Hii ndoto inachanganya kichwa: Nimeota nimekoswakoswa kubamizwa na gari kwenye mti likaenda kuparamia nyumba ya watu

Hii ndoto inachanganya kichwa: Nimeota nimekoswakoswa kubamizwa na gari kwenye mti likaenda kuparamia nyumba ya watu

Mungu amekuepushia ajali ambayo ibilisi ameipanga kwako
 
Niliwahi kuota nipo kwenye coaster, kitonga moja ghafla coaster ikaacha njia inaingia korongoni hapo tupo juu kule, sijui kilichoendelea nlishtuka sana na kuamka hapohapo kama nimepigwa banzi la uso😂, mpaka sasa bado namtafuta yule dereva alietaka kutuchomoa roho😂 ama zake ama zangu.
 
Mkuu Kuna uwezekano ulikunywa maji baridi kabla ya kulala ama ulilala sehemu yenye ubaridi.
 
Unajulishwa kuwa kuna watu wanakufanyia uchawi lakini bado hawajafanikiwa wanachokilenga kukifanya kwako. Chukua hatua, na kama ni ndoto inayojirudiarudia usiipuuze.

NB: Kama hauamini uchawi upo basi amini kwamba ni ndoto tu kama ndoto zingine.
 
Huu ndio uwezekano mkubwa.
 
Kabla ya kukimbilia kwenye uchawi..
Kwanza nyumba unayo lala inapitisha hewa vizuri?..hauna malaria?au magonjwa? Unakula vizuri?
 
Back
Top Bottom