Hii ni aibu kubwa sana kwa Harmonize

Unastahili kupata nishani ya juu ya kusagia kunguni
 
Nimetizama kiclip nimeona anadaiwa mil 150, wakati kodi ni dola 800 kwa mwezi, sasa najiuliza 150m na Dolla 800 nahisi kama hamna uwiano na mda alio ishi hapo.

Ila Ok acha tuone mahakama zipo, mzee aende huko,huku ICU sizani kama watamsaidia as long ana nyaraka aende akadai hela yake kwa pilato.
 
Ukisikiliza vizuri kabisa swala sio kodi ingawa hawa kina Maimartha wamesema kodi ila huyo mzee anataka nyumba yake ikarabatiwe kwa madai kuwa Harmonize kaiharibu tofauti na alivyompangisha. Hivyo anadai kaita contractors watatu tofauti na gharama zimekuja hiyo milioni 150
 
Yule mmakonde naye kavu sana, sasa mpaka KY Jerry jaacha ndani ameshindwa jutupa kwenye dustbin?
 
Hivi kuna celebrity bongo ambae anamiliki nyumba kweli maana msanii wa bongo akifulia au kuugua sana ama kufariki mengi yanaibuka hata unakuta bima ya afya ya elfu 50 na mia 4 kwa mwaka hajawahi miliki. Hivi tukisema hawa wasanii wengi wanaishi kwa masharti ya sangoma tunakosea kweli??????
 
Okay sasa aende mahakamani sio kulialia kwenye TV.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…