchezo soka hasa watani wa Jadi

Eti kinda, karibu mgeni wa jf, nimeijua kabla yako.
Turudi kwenye mada, acha imani potofu.
Nilimaanisha kinda katika mtazamo ndo maana hapo nikakuambia acha papara Jf ipo.

Lakini cha kushangaza umeibuka ohh naijua kabla, yote ya nini jenga hoja zenye mantiki wewe kinda.
 
Nilimaanisha kinda katika mtazamo ndo maana hapo nikakuambia acha papara Jf ipo.

Lakini cha kushangaza umeibuka ohh naijua kabla, yote ya nini jenga hoja zenye mantiki wewe kinda.
Acha Kwanza imani potofu ndo ujenge hoja. Kama mmeshindwa score goals ni mmeshindwa tuu hakuna uchawi wala nini.
 
Haya, hakuna uchawi kwanini? Elezea!
Uwezo wa mtu mmoja mmoja (wachezaji), team play, team tactical ndo vitu vinaweza kukupa matokeo. Ili umshinde mpinzani inabidi umzidi kwenye baadhi ya hivyo vitu
 
Mleta mada ni mshirikina full stop.
Kipindi Babu Tambwe akiwa Simba alikua akishangaa masuala ya ulozi yanayofanywa na timu pinzani hasa has a Ndala.. Lakini sasa kawa mshika tunguri.

Nanukuu kipande cha habari ya kipindi hicho...
Tambwe alisema tukio la kwanza lililomshangaza ni katika mechi kati ya Yanga na Mgambo JKT baada ya wachezaji wa Yanga kumtaka mwamuzi kumkagua mshambuliaji wa Mgambo, Mohamed Neto kwa madai kuwa alibeba hirizi.

Source: ‘Imani potofu zinaua soka’
 
Uwezo wa mtu mmoja mmoja (wachezaji), team play, team tactical ndo vitu vinaweza kukupa matokeo. Ili umshinde mpinzani inabidi umzidi kwenye baadhi ya hivyo vitu
Umeeleza namna ya kupata matokeo dhidi ya mpinzani hiyo ipo hivyo, baadhi ya wachezaji na viongozi hawapendi ushirikina na ndo lengo la timu ilivyoanzishwa.

Lakini ujanielewa nazungumzia ushirika kwamba pamoja na benchi la ufundi, kuna kikundi hapo hapo kina mambo yake kama wanavyosema baadhi ya wachezaji.

Kama ungeelewa hivyo tusingefika hapo
 
Watu wengine bhana kama bata hata uwalishe kokoto watahara tu.

Hivi wewe na Sunday nani anajua mpira. Ikiwa mimi sijui je unamshinda Sunday wewe aliyeelezea hapo?

Kwa akili kama zako za ndezi unadhani nimetunga ilhali nimekuwekea chanzo hapo..bata maji wewe.
Tatizo wengine hata mpira hawajui na hata timu ya kijiji hawajawahi cheza lazima wabishe
 
Kuna baadhi wanadai kuwa mpira hakuna uchawi wakasema na kwa namna Mji wa Sumbawanga ulivyotamalaki katika uchawi basi wangekuwa na Klabu ya Ligi Kuu. Na Nigeria wangechukua Kombe Kombe la dunia.

Akihojiwa na gazeti la michezo la Championi Golikipa wa zamani wa Yanga kwa sasa ni Kocha wa Makipa Juma Pondamali, alisema uchawi unatumika katika soka na yeye anauamini huku akisisitiza uchawi ni utamaduni wa mwafrika.

Kama hiyo haitoshi Nyota wa zamani wa mpira hapa nchini, Sunday Manara Computer, ambaye aliitwa Computer kabla hazijaja nchini kutokana na umahiri wake katika kusakata kabumbu.

Yeye wakati anahojiwa na Azam Tv kabla ya mchezo wa Simba na Yanga alisema kuna mambo ya utaalamu kwa wazee katika mpira wa miguu huku akitoa ushahidi kuwa katika Yanga kuna kitengo maalumu cha wataalamu ambapo wao kazi yao ni hiyo huwezi kuwakataza.

Kwa mukhutadha huo; Yanga walitumia wataalamu kuepuka kipigo kizito..tena kipigo kizito chenye kufedhehesha. Na namna walivyotumia ni hivi, kwa kuwa huwezi kuzuia mashuti yasije golini kwako basi unayadivert uelekeo mwingine.

Kwahivyo ili kufanya hilo mpira wa kwanza ukianza tu piga shuti uelekeo unaotaka basi kitakachofuata hapo mashuti ya mpinzani hayaendi ndani kwa maana kuwa goli..hapo itakuwa Deal done!
View attachment 884673View attachment 884674
Mbona mnaweweseka sana nyie Mikia. Mmekumbwa na jinamizi gani? Rudini Uturuki mkajifunze tena kucheza mpira!!!
 
Mbona mnaweweseka sana nyie Mikia. Mmekumbwa na jinamizi gani? Rudini Uturuki mkajifunze tena kucheza mpira!!!
Hivi kati Simba na Gongowazi nani wa kujifunza mpira. Embu jionee mwenyewe hapa.
IMG_20181002_204739_128.jpeg
 
Asante kwa kukiri kwamba kuna tatizo mahala. Na hilo kama tulivyoeleza kwenye Thread

Ukiachilia mbali magoli, kama mpira nimekufundisha namna unavyochezwa aisee!
Anayeweweseka ndiye akajifunze mpira, maana haiwezekana upige mashuti 10 on target Halafu usiingize hata Mpira mmoja golini. Ni dhahiri kuna tatizo mahala!!!
 
Hawa jamaa bila maushirikina ni weupe kweli.. Game ijayo hata wakienda kuweka kambi Gamboshi.. Kipigo lazima kiwahusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
hakuna kitu uchawi kwenye mpira
Lazima tujiamini kwa mbinu sahihi tunazotumia, hata kama wengine wanasema ni ujinga. Mchezo wowote, hasa wa mpira, ni mapambano ya kimwili, kiakili na kiroho. Kila jamii ina namna yake ya kutibu akili na roho za wachezaji wake kabla ya mechi muhimu, kadhalika kutibua roho na akili za wapinzani wao. Wazungu wanaiita hiyo saikolojia, na hata wanapofanya hadharani haiwi tatizo. Kwenye Fainali za Komba la Dunia la Ufaransa, kwenye kila mechi ilikuwa lazima beki wa Ufaransa abusu upara wa kipa Bartez. Ni kuwakuza imani yao na kuwaduwaza wapinzani. Lakini kitendo kilekile kikifanywa na timu zetu kinaitwa ushirikina. Kabla ya kila mechi, timu huwa zinaamshaamsha kwa kuweka duara na kutoa sauti ya pamoja ili kujenga ari ya wachezaji. Limeanzia New Zealand kwenye Rugby, ambako wachezaji walikuwa wakiigiza matambiko ya wenyeji asilia wa nchi hiyo, Wamaori.
Kuanza mpira kwa kuutoa nje hakukuanza leo, na hakutaishia kwa Ibrahim Ajib. Kwanza hajawa mbunifu kiasi hicho kwamba aje na kitu kipya asichopata kukiona popote kabla ya hapo. Mbinu hiyo inatumika sana na ina madhumuni tofauti. Moja ni kuharakisha kuingia mchezoni kwa kulazimika kuanza na kukomboa mpira uliotolewa nje. Na mkifanikiwa, ina faida ya kuuweka mpira kwenye ngwe ya wapinzani. Madhumuni mengine ya mbinu hiyo ni kuanza kwa kukumbushana kwamba ‘kazi imeanza, haya twendeni kazini’, lakini pia ina madhumuni ya kuwaduwaza wapinzani ambao badala ya kuzingatia walivyoagizwa na mwalimu wao, watapoteza umakini kwa kuhoji ‘ana maana gani kufanya vile?’. Lakini kwa timu inayoamini ushirikina kama Simba, ule kweli ni ‘uchawi’ dhidi yao, maana wachawi wao hawakuwahi kuwadokeza kuwa kitu kama kile kingetokea. Kwa maana hiyo, nakubaliana na Manara kwamba wameambulia pointi wasiyoitarajia shauri ya ‘uchawi’ ule!
 
Back
Top Bottom