Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Baada ya kuingia madarakani serikali ya awamu ya tano mwaka 2017 ililitangazia Taifa na dunia azma yake ya kurekebisha sekta ya madini nchini hususan dhahabu.
Ikaunda tume Mbili za Osoro na Mruma, zikaja na matokeo ya kitafiti na maazimio yaliyotikisa nchi.
Miongoni mwa matokeo hayo ni amoja na:
(1) kwa miaka yote ambayo Acacia amefanya kazi nchini wameunder declare madini wanayo chukua (yaani walikuwa wakichukua madini mengi kuliko wanayotuambia)
(2)Ukiachilia mbali dhahabu kwenye makinikia, walikuwa wakituibia madini mengine kama vile nickel, cobalt na rare earth metals
(3) Kwamba makadirio ya wizi huo ni takriban dola za kinarekani bilion 190, ambayo ni kama shilingi za Kitanzania zaidi ya Trilion 420 na ushehe
Serikali mwaka 2017 ikatunga sheria na ikaweka vitu vifuatavyo:
1. Makinikia yatakuwa hayasafirishwi nje ya nchi, makampuni yatatakiwa kuchenjulia hapahapa
2 Mikataba yote ya madini lazima ipitishwe bungeni
3. Kesi zinazohusu madini yetu lazima ziamuliwe kwenye mahakama za Ndani
Licha ya uwepo wa sheria hiyo ambayo profesa Kabudi alijitapa nayo sana lakini serikali yenyewe ikaivunjilia mbali kwenye makubaliano yake na Barrick kwa mfano:
(1) Barick wakaruhusiwa kuwa wanachukua makinikia na kuyapeleka nje
(2)Mkataba wa Barick na serikali haukuelekwa bungeni
(3) Mkataba wa Barick na serikali unawaruhusu kufungua kesi za migogoro nje ya Tanzania
Katika muktadha huo inashangaza kidogo
1. Kwanza unafahamu hawa watu wamekuibia zaidi ya Trilion 420, kwa nini ukubali settlement ya dola milion 300 tu, ambayo ni sawa na shilingi bilion 690 (0.69 Trillion), ambayo ni pesa mbuzi kulinganisha na Trillion 420?
2. Kama hawa unajua kuwa ni wezi na ushahidi unao, kwa nini uendelee kufanya nao kazi in the first place kwa nini tusidai matrillion yetu kwanza halafu tutafute watu honest tufanye nao biashara?
3. Kwa nii uvunje sheria zako mwenyewe ulizojiwekea ukiamini hizo ndo zitakazolinda utajiri wako?
Kutokana na maswali haya magumu si ajabu kuona CCM wanakwepa sana kuzungumzia ishu ya madini maana inawavua nguo
Kwa uchambuzi zaidi wa hili suala, angalia mahojiano haya, wameyaelezea vizuri sana hayo: