Tangu Uhuru ,tunatambaa hatusimami. Vinavyofanyika leo vilitakiwa vifanyike mwaka 1995. Ccm imetufikisha pabaya Sana. Hadi leo mji wa katoro uliopo jimbo la CHATO mkoa geita hauna maji Safi na salama. Miaka yote Jimbo hilo limekuwa ccm na mbunge wake miaka yote ni JPM. Huku Kamwanga,lwenge Nyamikoma kms 5 kutoka mji wa Geita hakuna umeme,hakuna maji,hakuna hata barabara ya vumbi,hakuna shule. Kutoka mji wa Geita kwenda mji wa kahama hakuna barabara ni zaidi ya kms 110. Chato wananchi wanachota maji ziwa Victoria. Wilaya ya bukombe,mbongwe, nyawhale,geita vijijini mkoa wa Geita hazina maji,hakuna km moja ya lami. Sasa ni miaka 50 tangu tupate uhuru. Ndipo CCM ilikotufikisha.