The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Abiria wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) maarufu mwendokasi wameelezea malalamiko yao baada ya moja ya mabasi hayo kuvuja maji wakati wa mvua jijini Dar es Salaam.
Katika video iliyosambaa mitandaoni, abiria walionekana wakitumia miamvuli ndani ya basi huku wengine wakieleza kusikitishwa na hali hiyo.
"Tuko ndani ya mwendokasi hapa, watu wana miamvuli na basi linavuja," alisikika mmoja wa abiria akisema na kuonesha hali ya kero inayowakumba wasafiri.
Abiria wengine pia walionesha hasira zao, wakieleza kuwa hali hiyo ni aibu kwa mfumo wa usafiri unaopaswa kuwa wa kisasa.
"Hii ni aibu," alisema mmoja wao, huku mwingine akiongeza:
"Watu wanalowa kwenye mwendokasi!"
Tukio hilo limezua mijadala kuhusu uimara wa miundombinu ya mabasi hayo, huku baadhi ya wananchi wakipendekeza ubinafsishaji wa huduma hiyo ili kuhakikisha ubora.
"Wabinafsishe tu, wanang’ang’ania nini?" alisikika abiria mwingine akisema.
Hili si tukio la kwanza kwa abiria wa mwendokasi kulalamikia matatizo ya mabasi hayo, ikiwemo msongamano, ucheleweshaji wa huduma, na sasa uvujaji wa maji.
Hali hii inaashiria hitaji la ukarabati wa mabasi na usimamizi madhubuti wa mfumo wa usafiri wa mwendokasi.
Wananchi wanaitaka mamlaka husika, hususan Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha mabasi yanakuwa katika hali bora na kuendana na viwango vya huduma za kisasa.