Hii ndondo ni utopolo mwingine nchi hii, inaamsha tamaduni za "kishenzi"

Hii ndondo ni utopolo mwingine nchi hii, inaamsha tamaduni za "kishenzi"

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Kwanza naomba nieleweke vizuri kuwa nimekosa neno sahihi la kutumia zaidi ya hilo "ushenzi"Neno ushenzi ni kinyume cha neno ustaarabu.

Kwa miaka mingi nchi zetu tumekuwa tukipambana na utamaduni huu wa ndumba " black magic" ambao huwa hauishii kufanya vitu vidogo vidogo vya kimazingaombwe kama tunavyoviona katika ndondo cup.

Mambo haya yanayopigiwa upatu na mtu anayejiita shaffih Dauda, clouds na wafanyakazi wao ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha sana, kwa kuwa wanarithisha utamaduni mbaya sana kwa kizazi hiki ambacho kilianza kuingia kwenye tamaduni za kistaarabu.

Kwa nini nauita utamaduni huu ni wa kishenzi?

Kama nilivyosema hapo juu,ni kuwa mambo haya hayaishii kwenye vitu vidogo tunavyoviona hapo, Bali kuna wakati watu hao watahitaji kutoa makafara hadi ya damu.

Na ukweli iwapo yatapata wadhamini, huenda wakaanza kutoa kafara za binadamu ili washinde. Watanzania hatujasahau mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Mambo haya tunayachukulia mzaha mzaha lakini maonyesho ya ndumba wazi wazi,ni hatua muhimu sana katika kuwazoesha watoto ambao wengine wanayachukulia kuwa mambo ya kishetani kitu ambacho ni kweli. Lakini kwa chombo kama clouds na waajiriwa wake wakiyapigia upatu,yanaonejana kana kwamba ni ya kawaida tu.

Binafsi siungi mkono ushirikina kwa namna yoyote. Mpira ni sayansi. Msitumie nguvu kukuza utamaduni wa kishenzi katika soka. Mtafanya baadhi ya watu wasiingie huko ijapo wanaweza kuwa na vipaji.
 
Back
Top Bottom